Mzazi wangu hajaridhika na mchumba wangu, hajasema lakini nimeona ishara

Mzazi wangu hajaridhika na mchumba wangu, hajasema lakini nimeona ishara

Kwanza hujaeleza baba yako yupo wapi, kama amekufa baba mdogo/mkubwa wanasemaje? Baraka hazitoki kwa mzazi mmoja tu wa kike peke yake. Baraka ni pande 2 na za baba ni final n conclusive.
Mkuu, kwa sasa sina mpango wa kuoa, alikuja kumleta mtoto Bibi yake amuone tu na si vinginevyo
 
Ni kweli sio kila kitu lazima mzazi ashauri, lakini jambo kama hili ni muhimu kumpa nafasi ya kushauri, pia Mama yangu ni mtu wa hekima sana, namuamini katika maamuzi yake
Ni kweli mama yako ni mtu wa hekima sana, lakini ulitakiwa kumpa hyo nafasi kabla hujamtia mimba huyo binti.

Kwa sasa hekimq ni kumuoa huyo bint and make familly out of her.
 
Ni kweli mama yako ni mtu wa hekima sana, lakini ulitakiwa kumpa hyo nafasi kabla hujamtia mimba huyo binti.

Kwa sasa hekimq ni kumuoa huyo bint and make familly out of her.
Kumuoa ni jambo ambalo linahitaji muda kidogo, kwa sasa sipo tayari kuanzisha familia
 
Kuna mambo nayaona katika jamii, hua najisemea kuzaliwa mwanamke ni mtihani mkubwa sana.

Hili la mleta maada ni moja wapo.
 
Nimekutusi moyoni ......

Alafu badae mnakuja kuwakandia ma single mama hapa.

Ukilifanya hili unalotaka kulifanya na zaburi 109 na iwe juu yako
 
Umeshazaa nae mpaka home umempeleka na kama hana shida yoyote ile binafsi then unataka umuache kwasababu hiyo,mkuu utakuaumemtendea ukatili wahali ya juu sana.
 
Akikutia bisu la kifua, muanze kusema wanawake wana roho mbaya.
Umazalishe, ukamtambulishe kwenu afu umuache kisa mama kasema, dadeki
 
Kuna mambo nayaona katika jamii, hua najisemea kuzaliwa mwanamke ni mtihani mkubwa sana.

Hili la mleta maada ni moja wapo.
Sawa, ila mimi sina tatizo na mzazi mwenzangu, tunaelewana vizuri na naamini tutakuwa pamoja ila tu lazima nimuulize bimkubwa maoni yake
 
1. Mzazi ni mama tu
2. Baba hayupo
3. Bado hajanipa viashiria na nitamuuliza aniambie
4. Tayari nimezaa na siku hazirudi nyuma
5.sina mpango wa kuoa kwa sasa mpaka nimalize masomo
1.unawezaje kuamini mawazo ya mtu mmoja mama tu?,huoni kama atakua bias?
2.hauna watu wengine wakubwa kwenye familia na kwenye koo zenu?
3.sasa hauna mpango wa kuoa hadi umalize shule kwa nini umeleta huu Uzi hapa?,si usubirie hadi umalize shule ndio uje kuomba ushauri?
 
sasa hauna mpango wa kuoa hadi umalize shule kwa nini umeleta huu Uzi hapa?,si usubirie hadi umalize shule ndio uje kuomba ushauri?
Kila mtu ana uhuru wa kuleta uzi wowote kwa wakati wowote, ilimradi asivunje sheria za jukwaa
 
Vita ya Mke na Mzaa chema (Mkwe wa kike) huwa ni ngumu sana.
Hutoboi mkuu "as long as" Mama yako yupo hai, muoe ila hakuna rangi ataacha kuona huyo mkeo.
 
Umeshazaa nae mpaka home umempeleka na kama hana shida yoyote ile binafsi then unataka umuache kwasababu hiyo,mkuu utakuaumemtendea ukatili wahali ya juu sana.
Hayo siyo maneno yangu, umetunga uongo.

Sijasema hana shida yoyote, ila nimesema nahisi Mama kuna vitu ameviona, na nataka nimuulize aniambie
 
Vita ya Mke na Mzaa chema (Mkwe wa kike) huwa ni ngumu sana.
Hutoboi mkuu "as long as" Mama yako yupo hai, muoe ila hakuna rangi ataacha kuona huyo mkeo.
Lazima niongee na Mzazi wangu kwanza, pia swala la kuoa ni baadae na sio sasa
 
Hayo siyo maneno yangu, umetunga uongo.

Sijasema hana shida yoyote, ila nimesema nahisi Mama kuna vitu ameviona, na nataka nimuulize aniambie
Umeona neno "kama hana shida yoyote" au kiswahili sio ligha yako boss?
 
Umeona neno "kama hana shida yoyote" au kiswahili sio ligha yako boss?
Nimesema mwanzo alikuja na akaookelewa na akaishi bila shida yoyote, sijamaanisha kwamba hivyo ulivosema wewe
 
Back
Top Bottom