Mzazi mwenzangu hahudumii mtoto; nataka nimpeleke mahakamani

Wewe unamponza mwenzio, nyumba so kaachiwa??.... Apambane na Hali yake, hiyo Hela ya kutafuta wanasheria wa kukutetea kamalizie ada ya mwanao huko ingilishi midiam, au kuondoa mzizi wa fitna mpeleke mtoto Kwa baba yake asome huko huko baba ataamua shule ya kumpeleka mtoto wake usimlazimisheee!!!! Usikute ni wivu tu unamsumbua baada ya kuona Kuna mwanamke mwenzie analamba asali aliyoimwaga yeye.
 
Vipi Kama Baba wa mtoto au wakili wake akimuuliza Hilo swali unazani atakuwa na uwezo wa kulijibu?
Honestly sidhani...ila pia sidhani kama watamuuliza, sababu hio mentality shule za private ni nzuri kwa watoto haipo kwa watu ambao watakuwepo hapo mahakamani peke yake....hili ni jambo lipo hata wakitoka kupata chai nje ya mahakama...
 
Mtoto alelewe na mama wa kambo wakati nipo...????

Siwezi kukujibu utoto wote ulioandika hapa.....

Again kama mzazi una uwezo na hutaki kupeleka mtoto wako English Medium school kisa humpeleki unadhania kwa kufanya hvyo unamkomoa mama yake, then wewe ni dume suruali tuu...no better word to describe you!
 
Mnhhh....nyumba kuachiwa na ada ya mtoto ni vitu tofauti...umeamua tu kuwa mbishi...kisa mnadhani huyo mama anafaidi sana kwa mtoto kukaa nae..men are soo selfish at times..sijui kwa vile hamzai?
 
Acha ngonjera, hayo ma-slay and drama queens lazima wajifunze in a hard way.
 
Honestly sidhani...ila pia sidhani kama watamuuliza, sababu hio mentality shule za private ni nzuri kwa watoto haipo kwa watu ambao watakuwepo hapo mahakamani peke yake....hili ni jambo lipo hata wakitoka kupata chai nje ya mahakama...
Akienda mahakamani kwa hoja ya kupewa Ada ya mwanae kesi anapoteza kwa nock out mapema sana maana elimu ni bure. Akienda kwa hoja ya matunzo ya mtoto anaweza kuishia kupewa 30k kwa mwezi au anapoteza kesi na mtoto kabisa maana dogo kashafikisha miaka 8+ Sheria inamruhusu Baba kukaa na mwanaye .In short Hana pa kutokea akizubaa mume anaweza akasema wauze nyumba wagawane Mali ambapo itakua hasara kwake.
 

Unaona ulivyocherema😂

Kwa hiyo mtoto alelewe na Baba WA kambo wakati Baba yake mzazi yupo sivyo,

Wanawake macherema Kama ninyi mnatakiwa Mungu awape wanaume dizaini yangu ili akili ziwakae.

Mahakamani au ustawi wa jamii, usifikiri kuna watu wajinga wajinga Kama wewe.

Hoja mwanaume atazozitoa
1. Mtoto anamiaka 9 hivyo anaweza kuishi na Baba. Hata sheria zinaeleza.
2. Mpaka tunafika hapa Mama yake(wewe) ameonyesha Hana uwezo wa kuendelea kumtunza Mtoto kutokana na mahitaji ya mtoto kuongezeka. Hivyo naiomba Mahakama au Ustawi Kwa ruhusa yenu mniruhusu nimchukue mwanangu nimlee mwenyewe. Atakuwa anaenda kumsalimia Mama yake.
Pia sitamuomba Mama yake pesa yoyote ya kumuangalia mtoto.

3. Kutokana na matukio ya ulawiti kushika Kasi, mtoto wangu nahofia kulelewa na Baba WA kambo. Wote tunajua dunia imebadilika.

4. Nafikiri mtoto nikimlee itamrahisishia Mama na taifa letu kupata mtoto Bora kwani nitamuandaa kama wenzake kufanya shughuli ndogondogo za Ujuzi
Watoto wenzake waliopo pale NYUMBANI kila mmoja anamradi wake anaousimamia, kuna anayefuga kuku, mwingine Bata mzinga, hivyo wanajenga Ujuzi hata pesa ya matumizi siwapi wanazitolea kwenye miradi Yao.
Mtoto wangu huyu Naye atakuwa kama wenzake tena hiyo pesa anaweza msaidia hata mama yake.

5. Mtoto nikimlea Mimi wala hatutarudi tena hapa ustawi wa jamii au mahakamani kuwasumbueni. Kwani mahitaji yake na haki zake zitalindwa Kwa ukaribu zaidi kuliko akiwa mbali nami.

6. Mama yake Hana kazi inayomtosheleza kumhudumia huyu mtoto.

7. Mama yake anakosa fursa ya kuolewa na kutukanwa kuwa ni single mother kisa mtoto wangu. Ni bora nimchukue mwanangu ili kumpunguzia adha na masimango kutoka Kwa jamii.
Ndugu Hakimu, au afisa ustawi sote tunajua ilivyongumu Kwa Mwanaume kuoa single mother, ndio maana Kwa kumsaidia mwenzangu ili apate mtu mwingine nimeonelea mahakama iniruhusu nimlee mwanangu

8. Tunawapa mzigo watu wasiohusika.
Kwa nini mtoto wangu awe mzigo Kwa Baba yake wa kambo ilhali Mimi nipo, pesa kuigawanya ni ngumu ndio maana naomba mwanangu ajumuike huku na apunguze mzigo Kwa Baba WA kambo. Wote tunajua maisha ni magumu
 
