Habarini ndugu
Baada ya kupata mtoto, ilibidi mzazi mwenzangu aje nyumbani kwetu kumleta mtoto Bibi yake amuone kwani alikuwa na shauku ya kumuona mjukuu wake.
Walikaa kwa kipindi cha miezi kadhaa, na walikaa kwa furaha na amani. Mama yangu alifurahi kwani mwanzo aliona na kusifia tabia nzuri na kujituma kwa binti yule.
Kadri siku zilivyokuwa zinasonga, nikahisi kuna jambo halipo sawa, kila nikiongea na Mama kuhusu mipango ya baadae alikuwa haonyeshi dalili za kubashiri ndoa yangu na binti yule. Nikajua tu hajaridhika nae.
Lakini naamini Mzazi wangu ananijua vizuri na anajua ni kipi kitanifaa na kuendana na mimi, nahisi kuna vitu amegundua kwa binti yule kwa muda aliokaa nae.
Mimi sina tatizo na mawazo na ushauri wa Mzazi wangu, lakini najiuliza je ni sahihi kuendelea kumuaminisha binti huyu kwamba nitamuoa ilihali najua Mzazi wangu hajaridhika nae?
Najiuliza nimwambie mapema kwamba haitowezekana kufunga ndoa hapo badae? Naogopa kumpa maumivu na kumfanya akose amani.......
Ni uamuzi gani wa busara napaswa kufanya wadau? Naombeni ushauri wenu bila kebehi na masihara..
Asanteni.....