Mzazi wangu hajaridhika na mchumba wangu, hajasema lakini nimeona ishara

Mzazi wangu hajaridhika na mchumba wangu, hajasema lakini nimeona ishara

Kwa hiyo ukampeleka mdada wa watu miezi akae na mama Yako agundue Nini? Unaoa wewe au mama Yako, akili Yako haitoshi mpaka utumie ya mama Yako, hebu tutolee utoto wa mama hapa be a man, ni Nini unataka eti nimegundua mama kaona Kuna kitu hakipo sawa muone kwanza hovyoooo
Vitoto vya afu mbili hao kasamehe bure tu
 
Kutafuta mke sio jukumu lake, Mimi ndy natafuta then yeye ananipa ushauri
Kuomba ushauri ni vizuri.
Kuna point ya kuomba ushauri ambayo imeshaivuka. Nadhani ndo maana hata bimkubwa anakosa la kukuambia. Kabla hujamtia mimba ndo ilikuwa muda sahihi wa kuomba ushauri.
1. Kama inamkubali mkeo, una wajibu wa kumshauri mama ukijenga hoja Kwa nini wampenda huku ukidefend hoja zake.
.2. Ni ngumu mama na mkwewe wakaendelea kupendana wakikaa pamoja zaidi ya mwezi mmoja.
 
Maoni ya wazazi ni muhimu katika hilo. Ila tambua ya kwamba wewe ndie unae kwenda kuishi nae na sio mzazi wako. Jiridhishe na moyo wako kwamba kweli unampenda na utaenda kujenga naye familia, hiyo inatosha kabisa.
Nilisha jiridhisha nae na wote tuna mpango wa kuishi pamoja hapo baadaye, lakini kwa sasa nahitaji kusikiliza maoni ya mzazi wangu, naamini ameona kitu baada ya kuishi nae
 
Kwa sababu unamuolea mamako, endelea kutafuta mpaka upate atakayemuelewa.
Mkuu hujaelewa mada yangu vizuri, sijasema natafuta mtu wa kuoa, ila nimesema nahisi Mama yangu kuna kitu amekiona na nahitaji anieleze ili na mimi nijue
 
Huyo binti kwanini ukampa mimba wakati unafahamu kuwa haupo tiyari kumuoa? Na unavyotaka kumuacha unatarajia Nani atamuoa?
Kujiuliza kwanini nilimpa mimba ni kitwanga maji kwenye kinu, tayari imeshatokea na sipaswi kuangalia nyuma
 
Unahitaji msaada wa kisaikolojia tunza comment yangu ipo siku utajutia kwa kuharibu familia yako ili kufurahisha familia ya Mama yako
Huenda kweli nahitaji Msaada, basi niambie nini nifanye niwe sawa kisaikolojia?
 
Kuomba ushauri ni vizuri.
Kuna point ya kuomba ushauri ambayo imeshaivuka. Nadhani ndo maana hata bimkubwa anakosa la kukuambia. Kabla hujamtia mimba ndo ilikuwa muda sahihi wa kuomba ushauri.
1. Kama inamkubali mkeo, una wajibu wa kumshauri mama ukijenga hoja Kwa nini wampenda huku ukidefend hoja zake.
.2. Ni ngumu mama na mkwewe wakaendelea kupendana wakikaa pamoja zaidi ya mwezi mmoja.
Saivi sio kama namuomba ushauri Mama, ila nahitaji aniambie kwanini hana imani nae, anieleze sababu
 
Mkuu wewe ni wa mama NDOA ya nini ukizingatia ndoa zenyewe ni utapeli tu? Endelea kula maisha acha kuwaza masuala ya ndoa
 
Hio kwa upande wako
Qur'an 39:41. Hakika Sisi tumekuteremshia Kitabu kwa ajili ya watu wote kwa Haki. Basi mwenye kuongoka ni kwa nafsi yake, na mwenye kupotoka bila ya shaka amepotoka kwa khasara yake. Na wewe si mlinzi juu yao. 41
 
Hapo umechagua mama yako kuwa ndio mwongozo kwenye kukuchagulia mtu wa kuishi nae mkuu.
Mkuu hujaelewa, sio anichagulie ila lnahisi kuna kitu amekiona na nataka aniambie ni kitu gani, sio kunichagulia
 
Back
Top Bottom