Mzazi mwenzangu hahudumii mtoto; nataka nimpeleke mahakamani

Comments nyingi za kwenye Uzi huu zinasiktisha na kuhudhunisha na wakati huo huo zinakupa picha kamili za aina ya kizazi Cha vijana wa kiume kwa nyakati hizi......na pia inatoa fursa kwa mabinti kuona uhalisia wa aina ya vijana na kufanya mamuzi sahihi.........

Na ndio mambo kama haya ndio yanayowasukuma wanawake kudai usawa kwenye jamii vile vile kufanya wanawake watamke wazi kuwa kazi ndio mume wake........
 
Mkuu, kuna gap kubwa sana ya uelewa kati yetu. Hiyo story ni one sided, with little or no facts, hatuwezi kuongea mambo mengi kama vile watu wa ustawi wa jamii. Atueleze kwanini kaachwa na kutekelezwa
Hakika ndugu ngoja tuache kama ilivyo lakini katika uhalisia kwenye jamii zetu Hilo jambo limetamalaki sana.......na ndio jambo ambalo limeamsha hisia za chuki kwenye mjadala huu huku kila mmoja akichukua upande wake.........
 
Bab si anatakiwa awajibike kwenye malezi.

Lakini sio malezi ya kupangiwa na Mwanamke tuliyekwisha kuachana naye.

Yaani achague shule ya gharama Mimi ñilipe,
Mtoto akiumwa achague Hospitali ya gharama Mimi ñilipe tuu, kisa malezi ya Baba. Never ever.

Mimi ndiye Baba, nachagua wapi mtoto wangu asome kulingana na uchumi wangu, Kama mama yake anauchumi zaidi simkatazi kumpeleka shule atakayo. Lakini sio anipe Misalaba ya kipuuzi nami nimuendekeze. Hilo halipo. Hata aende Kwa Nani.

Nina watoto wengi asifikiri kuwa nina huyo mmoja wa kwake
 

Irrelevant.
 
Unaongea maneno ya mwisho.
 
Lakini tujiulize, hadi mwamba kuamua kuachia nyumba ili bimama aishi na mtoto inamaana jamaa yupo mstari wa mbele kutimiza majukumu yake. Kuna kitu huyu bimama hajakiweka wazi, akiwa muwazi tunaweza kufumba midomo.

Bahati mbaya wanaoleta nyuzi za hivi kuna vingi wanaficha, hawawi wazi coz wana makandokando mengi.

Huyu mwamba anaonekana kutimiza wajibu wake, hadi nyumba kakuachia...uwe mjinga sasa uiuze ili dogo aende english medium school. Utakuwa mbatata ya marikiti kule mchambawima.
 
Watu tozo, mafuta Bei juu halafu mtu analeta habari za ada milioni na ushee halafu amejipangia mwenyewe na form ya kujiunga kaifuata mwenyewe hajatumwa na mtu sinamejipima huyo kuwa anaweza
Ha ha ha...
Hawa wanawake wa kisasa (feminist) Ni Changamoto Sana mkuu,

Huenda ndo aling'ang'ania ndoa ivunjike, kisingizio Kuna kijikazi kinampa kiburi mpk mtoto kapeleka shule za gharama. Jamaa kamuachia Hadi nyumba.

Kasahau
Kuna kupata na kukosa,
kijikazi kilichompa kiburi kimeota mbawa. Anarud kwa jamaa kudai ada.

Hata ningekua Mimi,
Ningekukaushia, sema najua jamaa anafanya for good Ila adabu iwepo.
Sio kwamba anamchukia mwanae
 
Mbona unakuwa mkali hivo?
 
anyway fuata taratibu utapata stahiki yakoo
Apambane na hali yake tu! amtafute Nani????! me wa siku hizi atakwambia kazi hana, huko Mahakamani ataenda atawaambia mkitaka,mnipe kazi au nifungeni kazi sina! wakili atakula hela dem weeee! kuliko karo!
 
Yani MTU umuachie Nyumba halafu akulazimishe umtumie ada ya Shule Binafsi? Akienda kulipa anamdanya Mtoto kuwa yeye ndio amelipa na baba yake amemtelekeza hamjali!! Watoto Hao wanaosomeshwa Vizuri na baba zao wakilelewa na akina mama wapumbavu wanakua hatari sana baadae kwani wanadanganywa kuwa ada ya mamilioni alikua anatoa mana Kwa vikoba na kuuza vitunbua kumbe ni uongo.

Kifupi tu kama Mtoto amemshindwa basi amkabidhi Mtoto Kwa baba yake na apangishe Nyumba yeye Yuko huru kuolewa na MTU Mwingine Maisha yasonge mbele
 
Taikon wa fasihi.
Mtoto akiwa kwa baba huwaga wanawake nao wanatumaga pesa ya malezi?
 
Taikon wa fasihi.
Mtoto akiwa kwa baba huwaga wanawake nao wanatumaga pesa ya malezi?

Uliwahi sikia kesi ustawi WA jamii au mahakamani kuwa Mwanaume kaenda kushtaki mama watoto hamhudumii Mtoto? Jibu ni hapana.

Wanawake hawatumi na wala hakuna sheria inayowabana watume.
Ingawaje wapo wanawake wanaowatumia watoto wao pindi wakikua/wakijitambua
 
Katika maandiko matakatifu Mungu ameseama anachukia kuachana,consequences za kuachana huwa ni nyingi sana hata kama mna pesa kiasi gani,nasema kila siku humu maisha ya ndoa bila ya kuwa na Mungu usitegemee muujiza,kama ikiwezekana mrudiane au tafuteni amani,lakini kama mnaendelea kuvimbishiana vifua utashuhudia maumivu mengi sana na hilo unalopitia ni moja wapo.....
 
Ilibidi wakati mnaachana mambo matatu kama mliachana mahakamani kwa kupewa talaka. 1/ talaka 2/ mgawanyo wa mali 3/ matunzo ya watoto kama wapo.
Kwa ushauri wa hitaji lako nenda ofisi ya kata kwa afisa maendeleo ya jamii kuhusu lalamiko lako. Ikishirikiana hapo kupata suluhu ndipo utaenda baraza la kata au mahakamani
 
Hela imepungua tena duuh.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…