Mzazi wangu hajaridhika na mchumba wangu, hajasema lakini nimeona ishara

Wanawake jamani tusizae kwa ajili ya kumfurahisha mwanaume na pia kabla ya ndoa ingawa pia unaweza kuzaa ukiwa ndoani na bado ndoa ikavunjika, Siku hizi wanaume hawaoni shida kuacha mtoto akalelewa bila wazazi wawili, kama huyu hajaambiwa chochote tayari ameshaconclude kutomuoa dada wa watu.

Kaka hayo maisha ni yako wewe na maamuzi yawe yako wewe ndio utaishi na huyo mwanamke na sio mama yako, ina maana siku zote ulizoishi nae hadi mmezaa hujamjua bado??, Mamazboy mwingine huyo anenda kutengana na familia yake kwa ajili ya kumfurahisha aliyelea familia yake hadi uzeeni.
 
Habarini ndugu

Baada ya kupata mtoto, ilibidi mzazi mwenzangu aje nyumbani kwetu kumleta mtoto Bibi yake amuone kwani alikuwa na shauku ya kumuona mjukuu wake.

Walikaa kwa kipindi cha miezi kadhaa, na walikaa kwa furaha na amani. Mama yangu alifurahi kwani mwanzo aliona na kusifia tabia nzuri na kujituma kwa binti yule.

Kadri siku zilivyokuwa zinasonga, nikahisi kuna jambo halipo sawa, kila nikiongea na Mama kuhusu mipango ya baadae alikuwa haonyeshi dalili za kubashiri ndoa yangu na binti yule. Nikajua tu hajaridhika nae.

Lakini naamini Mzazi wangu ananijua vizuri na anajua ni kipi kitanifaa na kuendana na mimi, nahisi kuna vitu amegundua kwa binti yule kwa muda aliokaa nae.

Mimi sina tatizo na mawazo na ushauri wa Mzazi wangu, lakini najiuliza je ni sahihi kuendelea kumuaminisha binti huyu kwamba nitamuoa ilihali najua Mzazi wangu hajaridhika nae?

Najiuliza nimwambie mapema kwamba haitowezekana kufunga ndoa hapo badae? Naogopa kumpa maumivu na kumfanya akose amani.......

Ni uamuzi gani wa busara napaswa kufanya wadau? Naombeni ushauri wenu bila kebehi na masihara..

Asanteni.....
Nadhan wewe ndo utaishi na huyo Binti na sio mama, kama hajaridhika Badi muoe yeye.
 
Wanawake jamani tusizae kwa ajili ya kumfurahisha mwanaume na pia kabla ya ndoa ingawa pia unaweza kuzaa ukiwa ndoani na bado ndoa ikavunjika, Siku hizi wanaume hawaoni shida kuacha mtoto akalelewa bila wazazi wawili, kama huyu hajaambiwa chochote tayari ameshaconclude kutomuoa dada wa watu.

Kaka hayo maisha ni yako wewe na maamuzi yawe yako wewe ndio utaishi na huyo mwanamke na sio mama yako, ina maana siku zote ulizoishi nae hadi mmezaa hujamjua bado??, Mamazboy mwingine huyo anenda kutengana na familia yake kwa ajili ya kumfurahisha aliyelea familia yake hadi uzeeni.
Madame, nadhani hujanielewa point yangu, sijasema nataka kumuacha wala kumtelekeza, nimesema nimeona dalili kwamba kuna kitu hakipo sawa kwa Mama.

Nataka nimuulize anipe sababu, akiniambia ndyo nitapima uzito wa hilo jambo na kufanya maamuzi
 
Madame, nadhani hujanielewa point yangu, sijasema nataka kumuacha wala kumtelekeza, nimesema nimeona dalili kwamba kuna kitu hakipo sawa kwa Mama.

Nataka nimuulize anipe sababu, akiniambia ndyo nitapima uzito wa hilo jambo na kufanya maamuzi
Najiuliza nimwambie mapema kwamba haitowezekana kufunga ndoa hapo badae? Naogopa kumpa maumivu na kumfanya akose amani.......

Hayo hapo juu ni maneno yako wewe mwenyewe kaka yangu, mama/baba yako abaki kuwa mshauri wako na sio mwamuzi wa maisha yako ambapo hata ushauri unaangalia unaofaa chukua usiofaa achana nao. Hata wazazi wetu pia wanakosea so usiseme mama yako ana hekima tuu, kwanza kwanini umuache mkeo akae muda mrefu na mama yako wakati hujamuoa bado??

