Jackwillpower
JF-Expert Member
- Oct 4, 2017
- 2,467
- 3,687
Katika Qurani yenye jumla ya juzuu 30; Surah 114; aya 6236; maneno yenye kutamkia 76,440; herufi 322,373; jina Isa linatamkwa lisa au Aysi limetajwa mara 25. Isa pia ameitwa masihi mara 93. Lakini tunaposoma Qurani iliofarsiriwa/tafsiriwa na Imam Baidawi Vol 1 Ukurasa 160 ameeleza kuwa Isa jina la Kiarabu maana yake ni Wekundu unaozidiana na weupe. Hii ndio maana ya Jina la Isa wa Quran. Je, Yesu wa Biblia maana yake nini?maana kwenye Uislam hYesu alyahi salaam pia ni mtume.
JINA LA YESU MAANA YAKE NINI?JINA Yesu linatokana na lugha ya Kiebrania ‘Yehoshua’ katika lugha ya Kigiriki wanasema ‘lesous’ inatamka ‘Yesous’ yaani Yesu. Katika lugha ya Kiarabu wanasema ‘Yasu’, kwa kiingereza ni “Jesus” maana yake ‘Bwana anaokoa au Bwana ni Mwokozi’ Isaya 43:6, 10-11.
Katika Biblia ambayo ina jumla ya Sura 1189; aya 31,102; vitabu 66 – Agano la kale vitabu 39 na agano Jipya vitabu 27; Neno Mwokozi kwa Kiingereza wanasema ‘Saviour’ limetajwa mara 55. Ikumbukwe kwamba katika agano jiypa jina Yesu au Yehoshua (kwa Kiebrania) limetajwa mara 1275 katika aya zipatazo 1226.
Zingatia pia kuwa agano jipya lina jumla ya aya 7930 na sura 260 hivyo hapa tunaona jina Yesu maana yake ni Mwokozi na jina Isa ni wekundu uliozidiana na weupe. Kwa kuwa maana ya haya majina tofauti bila shaka Isa sio Bwana Yesu.