Mzazi wangu hajaridhika na mchumba wangu, hajasema lakini nimeona ishara

Yani wewe ni tatizo kubwa wewe huwezi kujenga mji wako kamwe na hakuna mwanamke wa kuvumilia ujinga wako uo inaonekana kila jambo lako lazima lipitishwe na Mama yako nakupa pole sana
Mama yangu ni Nguzo yangu, Angekuweopo baba huenda ningekuwa na mshauri mzuri zaidi lakini nimebaki na Mama na siwezi kumpinga
 
Madhara gani? Mimi nafurahi kuwa na mtoto na sioni kama napaswa kujuta au kulaumu, hakuna kitu mtoto amekosa, kama ni malezi yapo tena mazuri tu
Mtoto amepata baba mjinga asiyejielewa, laiti huyo mtoto angefahamu kuwa Una mpango wa kumtelekeza mama yake
 
1.Mzazi wako ni mama tu?
2.baba yako anasemaje?
3.Viashiria vipi umeviona?
4.kwa nini umezaa ndio unataka uoe?
5.kwa hio,huyo atayaridhika naye mama yako naye utazaa naye kisha ndio utamuoa?
Ukiweza kujibu hayo maswali kutoka moyoni,una 97% za kutatua kinachokusumbua
 
Unahitaji msaada wa kisaikolojia tunza comment yangu ipo siku utajutia kwa kuharibu familia yako ili kufurahisha familia ya Mama yako
Kuharibu familia yangu kivipi? Hata mama yangu ni familia yangu
 
Mama yangu ni Nguzo yangu, Angekuweopo baba huenda ningekuwa na mshauri mzuri zaidi lakini nimebaki na Mama na siwezi kumpinga
Ndio shida ya kulelewa na Single Mother yani ni kama umeharibika kisaikolojia nakuonea huruma sana upo controlled na Mama yako ukihitaji msaada wa kujitambua utasema nikusaidie maana akili zako zimeshikwa na Mama yako
 
Kuharibu familia yangu kivipi? Hata mama yangu ni familia yangu
Mama yako ni mzazi wako na ana familia yake lakini uyo binti ulie zaa nae uyo na mtoto ao ndio familia yako kwasasa inatakiwa uijenge vizuri na kama unataka kuendelea kua familia ya mama yako basi usinge mpa mimba uyo binti ungekaa kwenu na Mama yako mfurahie maisha yenu
 
1. Mzazi ni mama tu
2. Baba hayupo
3. Bado hajanipa viashiria na nitamuuliza aniambie
4. Tayari nimezaa na siku hazirudi nyuma
5.sina mpango wa kuoa kwa sasa mpaka nimalize masomo
 
Ndio shida ya kulelewa na Single Mother yani ni kama umeharibika kisaikolojia nakuonea huruma sana upo controlled na Mama yako ukihitaji msaada wa kujitambua utasema nikusaidie maana akili zako zimeshikwa na Mama yako
Mama yangu ni nguzo yangu
 
Mama akiniambia sababu na mimi nitazichunguza, nikiona ni sahihi nitafanya maamuzi
🤣🤣🤣🤣 Nishaona tuna hangaika kushauri mbuzi kuacha kula manyasi aya kila la kheri kwenye maisha yako ya hovyo ayo
 
Sasa kiherehere gani kilikupeleka kuharibu maisha ya uyo binti si ungekaa na uyo nguzo yako kivyenu yani wewe akili huna kabisa
Nimeharibu maisha yake kivipi? Mbona bado anaishi vizuri tu na hana tatizo
 
Kwanza hujaeleza baba yako yupo wapi, kama amekufa baba mdogo/mkubwa wanasemaje? Baraka hazitoki kwa mzazi mmoja tu wa kike peke yake. Baraka ni pande 2 na za baba ni final n conclusive.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…