Mzazi mwenzangu hahudumii mtoto; nataka nimpeleke mahakamani

Mzazi mwenzangu hahudumii mtoto; nataka nimpeleke mahakamani

Inawezekana ikawa ni lugha ya kejeli kwa jambo usiloendezwa nalo......kwa mfano mtu anapokuambia uuze simu ununue vocha.....
Naona unatumia nguvu nyingi sana kuwa nyuma ya huyo dada, hakuna lugha ya kejeli hapo ni wazi kabisa kaachwa na nyumba kama maelezo ya mtoa mada yanavyoeleza, kama asingekuwa na nyumba angesema hapa kwamba ananiambia niuze nyumba ambayo hata si yake au hatukuwa na nyumba
 
Wewe ni masikini wa kila kitu

Huwezi sikia mwanamke wa kichaga anafanya huo upumbavu wamezaliwa kupambana

Wewe Hadi mtoto wako huwezi mlea .je baba wa mtoto asingekuepo sa hio kafa?

We sijui kabila gani ila my self siwezi zaa na mtu ambae yeye Kama Yeye hawezi Lea mtoto bila Mimi..wewe ni mvivu inshort

Sisi wazazi wetu wamefanya kazi za kawaida sana hajawahi yumbishwa na baba wa mtoto kampeleka mwanae shule za gharama Hadi baba mtu anashangaa kwamba ipo siku atakwama ila wapi...chuo bila mkopo umetoboa Sasa wewe katoto hako kanakushinda😁 siku hizi hamna wanawake Kuna wadada wa kazi
Naomba msaada wa namna bora au mwanasheria atakayenisaidia kumpeleka mahakaman baba mtoto wangu ili angalau awe analipa ada tu.

Mtoto ana miaka 9 yuko darasa la nne siku zote nimekua nikimlipia ada na matumizi yote lakini safari hii hali imekua ngumu nimeshindwa na nimemuambia kiungwana tu kakataa kasema hana hela niuze nyumba nimlipie ada mtoto.

Alikua ni mtoto wa kwenye ndoa ila tuliachana kabla mtoto hajaanza shule.
 
Wanawakee mnakuwaga na maneno sana mkiachana , sasa hv mnatafuta huruma za watu.
Mimi nilitengana na mzazi mwenzangu mwaka 2019,aliniambia waz waz kuwa hana mpango na mimi na wala hataki mia yangu kwani mtoto atahudumiwa na babake mpya.Tenaakataka kubadili mpaka majina ya mtoto ili ampe huyo msengerema mwenzake.
Sasa hivi analalama sana kwa marafiki na jamaa zangu kuwa sihudumii mtoto.
 
Siku hizi humu jukwaani kumejaa watoto wadogo sana wanaotumia sehemu ndogo sana ya akili zao kujibu au kutatua mambo......utalifahamu hilo kupitia majibu yao.....

Kuachana na mwenza ni vitu vya kawaida kutokana na changamoto kadhaa ambazo pengine zimeshindwa kutatulika na wawili hao wakamua kwa amani na usalama kila mmoja aishi maisha yake......

Lakini kutengana na mwenza hakuondoi uwajibikaji wako kama mzazi juu ya mtoto au watoto wenu.....kwa maana ya kuhakikisha watoto au mtoto anapata huduma sitahiki kulingana na uwezo au kipato Cha mzazi wake.......

Vijana wengi wakichana na mwenza wanatoa sababu zisizo na kichwa wala miguu ili kuepuka uwajibikaji kama baba wa mtoto......na ndio maana mamlaka au taasisi zinazosimamia Hilo kwa manufaa na maslahi ya mtoto na sio mama.......

Unapoachana na mkeo jukumu la kumuhdumia mwanamke ndio linakoma hapo na linabakia la watoto au mtoto wako........

Ewe Binti kama una hakika uwezo wa kuhudumia kwa maana ya kipato anao basi fuata taratibu ili alazimishwe kufanya hizo na mamlaka kama ameshindwa kuwajibika kwa khiyari yake........

Guys hivi mnajenga taswira gani kwa watoto wenu hapo mbeleni angali anashuhudia mnavyokimbizana mahakamani au kwenye korido za ustawi wa jamii na mama yake ili kukulazimisha wewe kumhudumia......hivi unadhani mtoto atakuthamini kama baba.....??

Vijana msitumie mzigo wa malezi ya mtoto kama njia za kuwaadhibu wanawake mlioachana nao.....wajibika kama baba ili kuendelea kujenga uhusiano mzuri na watoto wenu.......maneno mabaya atakayolishwa na mama yake kwa hasira na visirani vinazimwa na matendo mema kwake..,....
Angalau tangu nimeanza kusoma Uzi, nimefanikiwa kuona Uzi wa mwanaume/baba/mzazi aliyefikiria Kwa busara.

Watoto wanapitia mateso mengi kisa kukomoana Kwa wazazi.
 
Loh pole sana

Usikwazike na majibu ya wanazengo wa humu

Kama upo Dar nenda pale Chang'ombe Mahakama kituo Junuishi ya Ndoa na mirathi. Kuna ofisi za WILDAF wanatoa ushauri mzuri kisheria kuhusu masuala aina hii.

