Mzazi wangu hajaridhika na mchumba wangu, hajasema lakini nimeona ishara

Mzazi wangu hajaridhika na mchumba wangu, hajasema lakini nimeona ishara

Ni kweli sio kila kitu lazima mzazi ashauri, lakini jambo kama hili ni muhimu kumpa nafasi ya kushauri, pia Mama yangu ni mtu wa hekima sana, namuamini katika maamuzi yake
Ukitaka kujua mwenye hekima na maamuzi siyo mama yako tu, nenda kakae na wewe week moja ukweni kwako(achana na miezi kadhaa).

Uone kama wazazi wake watakubali mtoto wao aolewe na mme kama wewe, yawezekana we ndiyo ukawa na mapungufu mengi kuliko huyo demu.
 
I already think like a Man, there is no need to watch anything
You don't think like one. You think like Mama's boy.

1. You draw conclusions that your mom dislikes your woman ilhali she never even mentioned it. Mbona usi-man up and ask her?

2. You want to 'single-mom' the mama of your child to please yourself through your mama? You are selfish.
Hatutaki more single moms mtaani kwa sababu weak kihivyo.

3. You can't make important family decisions on your own. You need to rely on what your mom thinks and what JF user have to tell you?

What kind of a man to thinks like this?

Unaharibu ndugu. Think like a man.
 
Ukitaka kujua mwenye hekima na maamuzi siyo mama yako tu, nenda kakae na wewe week moja ukweni kwako(achana na miezi kadhaa).

Uone kama wazazi wake watakubali mtoto wao aolewe na mme kama wewe, yawezekana we ndiyo ukawa na mapungufu mengi kuliko huyo demu.
Mimi mapungufu ninayo na Mama yangu anayajua, huenda ameona nitampa shida mtoto wa watu kwahiyo anataka kumuokoa na mapungufu yangu
 
"Watoto wa mama tunawavisha kanga..."

Katika sauti ya Dogo Janja.
 
Sa hapa unataka tukusaidieje? Au ni taarifa tu unatupa sie washkaji zako?
Nimeomba ushauri na nimeipata naufanyia kazi, kama wewe huna maoni kwenye hili ni afadhali ukae kimya
 
Kaa na Mama muulize vizuri, naamini kuna kitu ameona na hawezi ruhusu uingie pabaya. Usiogope kwa maneno ya humu, Mama yako mpe thamani na usiache kumsikiliza.
Nashukuru sana mkuu kwa ushauri mzuri, pamoja sana
 
Anae oa ni mama yako au wewe? Ukitaka wa kufanana nae tabia oa dada yako ambae mmelelewa na mama mmoja.

Sorry mkuu kwa komenti zangu nahisi nimeanza kulewa usisahau leo weekend.
 
You don't think like one. You think like Mama's boy

What kind of a man to thinks like this?

Unaharibu ndugu. Think like a man.
Brother, Mimi najua ninacho kifanya, kuleta hii mada humu Jf ni maamuzi yangu pia, pia siwezi kuacha kumsikiliza Mama yangu.
 
Yukosahihi ,na alitamani kuona mjukuu kama ulivyosema ajiridhishe ni wako...... Mwanamke Bora hazalii nyumbani
 
Yukosahihi ,na alitamani kuona mjukuu kama ulivyosema ajiridhishe ni wako...... Mwanamke Bora hazalii nyumbani
Naamini nikikaa nae na kumuuliza atanipa sababu zote, na mimi nitazipima na kuona zina uhalisia gani
 
Brother, Mimi najua ninacho kifanya, kuleta hii mada humu Jf ni maamuzi yangu pia, pia siwezi kuacha kumsikiliza Mama yangu.
Sure mkuu, usimpuuze mama ako kama ana hoja za msingi, kumbuka mambo yakialibika mama ako atakua upande wako hata kama yeye ndie chanzo tofauti na mwanamke ambae atakukimbia.

Nina mshkaji alibadilisha dini ili aoe, wana tukamkataza, tulimwambia mwanamke ndie amfate au wafunge ndoa kisheria tu kila mtu abaki na dini yake., mwana akatuchomolea wana, maisha yameenda akafukuzwa kazi, mkewe akadai talaka akaenda kuolewa na mwanaume mwingine mpaka mtoto waliezaa akamwandikisha ubini wa mwanaume uyo mwingine alieolewa nae.

Mshakaji aliishi na sress akaingia kwenye ulevi mpaka alikuja kufa kwa sababu ya pombe, alifululiza siku 3 anakunywa pombe kali bila kula, siku ya tatu ile kumuamsha haamki tukambeba mpaka hospitali kuchukua vipimo dokta akatuambia jamaa tayari ashakata moto.

Hata siku moja usipuuze ushauri wa mzazi au rafiki zako wa karibu kwa sababu ya mwanamke.
 
Back
Top Bottom