Mzazi mwenzangu hataki mtoto apate Elimu nzuri, nadhani hajui elimu ni kwa faida ya mtoto sio mimi wala yeye

Iyo code mbona rahisi labda tu unajizima Data...Mama mtoto anataka kama ni mtoto kuja Dar aje na yeye mkae wote.
 
Wanawake wengi wanawatumia watoto kama kitega uchumi hivyo ukimchukua atazikosa hata hizo hela ndogo ndogo na hicho ndio kitu wanawake wengi wanawaza.
 
Wanawake wengi wanawatumia watoto kama kitega uchumi hivyo ukimchukua atazikosa hata hizo hela ndogo ndogo na hicho ndio kitu wanawake wengi wanawaza.
Kama ni hivyo basi anajali maslahi yake na si mtoto, ndyomaana hajali kuhusu umuhimu wa Elimu nzuri kwa mtoto
 
Shule nzuri na elimu nzuri ni vitu viwili tafauti, heheeee
 
Kwani huko mkoani hakuna shule nzuri ya private mtafutie hiyo hiyo kwa sasa huku ukiwaza baadae


Maana hata mikoani zipo shule nzuri tu na zitamjenga, mabishano ya sasa hayatamsaidia

Ila baadae sasa ndio unaweza kumhamishia kwingine
 
Umemzalisha mtoto wa watu then unategemea mama yako ndiyo akulelee huyo mtoto?
Nawe bado ni mtoto acha mama yake aendelee kumlea na kumsomesha huko kijijini.
 
Kuna baadhi ya wanawake ni kama wana LAANA wao wanahisi wanakomoa, lakini kiuhalisia hawamkomoi yeyote.

Mie mzazi mwenzangu alikuja kumchukua mtoto mikononi mwangu akiwa anamalizia darasa la 3, mie mtoto nilianza kukaa nae akiwa na miaka mi4 hivi, nimeishi nae, akaanza la kwanza, la pili, la 3, anaingia la 4 akaja kuleta utata sijui namhitaji mtoto kimeenda kimerudi,sikuona haja ya kumgombea mtoto ukizingatia kisheria mtoto bado ana umri wa kuishi na mama yake, wakati yupo kwangu likizo zoote mwezi wa 6 na wa 12 mtoto alikuwa nampeleka upande wa mama yake kusalimia.
Yeye toka amemchukua mtoto hataki kabisa kunipa mtoto kwenye likizo yoyote, mwaka wa pili huu na mwakani ni wa 3, hakuna likizo kanipa mtoto kila likizo ni visingizio.
Yaani namuona ni kama SHETANI vile, sasa sijui ndio ananikomoa kisa sikumuoa yeyr ama shida nini.. Nahisi kabisa anafanya haya kwa makusudi, na kuna sumu anamjaza mtoto, last time nilifunga safari toka dar mpaka shinyanga kumuona tu mtoto, lakini ule upokeaji, lile vibe la huyu ni baba mwaka wa pili huu sijamuona, halikuwepo, yaani ilikuwa kawaida mnoo, utafikiri tunaishi pamoja na tumetoka kuonana mchana wake

Ila kuna baadhi ya viumbe ni MASHETANI kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…