Mzazi wangu hajaridhika na mchumba wangu, hajasema lakini nimeona ishara

Wewe bado ni mvulana humfai huyo binti
 
Dont make mistake ya kumtupa mwanamke huyo kisa mama hajampenda. Unaenda kuishi nae wewe si wazazi wako. Wouka kufanyiwa maamuzi na wazazi
Asipuuze hisia za Wazazi wake, hakuna mzazi hata mmoja hapa duniani ambaye anapenda kumuona mtoto wake wa kumzaa akiishi maisha ya dhiki, mateso na tabu kubwa. Hayupo mzazi wa namna hiyo, kila mzazi anajisikia furaha Sana pale anapomuona mtoto wake akiishi maisha mazuri na yenye furaha siku zote.

Kitu Cha kufanya ni kwamba Bwana huyu anapaswa akae na mzazi wake kwa utulivu mkubwa na Kisha amchunguze au amdodose kwa undani zaidi huyo mzazi wake juu ya kwa nini anaonekana kutokuridhika na kutokubariki suala la ndoa la huyo kijana wake pamoja na huyo mchumba wake. Azijue sababu zake kwanza ndipo afanye Uamuzi wa aidha afunge ndoa na huyo mwanamke au la.
Asikurupuke kufunga ndoa Wala asipuuze hisia za mama yake.

Atafakari kwa kina kabla ya kufanya Uamuzi wa mwisho.
 
Kweli sijafika muda wa kuoa, hata yeye analijua hilo.

Sitafuti matatzo, ila nimeona kuna tatizo na lazima nijue ni tatizo gani

Umeona tatizo Kwa huyo Mchumba au Kwa Mamaako?

Kama hujafikia Muda wa Kuoa Bora umwambie huyo mchumbaako kuliko umtafutie ubaya Kutoka Kwa maneno na maoni ya Watu Wengine ikiwemo Mamaako
 
Mkuu umesema vizuri kabisa, lazima nikae na mzazi wangu nimdodose nijue ameona nini, siwezi kupuuzia mawazo yake lakini nitapima kama yana uhalisia au La. Hapo ndipo nitafanya maamuzi.
 
Kama hujafikia Muda wa Kuoa Bora umwambie huyo mchumbaako kuliko umtafutie ubaya Kutoka Kwa maneno na maoni ya Watu Wengine ikiwemo Mamaako
Mkuu naomba unielewe, huyu binti anajua kabisa muda wa ndoa bado, hata kwao wanajua.

Sio kama natafuta tatizo au sababu ya kumuacha, mimi natamani niendelee kuwa naye.. Ila nimeona tofauti kwa Mama yangu, na lazima nijue ameona kitu gani.
 
Wewe ni mvulana kwakuwa huwezi fanya maamuzi yako binafsi mpaka mama yako akufanyie
Wapi nimesema nataka Mama anifanyie maamuzi?

Nimesema nataka aniambie ni sababu gani naona hana imani tena na huyo binti, then mimi ndio nifanye maamuzi
 
Wapi nimesema nataka Mama anifanyie maamuzi?

Nimesema nataka aniambie ni sababu gani naona hana imani tena na huyo binti, then mimi ndio nifanye maamuzi
Si umepiga u turn kutaka kumwoa huyo binti baada ya kuona mama yako hajaridhika?
 
Mkuu naomba unielewe, huyu binti anajua kabisa muda wa ndoa bado, hata kwao wanajua.

Sio kama natafuta tatizo au sababu ya kumuacha, mimi natamani niendelee kuwa naye.. Ila nimeona tofauti kwa Mama yangu, na lazima nijue ameona kitu gani.

Kama anashida Mama yako atakuambia
Lakini wewe kutafuta shida mbayo hujaiona Kwa Mtu unayempenda, tenà shida hiyo unaitafuta kwa Mtu Mwingine hai-sound vizuri Kwa Mwanaume aliyekomaa

Huo unaitwa Umbeya au kupenda kusikia maneno ya kuambiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…