Mzazi mwenzangu hahudumii mtoto; nataka nimpeleke mahakamani

Mzazi mwenzangu hahudumii mtoto; nataka nimpeleke mahakamani

Comments nyingi za kwenye Uzi huu zinasiktisha na kuhudhunisha na wakati huo huo zinakupa picha kamili za aina ya kizazi Cha vijana wa kiume kwa nyakati hizi......na pia inatoa fursa kwa mabinti kuona uhalisia wa aina ya vijana na kufanya mamuzi sahihi.........

Na ndio mambo kama haya ndio yanayowasukuma wanawake kudai usawa kwenye jamii vile vile kufanya wanawake watamke wazi kuwa kazi ndio mume wake........
 
Mkuu, kuna gap kubwa sana ya uelewa kati yetu. Hiyo story ni one sided, with little or no facts, hatuwezi kuongea mambo mengi kama vile watu wa ustawi wa jamii. Atueleze kwanini kaachwa na kutekelezwa
Hakika ndugu ngoja tuache kama ilivyo lakini katika uhalisia kwenye jamii zetu Hilo jambo limetamalaki sana.......na ndio jambo ambalo limeamsha hisia za chuki kwenye mjadala huu huku kila mmoja akichukua upande wake.........
 
Bab si anatakiwa awajibike kwenye malezi.

Lakini sio malezi ya kupangiwa na Mwanamke tuliyekwisha kuachana naye.

Yaani achague shule ya gharama Mimi ñilipe,
Mtoto akiumwa achague Hospitali ya gharama Mimi ñilipe tuu, kisa malezi ya Baba. Never ever.

Mimi ndiye Baba, nachagua wapi mtoto wangu asome kulingana na uchumi wangu, Kama mama yake anauchumi zaidi simkatazi kumpeleka shule atakayo. Lakini sio anipe Misalaba ya kipuuzi nami nimuendekeze. Hilo halipo. Hata aende Kwa Nani.

Nina watoto wengi asifikiri kuwa nina huyo mmoja wa kwake
 
Unaona ulivyochenga sasa.
Ndio maana nikakumbia wengi wenu akili ni chenga, mnawatia aibu wanawake wenye akili ambao ni wachache.

Sasa Kama umechagua wewe international school si ulipe ADA. Kuna aliyekuzuia.

Ukishakuwa nje ya Mfumo wa mwanaume huna haki Kama Mke, mke aliyepo kwenye ndoa ndio anaweza kumshawishi mume wake tena Kwa majadiliano ya adabu kuwa Mtoto asome wapi.

Sasa ukishakuwa mpita njia huna hiyo Haki. Anayeangaliwa ni mtoto sio Kauli ya Mama yake(wewe).

Anayejua uchumi wa Mwanaume ni Yule mke WA ndoa anayeishi ndani ya mwanaume sio wewe WA nje huko.

Sijui wapi hamuelewi

Irrelevant.
 
[emoji23][emoji23][emoji23]
Limwanaume suruali ndio limekuzalisha kumaanisha na wewe ni hamnazo tuu!

Sio lazima mtoto aende Private,

Yaani ukifika Mahakamani au ustawi wa jamii usijeongea mambo ya kipuuzi kama hayo Utaonekana kichwani ni chenga/cherema.
Ustawi wataona ndio maana uliachwa Kwa akili matope.

Mtoto anamiaka 9 amekushinda peleka Kwa Baba yake. Hutaki lea uwezavyo.

Mnajifanya mnaupendo Kwa watoto kumbe ujinga na upumbavu tuu.

Tangu lini upendo ukazidi Uwezo Kama sio akili za kijinga.

Baba yake labda anawatoto WA nje wengine wanne unafikiri ustawi wa jamii atasemaje,
Kipato changu ni 500,000 Kwa mwezi ninawatoto WA NNE, uwezo wangu ni Kutoa elfu 60.
Kama ataiona ndogo anipe mwanangu nilee.

TATIZO Lenu wanawake mnadhani nikizaa na wewe basi kwengine sina watoto. Hivyo unadhani mtoto wako ndio spesho.

Mtoto anayefaidi pesa ya Baba yake mara nyingi ni Yule anayetoka Kwa mwanamke anayejielewa/anayemheshimu Mume
Unaongea maneno ya mwisho.
 
Lakini tujiulize, hadi mwamba kuamua kuachia nyumba ili bimama aishi na mtoto inamaana jamaa yupo mstari wa mbele kutimiza majukumu yake. Kuna kitu huyu bimama hajakiweka wazi, akiwa muwazi tunaweza kufumba midomo.

Bahati mbaya wanaoleta nyuzi za hivi kuna vingi wanaficha, hawawi wazi coz wana makandokando mengi.

