Mzazi mwenzangu hahudumii mtoto; nataka nimpeleke mahakamani

Aliyechagua shule ndio alipe Ada.
Mbona unashindwa kuelewa mambo madogo.

Yaani kuna wanawake ukizaa nao inakuwa Kama umezaa na mwendawazimu.

Shule uchague wewe alafu mwanaume uliyezaa Naye alipe Ada. [emoji23][emoji23]
Huyo unayejibishana naye kaachwa hivo ana hasira za kuachwa
 
Nacho ona wanawake ni selfish sana kama ivyo.
 
Sasa mentality na uhalisia vimeumana haya apambane. "Cut your cloth accordingly to your size".
 
Mliachana au mlitengana?Ilikuwa ndoa ya kanisa au msikitini?Ada ya shule ni kiasi gani?Shule za bure si zipo?Anatoa matunzo ya mengine?Ana uhusiano mzuri na mtoto?Ana watoto wengine?Kabla hujaenda mahakamani jijibu hayo maswali ili ukienda ujue unaenda kudai nini haswaaa.
 
Unachotakiwa kufanya mpeleke mtoto kwenye shule za serikali na hazina shida yoyote mu dia mbona tulisoma huko menhine ni fashion za siku hizi tu kuonekana kwa watu.
 
Loh pole sana

Usikwazike na majibu ya wanazengo wa humu

Kama upo Dar nenda pale Chang'ombe Mahakama kituo Junuishi ya Ndoa na mirathi. Kuna ofisi za WILDAF wanatoa ushauri mzuri kisheria kuhusu masuala aina hii.

Sheria inamtaka baba kugharimia matunzo ya mtoto hata kama mmeachana kisheria. Tatizo ninaloliona ni wamama wengi wamekuwa na moyo wa KUMUACHIA MUNGJ pale wanapokosa matunzo ya watoto.
 
Sidhani kama kuna sehemu huyu mtoa mada amesema au kuandika kuwa baba wa mtoto amemuachia nyumba....??
 
Hata mm nilipatwa na hili Jambo

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Sidhani kama kuna sehemu huyu mtoa mada amesema au kuandika kuwa baba wa mtoto amemuachia nyumba....??
Na mimi nashangaa Wana uhakika gani huyo Mama kaachiwa nyumba na Mzazi mwenzie?What if Nyumba ni ya Mwanamke mwenyewe aidha alijenga ama Karithi kwa wazazi wake?

Pia Mtoa Mada kasema anataka Ampeleke Mahakamani Mzazi mwenzie ili Japo asaidiwe kulipa Ada tu, means Huyo Baba hatoi matunzo yoyote ya Mtoto ila huyu Mtoa Mada kaomba asaidiwe Ada tu hayo mengine anayamudu mwenyewe.
 
Hiyo beta start ndio alivyoshauriana na Mzazi mwenzako au anataka afosi king baada ya mambo kukwama?? Kama anafosi king kupitia mahakamani anaweza akakwama, kama kulikuwa na kauli za mtoto nitamlea mwenyewe hawezi nishinda Seb linaanzaga hapa
Wanawake ni mabingwa wa kauli za kishujaa ila mziki ukiwa mnene wanarudishaga majeshi nyuma na kuanza kulia lia wapewe child support
 
Wanawake wanamatatizo Sana Mimi wangu alinipokonya mtoto na kashfa kibao kwamba Mimi maskini siwezi mtunza mwanae na nikimuhitaji masharti kibao lakini Leo hii ananitafuta nitoe maela kwa mtoto🤣 na Mimi namkazia tuone yeye si alisema yupo vizuri atamtunza mwenyewe na anauwezo minipozangu tu namtazama kama nacheki derby ya kariakooo
 
Sasa mtoto kumlisha utalinganisha na ada? Ada kwa mwaka kwa shule za wapenda show off inaweza fika hata 4M kwa mwaka 😅 yeye kajichagulia kipengele cha kumlisha ambacho mtoto anakula kile kile anachokula yeye which is inexpensive compared na malundo ya school fees, unapigiwa simu inatakiwa laki 8 ya ada fasta.
 
Sasa hapo furushi si mwanamke aliefosi kuondoka kwa kiburi huku akijifanya superwoman. Mtoto arudi kwa baba yake
 
MKIISHA TALIKIANA AU TENGANA

kila mmoja ana kwenda kuanza maisha yake na vipaumbele vyake. Hapana wewe unataka mtoto asome Private schools za Gharama, ili kufurahisha macho ya wengi, na mwanaume kwa sbb ya kuanza maisha mengine. Uwezo wake ni kusomesha shule za serikali(Kuna mgogoro hapo).

Wakati mwingine mwanamke anamtumia mtoto kama fimbo ya kuchapa mwanaume (amin hapa unajiumiza wewe au mtoto) baba ni majeruhi wa tatu baad aya ninyi. Kama baba anahitaji mtoto na wewe hutaki kumpa basi anakata huduma. (Naona kuna tatizo zaidi upande wako)

Mara nyingi wanawake wana nguvu sana mdomoni na ni dhaifu sana moyoni hasa kwenye mambo haya ya migogoro ya mahusiano. hapa hata ukitafuta mwana sheria mzuri hakuna cha maana utakacho pata sana ni kupoteza muda na fedha. na PENGINE HATA HAKI YA KUISHI NA MTOTO UKAJA KUKOSA
 
Nyakati hizi tuna vijana wa kiume wanaokuwa miili tu lakini akili zinabakia pale pale.......ukifuatilia hii michango utalifahamu hilo.....na ndio chimbuko la mabinti wanaoitwa single moms.......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…