Natamani sana kukupa mfano hai wa mtu aliyekuwa na situation kama yako sasa hivi anajutia ila wewe ni mtu mzima jifunze mwenyewe, nitakachokushauri ni kwamba ukishazaa na mwanamke hakikisha kwa namna yoyote mnalea mtoto wenu pamoja madhara ya baadae ni makubwa mno na utakaeteseka ni wewe while mama yako atakuwa pembeni anakuangalia tuu na kukufariji kusiko na maana kwako. Muoe mama mtoto wako kabla haijawa too late kama wewe umeridhika na tabia zake na unaona anakufaa.
 
Nimekuelewa sisiter pia nashukuru kwa ushauri huo mzuri, ila lengo langu halikuwa kumuacha au kumtenga, na najiuliza ntaanzaje kumuambia hivyo kwani sitaki nimkwaze..

Ila Mama akinipa sababu na mimi nitaangalia kama ina mashiko au la, kama haina uzito mkubwa mimi nitaendelea kuwa na mzazi mwenzangu japo ndoa sio jambo la saivi, mpaka nimalize masomo
 
Habarini ndugu

Baada ya kupata mtoto, ilibidi mzazi mwenzangu aje nyumbani kwetu kumleta mtoto Bibi yake amuone kwani alikuwa na shauku ya kumuona mjukuu wake.

Walikaa kwa kipindi cha miezi kadhaa, na walikaa kwa furaha na amani. Mama yangu alifurahi kwani mwanzo aliona na kusifia tabia nzuri na kujituma kwa binti yule.

Kadri siku zilivyokuwa zinasonga, nikahisi kuna jambo halipo sawa, kila nikiongea na Mama kuhusu mipango ya baadae alikuwa haonyeshi dalili za kubashiri ndoa yangu na binti yule. Nikajua tu hajaridhika nae.

Lakini naamini Mzazi wangu ananijua vizuri na anajua ni kipi kitanifaa na kuendana na mimi, nahisi kuna vitu amegundua kwa binti yule kwa muda aliokaa nae.

Mimi sina tatizo na mawazo na ushauri wa Mzazi wangu, lakini najiuliza je ni sahihi kuendelea kumuaminisha binti huyu kwamba nitamuoa ilihali najua Mzazi wangu hajaridhika nae?

Najiuliza nimwambie mapema kwamba haitowezekana kufunga ndoa hapo badae? Naogopa kumpa maumivu na kumfanya akose amani.......

Ni uamuzi gani wa busara napaswa kufanya wadau? Naombeni ushauri wenu bila kebehi na masihara..

Asanteni.....

Bado hujakomaa kuanzisha Familia.
Siku àmbayo utakuwa na maamuzi yako binafsi kuhusu Maisha yako ndîo Siku àmbayo Ipo tayari kuitwa Baba na Mume.
 
Sio kwamba yeye ndyo afanye maamuzi, ila nataka aniambie ni sababu gani ambazo zinafanya asimkubali huyu binti

Yeye ndîo amamuoa?
Yeye ndiye ataishi naye?
Yeye ndiye aliyemchagua au wewe?
Au yeye kwako mdhibitu na mkaguzi wa mahusiano yako?
 
Ni kweli sio kila kitu lazima mzazi ashauri, lakini jambo kama hili ni muhimu kumpa nafasi ya kushauri, pia Mama yangu ni mtu wa hekima sana, namuamini katika maamuzi yake

Na kama anahekima hatakushauru chochote zaidi ya kukuambia fuata Moyo wako.

Mzazi jukumu lake lilikuwa kukulea na kukufundisha jinsi ya kufanya maamuzi. Ukishafikia umri ulionao anakuwa ameshamaliza wajibu wake.

Unàtaka ushauri wa Mama baàda ya kumzalisha Binti wa Watu?
 
Naelewa majukumu yote ni yangu katika kufanya maamuzi, lakini still bado nahitaji kujifunza na kupata ushauri kuhusu mambo haya kwani mimi bado ni kijana ambaye sina experience na mambo ya Ndoa

Ndoa haina experience.
Ndoa inahitaji mambo yafuatayo;
1. Upendo
2. Utayari
3. Ukomavu
4. Sacrifice
5. Maamuzi Sahihi Kwa Wakati Sahihi
6. Uhimilivu wa Mambo íwe changamoto za Maisha au mafanikio ya Maisha
 
Mkuu hujaelewa, sio anichagulie ila lnahisi kuna kitu amekiona na nataka aniambie ni kitu gani, sio kunichagulia
Mama yako yuko Jf au unadhani kwa kutumia mtandao huu utapata majibu ya maswali yako.
 
Na kama anahekima hatakushauru chochote zaidi ya kukuambia fuata Moyo wako.

Mzazi jukumu lake lilikuwa kukulea na kukufundisha jinsi ya kufanya maamuzi. Ukishafikia umri ulionao anakuwa ameshamaliza wajibu wake.

Unàtaka ushauri wa Mama baàda ya kumzalisha Binti wa Watu?
Haitaji kumuoa huyo binti ana mtafutia sababu amuache.
 
Back
Top Bottom