Huyu mwamba anaonekana kutimiza wajibu wake, hadi nyumba kakuachia...uwe mjinga sasa uiuze ili dogo aende english medium school. Utakuwa mbatata ya marikiti kule mchambawima.
 
Watu tozo, mafuta Bei juu halafu mtu analeta habari za ada milioni na ushee halafu amejipangia mwenyewe na form ya kujiunga kaifuata mwenyewe hajatumwa na mtu sinamejipima huyo kuwa anaweza
Ha ha ha...
Hawa wanawake wa kisasa (feminist) Ni Changamoto Sana mkuu,

Huenda ndo aling'ang'ania ndoa ivunjike, kisingizio Kuna kijikazi kinampa kiburi mpk mtoto kapeleka shule za gharama. Jamaa kamuachia Hadi nyumba.

Kasahau
Kuna kupata na kukosa,
kijikazi kilichompa kiburi kimeota mbawa. Anarud kwa jamaa kudai ada.

Hata ningekua Mimi,
Ningekukaushia, sema najua jamaa anafanya for good Ila adabu iwepo.
Sio kwamba anamchukia mwanae
 
Mafurushi wenzie wanacoment takataka tu kama huyo furushi mwenzao. Kuachana kwenu hakupaswi kulipwa na mtoto wenu, mnapaswa kutafuta namna bora ya kumlea huyo mtoto maana hakuwaomba mumzae.

Kwanza kitendo cha nyie kuachana tayari ni doa kwenye maisha yake then bado mnamuongezea stress kwa upuuzi. Hebu muwapimage akili haya mafurushi kabla hamjaolewa nayo wala hamjayazalia.
Mbona unakuwa mkali hivo?
 
anyway fuata taratibu utapata stahiki yakoo
Apambane na hali yake tu! amtafute Nani????! me wa siku hizi atakwambia kazi hana, huko Mahakamani ataenda atawaambia mkitaka,mnipe kazi au nifungeni kazi sina! wakili atakula hela dem weeee! kuliko karo!
 
Hapana Ndugu...Mimi kwa mtazamo jawabu hilo halitoshi kuwa jibu la baba muwajibikaji kwa mtoto wake..... Hilo ni jibu fupi kwa mtu asiyependa kufanya kile alichoambiwa afanye.....ukipima uzito jambo lililo mbele yake na jibu alilotoa.......

Sasa mama atauzaje anayoishi yeye na mwanae kwa ajili ya kulipa tu ada....??

Na kama unapitia wakati mgumu kifedha si mambo ya kuzungumza na mwenzio kuamua hatima nyingine ya masomo na mustakabali wa mtoto wenu kwa pamoja.....??
Yani MTU umuachie Nyumba halafu akulazimishe umtumie ada ya Shule Binafsi? Akienda kulipa anamdanya Mtoto kuwa yeye ndio amelipa na baba yake amemtelekeza hamjali!! Watoto Hao wanaosomeshwa Vizuri na baba zao wakilelewa na akina mama wapumbavu wanakua hatari sana baadae kwani wanadanganywa kuwa ada ya mamilioni alikua anatoa mana Kwa vikoba na kuuza vitunbua kumbe ni uongo.

Kifupi tu kama Mtoto amemshindwa basi amkabidhi Mtoto Kwa baba yake na apangishe Nyumba yeye Yuko huru kuolewa na MTU Mwingine Maisha yasonge mbele
 
Unaona ulivyocherema[emoji23]

Kwa hiyo mtoto alelewe na Baba WA kambo wakati Baba yake mzazi yupo sivyo,

Wanawake macherema Kama ninyi mnatakiwa Mungu awape wanaume dizaini yangu ili akili ziwakae.

Mahakamani au ustawi wa jamii, usifikiri kuna watu wajinga wajinga Kama wewe.

Hoja mwanaume atazozitoa
1. Mtoto anamiaka 9 hivyo anaweza kuishi na Baba. Hata sheria zinaeleza.
2. Mpaka tunafika hapa Mama yake(wewe) ameonyesha Hana uwezo wa kuendelea kumtunza Mtoto kutokana na mahitaji ya mtoto kuongezeka. Hivyo naiomba Mahakama au Ustawi Kwa ruhusa yenu mniruhusu nimchukue mwanangu nimlee mwenyewe. Atakuwa anaenda kumsalimia Mama yake.
Pia sitamuomba Mama yake pesa yoyote ya kumuangalia mtoto.

3. Kutokana na matukio ya ulawiti kushika Kasi, mtoto wangu nahofia kulelewa na Baba WA kambo. Wote tunajua dunia imebadilika.