Mnhhh....nyumba kuachiwa na ada ya mtoto ni vitu tofauti...umeamua tu kuwa mbishi...kisa mnadhani huyo mama anafaidi sana kwa mtoto kukaa nae..men are soo selfish at times..sijui kwa vile hamzai?
Nikuambie tu ukweli huyo dada anajua vizuri kwamba na yeye atafaidika, sio suala la selfish, kwa sababu kitendo Cha mwanaume kumuachia nyumba mwanamke ambaye ndoa Yao imedumu muda mfupi maana yake anajali ustawi wa mtoto wake, na haya yanazungumzwa hapa yamkini yako katika uhalisia huo japo mtoa mada hajataka kufunguka, kama mama anataka mwanae asome shule bora na anaamini Mzazi mwenzie ana Maisha mazuri ampeleke mtoto Kwa baba yake huko Baba ataamua mwanae asome shule gani hakuna Mzazi ambaye hapendi mwanae asome pazuri na uwezo anao, hebu jiulize kwanini huyu dada anakimbilia mahakamani?? Anajuafika kwamba mahakama itakuwa upande wake na itamuamuru baba alipe na Hela ya matunzo hapo mama atapata faida na kama mwanaume huyo anaishi na mwanamke hapo usijefikiri mama mtoto anamkomoa mwanaume no hapo analenga kumkomoa mwanamke mwenzie anayelamba sukari, swali la kujiuliza unafikiri huyo baba huko Hana watoto wengine na je ikithibitika anawatoto wengine ambayo wanamtegemea hiyo mahakama Bado itamlazimisha apeleke mtoto ingilishi midiamu??? Msitafute huruma kupitia watoto, huyo Mtoto hakubakwa alikubali Kwa Moyo mweupe na kumtunza amtunze Kwa Moyo mweupe hivyoo hivyo bila kutafuta sababu na visingizio
 
Mmepeleka shule za kulipia mtoto ili nini? Mnavurugaga mambo wenyewe halafu unadhani utamsumbua mtu? Mahakama hata ikiamua, utakutana na pesa ndogo tu kulingana na kipato chako na majukumu mengine aliyo nayo vitagawanywa, bado utaendelea kulalamika tu, the way atapewa mtoto wake amchukue kisheria na hatashindwa.

Wanawake wengi hutibua ndoa na kuwatumia watoto kama siraha ambayo hainaga risasi za kutosha
 
Shida hapa ni kujua yupi ni tatizo kati yako na yeye. Maana inaonekana mliachana kwa shari mpaka akakuachia na nyumba, bado na yeye ana maumivu. Nikushauri tu kama ana pesa kukuzidi/mtu mwenye uwezo kifedha, jaribu kutumia hekima katika kudai hiyo pesa ya ada isije mwisho wa siku ukajutia maamuzi ya kumpeleka mahakamani. Pesa ina nguvu sana.
 

Baba alivyomwacha mtoto kwa mama yake hakujua kuna ulawiti sijui mambo gani..unandika mambo ya kufikirika ......Kwa kheri.
 

Yaani kumsomesha mtoto ni mpaka awe kwa baba yake?? ndio maana nikasema mko selfish, mnaona huyo mama anafaidi sana.... kama anaona ugumu si atoe ada shuleni moja kwa moja???
 
Baba alivyomwacha mtoto kwa mama yake hakujua kuna ulawiti sijui mambo gani..unandika mambo ya kufikirika ......Kwa kheri.

Alimuachia mama Kwa sababu Mama yake alizuia, pia sheria inakataza mtoto chini ya miaka 7 anahaki kupata malezi na upendo WA Mama.
Labda Kwa Hali ya dharura tuu.

Ninyi ndio mnaafikiria vitu ambavyo havipo. Kisa umezaa tuu basi unaona kila kitu ni Haki Kwa mwanao, Acheni uchizi.
Sio wewe Tu uliyezaa mwanaume uliyemzaa Naye anawatoto Kama wako Kwa wanawake wengine Kama wanne hivi.

Kwa heri
 
Yaani kumsomesha mtoto ni mpaka awe kwa baba yake?? ndio maana nikasema mko selfish, mnaona huyo mama anafaidi sana.... kama anaona ugumu si atoe ada shuleni moja kwa moja???

Aliyechagua shule ndio alipe Ada.
Mbona unashindwa kuelewa mambo madogo.

Yaani kuna wanawake ukizaa nao inakuwa Kama umezaa na mwendawazimu.

Shule uchague wewe alafu mwanaume uliyezaa Naye alipe Ada. 😂😂
 
Yaani kumsomesha mtoto ni mpaka awe kwa baba yake?? ndio maana nikasema mko selfish, mnaona huyo mama anafaidi sana.... kama anaona ugumu si atoe ada shuleni moja kwa moja???
Nakuambiaje Tena, hizo hoja za uselfish mahakamani hazipo mwambie shost yako asiende mahakamani aendelee tu kukomaa maana atapoteza Kila kitu na uhalali wa kukaa na huyo mtoto, maana Mtoto ana miaka 9 anaruhusiwa kwenda Kwa baba yake, baba ndo ataamua mwanangu asome wapi ssio mnajichulia tu uamuzi halafu mkimbilie mahakani kisa mnatetewa, mnavuruga Ili mje na hoja za ustawi wa mtoto
 

Yes kila kitu ni haki kwa mtoto,...una watoto watano,kumi it doesnt matter unatakiwa uwahudumie wote ipasavyo, sio kwa sababu uko bitter umeacha nyumba na aliyekua mkeo ana mtu mwingine then uhudumie watoto wengine huyu umuache,

Na kisha huyu mtoa mada sio mjinga kutokujua hapa hakuna pesa....

Mtoto ulawiti sijui nini hata akienda kwa baba anaweza kuwa vulnerable..ndio maana nikasema umeandika vitu vya kufikirika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…