Siku hizi humu jukwaani kumejaa watoto wadogo sana wanaotumia sehemu ndogo sana ya akili zao kujibu au kutatua mambo......utalifahamu hilo kupitia majibu yao.....
Kuachana na mwenza ni vitu vya kawaida kutokana na changamoto kadhaa ambazo pengine zimeshindwa kutatulika na wawili hao wakamua kwa amani na usalama kila mmoja aishi maisha yake......
Lakini kutengana na mwenza hakuondoi uwajibikaji wako kama mzazi juu ya mtoto au watoto wenu.....kwa maana ya kuhakikisha watoto au mtoto anapata huduma sitahiki kulingana na uwezo au kipato Cha mzazi wake.......
Vijana wengi wakichana na mwenza wanatoa sababu zisizo na kichwa wala miguu ili kuepuka uwajibikaji kama baba wa mtoto......na ndio maana mamlaka au taasisi zinazosimamia Hilo kwa manufaa na maslahi ya mtoto na sio mama.......
Unapoachana na mkeo jukumu la kumuhdumia mwanamke ndio linakoma hapo na linabakia la watoto au mtoto wako........
Ewe Binti kama una hakika uwezo wa kuhudumia kwa maana ya kipato anao basi fuata taratibu ili alazimishwe kufanya hizo na mamlaka kama ameshindwa kuwajibika kwa khiyari yake........
Guys hivi mnajenga taswira gani kwa watoto wenu hapo mbeleni angali anashuhudia mnavyokimbizana mahakamani au kwenye korido za ustawi wa jamii na mama yake ili kukulazimisha wewe kumhudumia......hivi unadhani mtoto atakuthamini kama baba.....??
Vijana msitumie mzigo wa malezi ya mtoto kama njia za kuwaadhibu wanawake mlioachana nao.....wajibika kama baba ili kuendelea kujenga uhusiano mzuri na watoto wenu.......maneno mabaya atakayolishwa na mama yake kwa hasira na visirani vinazimwa na matendo mema kwake..,....