Binafsi, si kwa muislamu tu, hata kama ni mkristu mwenzie, kwenda kuishi na mtu mnayetofautiana kiimani ya dini, ni hatari sana. Hili haliwezi onekana huku mwanzoni. Kile kinachofanya kila mtu awe na imani yake, siku kikiibuka ndo watajua joto ya jiwe. Embu fikiria, mkatoliki anayefunga ndoa na hawa wa kipentekoste, huyu mkatoliki atamueleza nini mpentekoste juu ya Bikira maria na akamuelewa? Kwenye IDI tu hawa wa suni na wengine mnaonaga kila mtu antangaza idi yake..!! Fikiria msuni aliyeolewa na muislamu asiye msuni, siku ya idi ya mmoja, huyu anayeendelea kufunga atafungua?