Kuna maswali ya kukuuliza hapa,
*Je, mlijadiliana na baba yake wapi huyo mtoto akasome, iwe private school au serikalini?
*Kama mlijadiliana, alikubali na mkakubaliana atakuwa na uwezo wa kulipia kiasi gani kwa mwaka?
*Kama alisema hana uwezo wa kumpeleka mtoto shule ya private, je ulifanya maamuzi ya kumpeleka huko mwenyewe?
Nauliza hivi kwa sababu haya mambo sio ya kujifanyia bila makubaliano. Kama jamaa hana uwezo wa kumpeleka mtoto shule ya 2m, wewe ukang'ang'ania huko kwa show off za wanawake walio wengi, kosa ni lako. Kama mlikubaliana basi ana makosa na anawajibika kumsomesha shule mliyokubaliana.
Humu watu wana makasiriko sana, hizi issues hatuombi zimkute mtu ila that's part of life, kuachana kupo japo hatuombei hivyo, shida ni jinsi mtakavyoishi na kumlea mtoto huku mkiwa separate.
Kingine, hizi ni issues za ustawi wa jamii, huko mahakamani nilidhani mnaenda kutengua(talaka) ndoa tu na kuweka misingi ya malezi ya mtoto.