Mzazi wangu amekogoma kupokea posa ya mwanaume wa kiislamu

Mzazi wangu amekogoma kupokea posa ya mwanaume wa kiislamu

Baba yangu mdogo Jana aliniita na kunieleza jinsi anavyoumia kwa kile mdogo wetu amekifanya kwa kutuleteaa mwanaume wa kislamu amuoe wakati sisi ni wakristo.

Mzee anasema hivi wanaume wameisha kiasi kwamba hadi aolewe na Waisilamu? kweli mdogo wetu ni mzuri sana, amesoma hadi chuo kikuu Sasa tunashamgaa posa inaletwa na watu wa imani nyingine wakati sisi tumemlea kwa taratibu zote za dini yetu ya kikristo kupitia KKKT.

Tumemshauri mdogo wetu atulie kwanza kwanza bado mdogo na pia mwanaume hawezi mkosa amtakae yeye lakini amegoma kutusikilizaa kabisa amesma ataolewa na ABDULI TU ova.

Wakuu nimshauri vipi mzee kwa ananitegemea mimi kumpa ushauri ametokea kuniamini.

Kuna msatari wa bibilia tumemsomea wa " usifunge nira na watu wasio amini " amegoma kutusikilizaa kbsa Ni ABDULI TU ANAMTAKA.
wajibu wenu nyie ni kumshauri, akigoma mwacheni aende kimyakimya
 
Ikiwa dini unayojinasibisha nayo haiongozi mfumo wako wa maisha basi jitafakari vizuri! either hiyo dini yako ni impractical au wewe si muumini wa kweli wa hiyo dini.

Huwezi kuamini mtuhumiwa hana hatia halafu bado ukamuadhibu!
Wewe ni mjinga pro max unaacha kufuata mila na desturi zenu unaenda saudi Arabia Israel kuabudu kwenye makaburi ya watu usiokua na unasaba nao
 
huyo binti ni mjinga sana, na atajuta maisha yake yooote. hakuna mwanamke aliwahi kubadili dini kuwa muislam asijutie baadaye, na huwa wanaishia kuwa makopo kichwani utafikiri akifika kule huwa anapakua ubongo wote halafu wanaweka hewa. nina ndugu zangu kadhaa walishawahi kubadili dini, wakazaa watoto na yakawashinda wakarudi na hawajawahi kutengamaa, wawili walikufa masingle mother, mmoja ndio anaishi kama ana laana tu. naona sijui walimsomea kisomo au walimpulizia harufu mbaya sijui.
Wewe ndio mtumwa wa fikra kabisa,yaani hapo unajiona mjaaanja kwa kufuata tamaduni za wagenj kutoka ulaya na uarabuni
 
Wewe ni mjinga pro max unaacha kufuata mila na desturi zenu unaenda saudi Arabia Israel kuabudu kwenye makaburi ya watu usiokua na unasaba nao
"Mjinga" ni neno tu, unaweza kuliweka sehemu sahihi ama vinginenyo! Ila Ujinga katika sura yake yenyewe kabisa huonekana pale wa mjinga kweli anapofungua mdomo wake!

Mi naweza kukuita wewe mwerevu kumbe kiuhalisia ndo MJINGA mwenyewe tunaemuongelea
 
Mnaolewa nyie au vipi?
Acheni watu kuwapangia aisee!
We hujii huyo dogo lenu anapata nini kwa hiyo jamaa!

Kwani wangapi wameachana kwa kuoana dini moja
 
Baba yangu mdogo Jana aliniita na kunieleza jinsi anavyoumia kwa kile mdogo wetu amekifanya kwa kutuleteaa mwanaume wa kislamu amuoe wakati sisi ni wakristo.

Mzee anasema hivi wanaume wameisha kiasi kwamba hadi aolewe na Waisilamu? kweli mdogo wetu ni mzuri sana, amesoma hadi chuo kikuu Sasa tunashamgaa posa inaletwa na watu wa imani nyingine wakati sisi tumemlea kwa taratibu zote za dini yetu ya kikristo kupitia KKKT.

Tumemshauri mdogo wetu atulie kwanza kwanza bado mdogo na pia mwanaume hawezi mkosa amtakae yeye lakini amegoma kutusikilizaa kabisa amesma ataolewa na ABDULI TU ova.

Wakuu nimshauri vipi mzee kwa ananitegemea mimi kumpa ushauri ametokea kuniamini.

Kuna msatari wa bibilia tumemsomea wa " usifunge nira na watu wasio amini " amegoma kutusikilizaa kbsa Ni ABDULI TU ANAMTAKA.
Mnakosea sana, inatakiwa kumuuliza mara tatu, kama bado msimamo wake ni huo, mruhusuni aoelewe.
 
Kwa msingi na ustawi mzuri kiimani wa matokeo ya ndoa(watoto) ni bora watu wa imani flani waoane kuliko kuchanganya mara kobazi mara Rosali,,,, !!!
 
TamekqA na jamii nzima imejuwa kuwa tumekataaa posa hyo hatuwataki
Mpeni sharti yeye ndio abadiri dini kama anampenda binti wote wawe Christian au binti yenu abadiri dini awe muslim.

Kwa hizi primitive society zetu simshauri mtu kuoa au kuolewa na mtu wa imani tofauti, kama mnapenda kweli basi mmoja ni lazima afuate imani ya mwenzake isiwasumbuwe hata kwenye malezi ya watoto.
 
Kabla ya ujio wa wageni babu zetu walikua hawasomi shule,wanavaa majani ya miti,wanapikia vyungu nk
Labda ni Babu zako lakini Babu zangu wa Kitutsi walikuwa na Himaya na wanashona nguo kupikia Vyungu sio tatizo tatizo ni hizo sufuria za Aluminium ambazo sio nzuri kwa Afya.
 
2 Wakorintho 6:14
"Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza?"

Waefeso 6:1
"Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki"

Nimeona wengi wakimwacha Yesu kwa sababu ya kutaka ndoa😭😭😭.
Hawajui wanachopoteza.
Mshaurini,akikataa mwacheni.
 
Back
Top Bottom