4. Nafikiri mtoto nikimlee itamrahisishia Mama na taifa letu kupata mtoto Bora kwani nitamuandaa kama wenzake kufanya shughuli ndogondogo za Ujuzi
Watoto wenzake waliopo pale NYUMBANI kila mmoja anamradi wake anaousimamia, kuna anayefuga kuku, mwingine Bata mzinga, hivyo wanajenga Ujuzi hata pesa ya matumizi siwapi wanazitolea kwenye miradi Yao.
Mtoto wangu huyu Naye atakuwa kama wenzake tena hiyo pesa anaweza msaidia hata mama yake.

5. Mtoto nikimlea Mimi wala hatutarudi tena hapa ustawi wa jamii au mahakamani kuwasumbueni. Kwani mahitaji yake na haki zake zitalindwa Kwa ukaribu zaidi kuliko akiwa mbali nami.

6. Mama yake Hana kazi inayomtosheleza kumhudumia huyu mtoto.

7. Mama yake anakosa fursa ya kuolewa na kutukanwa kuwa ni single mother kisa mtoto wangu. Ni bora nimchukue mwanangu ili kumpunguzia adha na masimango kutoka Kwa jamii.
Ndugu Hakimu, au afisa ustawi sote tunajua ilivyongumu Kwa Mwanaume kuoa single mother, ndio maana Kwa kumsaidia mwenzangu ili apate mtu mwingine nimeonelea mahakama iniruhusu nimlee mwanangu

8. Tunawapa mzigo watu wasiohusika.
Kwa nini mtoto wangu awe mzigo Kwa Baba yake wa kambo ilhali Mimi nipo, pesa kuigawanya ni ngumu ndio maana naomba mwanangu ajumuike huku na apunguze mzigo Kwa Baba WA kambo. Wote tunajua maisha ni magumu
Taikon wa fasihi.
Mtoto akiwa kwa baba huwaga wanawake nao wanatumaga pesa ya malezi?
 
Taikon wa fasihi.
Mtoto akiwa kwa baba huwaga wanawake nao wanatumaga pesa ya malezi?

Uliwahi sikia kesi ustawi WA jamii au mahakamani kuwa Mwanaume kaenda kushtaki mama watoto hamhudumii Mtoto? Jibu ni hapana.

Wanawake hawatumi na wala hakuna sheria inayowabana watume.
Ingawaje wapo wanawake wanaowatumia watoto wao pindi wakikua/wakijitambua
 
Katika maandiko matakatifu Mungu ameseama anachukia kuachana,consequences za kuachana huwa ni nyingi sana hata kama mna pesa kiasi gani,nasema kila siku humu maisha ya ndoa bila ya kuwa na Mungu usitegemee muujiza,kama ikiwezekana mrudiane au tafuteni amani,lakini kama mnaendelea kuvimbishiana vifua utashuhudia maumivu mengi sana na hilo unalopitia ni moja wapo.....
 
Naomba msaada wa namna bora au mwanasheria atakayenisaidia kumpeleka mahakaman baba mtoto wangu ili angalau awe analipa ada tu.

Mtoto ana miaka 9 yuko darasa la nne siku zote nimekua nikimlipia ada na matumizi yote lakini safari hii hali imekua ngumu nimeshindwa na nimemuambia kiungwana tu kakataa kasema hana hela niuze nyumba nimlipie ada mtoto.

Alikua ni mtoto wa kwenye ndoa ila tuliachana kabla mtoto hajaanza shule.
Ilibidi wakati mnaachana mambo matatu kama mliachana mahakamani kwa kupewa talaka. 1/ talaka 2/ mgawanyo wa mali 3/ matunzo ya watoto kama wapo.
Kwa ushauri wa hitaji lako nenda ofisi ya kata kwa afisa maendeleo ya jamii kuhusu lalamiko lako. Ikishirikiana hapo kupata suluhu ndipo utaenda baraza la kata au mahakamani
 
Kuna mwingine nae alishauriwa vibaya na wenzake, jamaa anampa 100k kwa mwezi, kampangia chumba ili mtoto apate pa kulala. Yule mwanamke akaona haitoshi bora aende ustawi wa jamii ili matunzo yaongezwe as aliona jamaa anapesa so ana wajibu wa kumhudumia yeye na mtoto, poor that girl.

Kafika ustawi akaulizwa unapewa kiasi gani, kasema 100k, malazi ya mtoto analipa baba yake. Akaulizwa unajishughukisha na nini kajibu hana kazi kwa sasa, kaambiwa TAFUTA KAZI. Jamaa kwa hasira akasema nina uwezo wa kutoa 50k kila mwezi na sina uwezo tena wa kulipia chumba. Ikapita hivyo, bidada akaambiwa arudishe mtoto kwa bibi ili hiyo 50k iwe inatumwa huko kila mwezi.

Watu mnadhani huko ustawi ni roller coaster sio.?
Hela imepungua tena duuh.
 
Back
Top Bottom