Sheria inamtaka baba kugharimia matunzo ya mtoto hata kama mmeachana kisheria. Tatizo ninaloliona ni wamama wengi wamekuwa na moyo wa KUMUACHIA MUNGJ pale wanapokosa matunzo ya watoto.
Na mimi nilikua ni mmojawapo kuwa niliamua kupambana tu nilee mwenyewe ila sasa hali imekua ngumu sana naona nitashindwa ndiyo nikaamua nimshirikishe lakini mwenzangu naona hataki anataka kunikomoa tu kwahiyo naona nimpeleke mahakaman ili awe analipia huko na matumizi kabisa
 
Hahahaha mtoa mada hebu elezea kisa chenyewe si unaona watu wanataja kutoana damu!
 
Kwa nini mnafosi watoto wasome private schools kuanzia primary?

Kama hana pesa unadhani mahakama itamfunga?

Na btw kesi za namna hiyo haziendi mahakamani zinaenda ustawi wa jamii ambako sana sana mtashauriwa mumpeleke shule ambayo inaendana na kipato chenu..
Kusoma private sio kuwa ndio atakuwa na uwezo mkubwa darsani watu wanajifariji. Going out and buying expensive cigarettes doesn't make you rich
 
Naomba msaada wa namna bora au mwanasheria atakayenisaidia kumpeleka mahakaman baba mtoto wangu ili angalau awe analipa ada tu.

Mtoto ana miaka 9 yuko darasa la nne siku zote nimekua nikimlipia ada na matumizi yote lakini safari hii hali imekua ngumu nimeshindwa na nimemuambia kiungwana tu kakataa kasema hana hela niuze nyumba nimlipie ada mtoto.

Alikua ni mtoto wa kwenye ndoa ila tuliachana kabla mtoto hajaanza shule.

Ushasema Mzazi mwenzako, Malizana nae nasi tumalizane na wenzetu Wakati wa Conjugal neno Mahakama halikutajwa kabisa iweje leo ebo!
 
Kama hicho ndiyo kipimo chakp cha aii mimi akili ninayo binafis na siku zote nimekua nikimwambia mchukue mtoto ukae naye yeye hatak anasema mke wake hatak
Yaani mke wangu akatae kuishi na mwanangu. Sasa anachohitaji sio mie ama Ni Nani. Mana huyo mtt Ni mie pia Ina Mana akimkataa namie Ina Mana amenikataa hapo kesi hakuna
 
Huyu mwanamke si useme tu kuwa ni wewe mbona ndiye unayejibu hoja zote humu na Sheila kapotea??? [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787]
Mimi najibu hoja zisizo na matusi, zenye ushauri unaoendana na kile nilichouliza, kupoteza nguvu kubishana nimeshindwa
 
Si kakuaachia nyumba,Hela ya ada mwenzio kahamishia kwenye kodi.Cha msingi we dogo mpeleke Kayumba tu.Kama nyumba inawapangaji chukua kodi mtoto apate chakula.Hakuna kesi hapo.
Nyumba hajaniachia nimehangaika mwenyewe baada ya kuachika
 
Kwa nini asimpeleke Mtoto Kwa Baba yake?
Baba kamwe wala hatamuomba hata senti yake yoyote.

Kama Hana uwezo asilazimishe, shida ya wanawake wengi hutumia watoto kama kitega uchumi kwao.
Jambo ambalo wanaume wote Duniani hawawezi kuvumilia kitu Kama hicho.
Kwanini Mtoto atenganishwe na Mama ake??
Suala la kulea ni lenu nyote haijalishi mmeachana ama bado mpo pamoja
 
Na mimi nilikua ni mmojawapo kuwa niliamua kupambana tu nilee mwenyewe ila sasa hali imekua ngumu sana naona nitashindwa ndiyo nikaamua nimshirikishe lakini mwenzangu naona hataki anataka kunikomoa tu kwahiyo naona nimpeleke mahakaman ili awe analipia huko na matumizi kabisa
Naam
Upo sahihi.

Tatizo wavulana wa humu wanadhani hao watoto mliwapata kwa mikataba. Hawajui maana ya malezi ndo maana wanatoa majibu hanayoashiria kuwa hawakulelewa.

Kama hataki kutoa matunzo ya mtoto sheria zipo na zinamuelekeza atunze mtoto. Siyo jukumu la mama bali baba
 
Kwanini Mtoto atenganishwe na Mama ake??
Suala la kulea ni lenu nyote haijalishi mmeachana ama bado mpo pamoja

Kwani Kwa nini atenganishwe na Baba yake?

Kama swala ni Kulea wote basi mwenye uwezo wa kutoa matunzo ndiye asikilizwe wapi mtoto akasome, achague shule.

Tatizo la wanawake wengi wakiachwa wanadhani wananafasi Ileile waliyokuwa nayo Kwa mwanaume Fulani.
Akiona watoto wa mke mpya wanapelekwa International school Naye anataka wakwake naye apelekwe ilhali hajui kuwa wenzake wamepanga na sio ajabu mke mpya ndiye anayegharamia sehemu ya Ada Kwa watoto.
 
Back
Top Bottom