Mzazi mwenzangu hataki mtoto apate Elimu nzuri, nadhani hajui elimu ni kwa faida ya mtoto sio mimi wala yeye

Mzazi mwenzangu hataki mtoto apate Elimu nzuri, nadhani hajui elimu ni kwa faida ya mtoto sio mimi wala yeye

Nilipanga kumuona hata wazazi wake niliwaambia hilo, lakini alifanya mambo ya ajabu ambayo hata ingekuwa ni wewe usingekubali kuoa mwanamke wa aina hiyo.
Sasa kwenye malezi ya mtoto hasa akiwa mdogo inabidi uyavumilie yapite tu.
 
Akitafta wilayani itakuepp. Jaribu kuwa muelewa na kujishusha wakati mwngne kaa na msma watot muyajenge Beef sio nzuri life is short
Mimi sina beef naye, tunaongea vizuri tu, hata hili swala alipokataa wala hatuja zozana, ila nilimwambia tu huko atamsomesha yeye.
 
Mpongeze sana, asome huko huko hautogaramika sana; kumbuka bado unamiaka 30 ya kumjengea maisha huyo mtoto.

Hakikisha umemuwekea ata kiwanda kidogo cha kupukuchua mahindi. Maisha si elimu tu, na mali pia ni muhimu kumuachia.

Waliosoma sasa hivi hawana ajira.​
 
Sawa. Huyo mtoto utambomoa kuliko unavyofikiria.
Nitambomoa mimi au mama yake? Akimpeleka kwa Baba mwingine ndyo atajenga au kubomoa?

Mimi nataka nimuokoe mtoto, aishi vizuri na kwa amani, asome vizuri na kwa usahihi.
 
Habarini ndugu

Mimi na mzazi mwenzangu bado hatuna ndoa, ila tumebahatika kupata mtoto mmoja, kwa sasa wamerudi mkoani baada ya kuja na kukaa nyumbani kwetu kwa lengo la kumleta mtoto familia yangu imtambue.

Baada ya mtoto kufikisha miaka mitatu na nusu, nikamwambia mama yake itabidi mtoto aanze shule, na natamani mwanangu arudi Dar asome shule nzuri na ya kisasa.

Mzazi mwenzangu anadai hawezi kuruhusu hilo, ni afadhali mtoto abaki kijijini asome shule za kawaida (serikali). Nikamwambia utamsomesha wewe huko, mimi nilitaka aje Dar asome shule nzuri na tofauti na hapo sitahusika na maswala ya shule endapo atasoma tofauti na nilivyotaka.

Nadhani labda bado anachuki au kinyongo dhidi ya familia yangu, lakini hajui Elimu bora ina faida kwa mtoto na maisha yake ya baadaye, sio mimi wala yeye.

Je ni sahihi nikikataa kutoa huduma za shule endapo atasoma kijijini? Kwani lengo langu lilikuwa aje asome Dar, akae na Bibi yake (Mama yangu) na yupo tayari kwa hilo.

pia soma: Mzazi wangu hajaridhika na mchumba wangu, hajasema lakini nimeona ishara
Kwani SAUTI YAKO VOLUME YAKE NI MWISHO HAPO? Please usiwe ZUZU kiasi hicho kwa mwanamke ambaye hata ndoa yenyewe bado. Au siyo damu yako? Kama ni damu yako kwanini unakuwa rahisi rahisi hivyo?
 
Mpongeze sana, asome huko huko hautogaramika sana; kumbuka bado unamiaka 30 ya kumjengea maisha huyo mtoto.

Hakikisha umemuwekea ata kiwanda kidogo cha kupukuchua mahindi. Maisha si elimu tu, na mali pia ni muhimu kumuachia.

Waliosoma sasa hivi hawana ajira.​
Kugharamika sio tatizo, ila Urithi wa Elimu ni bora kuliko urithi wa nyumba na magari.
 
Kwani SAUTI YAKO VOLUME YAKE NI MWISHO HAPO? Please usiwe ZUZU kiasi hicho kwa mwanamke ambaye hata ndoa yenyewe bado. Au siyo damu yako? Kama ni damu yako kwanini unakuwa rahisi rahisi hivyo?
Hizo ni techniques tu, hiyo ni damu yangu na lazima niwe karibu nayo kwa gharama yoyote.
 
Kwanini mmetengana nazani tatizo lipo hapa nyinyi sio kitu kimoja mmetengana alafu mme zaa lazima kuwe na vuta nikuvute hapo na sio kwamba mwenzako hqtaki mtoto apate elimu bora
Umeongea ukweli anaozungukazunguka,mama hataki mwanae alelewe nje ya yeye....na huyu hataki kutuma pesa ya matumizi....maana hata aliko mama lazima Kuna nursery school nzuri...hataki kutuma matumizi.
 
Umeongea ukweli anaozungukazunguka,mama hataki mwanae alelewe nje ya yeye....na huyu hataki kutuma pesa ya matumizi....maana hata aliko mama lazima Kuna nursery school nzuri...hataki kutuma matumizi.
Matumizi natuma bila hata kuulizwa, pia ni kweli nataka kukaa karibu na mwanangu.

Kuhusu nursery, niamini mimi nakuambia, huko HAKUNA hata moja.
 
Kugharamika sio tatizo, ila Urithi wa Elimu ni bora kuliko urithi wa nyumba na magari.
Tuma pesa atasoma kwa mama yake....la sivyo maamuzi utakayoamua ni sahihi pia,usitume chochote... watoto wanakua mkuu🤣🤣🤣🤣
 
Matumizi natuma bila hata kuulizwa, pia ni kweli nataka kukaa karibu na mwanangu.

Kuhusu nursery, niamini mimi nakuambia, huko HAKUNA hata moja.
Mhamishe mama na mtoto....umri wa mtoto ni wa kukaa na mama mzazi
 
Back
Top Bottom