Wa aina yako tuko wengi, ni mtu pekee aliye hai niliyewahi kumliliaMimi ile September 7, 2017 niliona hapa JF kwanza kwamba Lissu kapigwa risasi na hali yake ni mbaya sana. Nilijua ni uongo wa buku 7 hivyo sikuamini ila nikawa busy kwenye simu kutafuta ukweli. Nilipofahamu kama ni kweli nililia kama mtoto hata sijui machozi yalitokea wapi. Mwenyezi Mungu ni mkubwa.
Umesema kwa uchungu sana mkuu.Yani nikiona bongo fleva wanavyonyang'anyana peremende za CCM halafu kule Nigeria wasanii wana mahela lakini bado wanatumia ushawishi wao kuchochea mabadiliko kwenye jamii na mifumo ya nchi nasikia hasira mpka natamani kupiga ngumi ukuta…
Sent using Jamii Forums mobile app