Mzazi mwenzangu hahudumii mtoto; nataka nimpeleke mahakamani

  • Siku ukitumia akili zako bila kushikiwa naakina Joyce Kiria utapata mafanikio.
  • Wanaume si maduwanzi kiasi hicho! Ukitumia mbinu hiyo unapotezwa asubuhi sana!
  • Kuna mwenzako huku mtaani kwa ujinga kama huo mtoto hajasajiliwa mtihani wa taifa.
 
[emoji38][emoji38][emoji38]kwamba wewe ni maskini
 
Wengi wako hivyo,
yakibuma huko wanarudi kutia huruma
 
Utaharibu zaidi,
Kesi za hivi wasiliana na wazee (wazazi) wake, ukienda mahakaman umetangaza vita
 
Na akienda mahakamani sheria inasema mtoto kuanzia miaka saba anaweza kaa na baba yake,hvo utaambiwa kama umeshindwa kukaa nae mpeleke kwa baba yake.
 
Hawa viumbe ni kuishi nao kwa akili sana kwa kifupi najiona kabisa nakwenda kuitwa baba jina ( sio muwajibikaji kwa haya yanayotokea ).Ukikua mwanangu utakuja nikumbuka na utanitafuta .
 
Ukome inaonekana mwanzoni ulimuacha uyo mume kwa dharau ukijua utaweza mambo yote peke yako.
 
Kweli kabisa yani hakuna mwanaume Ambaye hataki kulea mtoto lakini shida ni mama zao miyeyusho sana
 
Single mothers hata umpe mshahara mzima hakosi cha kulalamika. Utasikia anakusemelea kwa ndugu eti kaka yenu akipiga simu kuongea na mtoto anaongea dakika moja tu anakata. Yani wanajifanya wanayaweza alaf wakienda huko wakakuta ndivyo sivyo wanaanza kulia lia
 
Mnhhh....nyumba kuachiwa na ada ya mtoto ni vitu tofauti...umeamua tu kuwa mbishi...kisa mnadhani huyo mama anafaidi sana kwa mtoto kukaa nae..men are soo selfish at times..sijui kwa vile hamzai?
Sorry to say this.. huna akili na acha kumpotosha mwenzio.
 
Mtoa mada, kwakuwa mtoto ana miaka 7+ na endapo Baba atamchukua mtoto wake. Umewaza mstakabali wa hiyo nyumba aliyoacha Baba mtoto
 
Halafu kingine kujazia nyama, wadada wengi wanadhani ustawi kunabase upande mmoja. Ila siku hizi hao ustawi wanajionea vituko vya wadada, mambo yamebadilika wengi wanaangukia pua.
 
Fanya kazi kwa bidii, mhudumie mtoto ako wewe mwenyewe.
Usimsumbue wala kugombana nae kweny simu.
Akipiga simu ongea vzuri na usilalamike
Jipende na upendeze.
Ataanza kukufuatilia alaf badae atataka kujua mbona siku hzi upigizani makelele, hulalamiki utamwambia umechagua furaha.
Hapo atakua kwenye mabano atataka ajue hiyo furaha ni nin.
Mengine utajiongeza siwez sema kila kitu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…