Kuna siku nilikuwa nipo sehemu. Watu wakawa wanapiga stori kuhusu wamama kuwafungia vioo waume zao kwa watoto wao ili wasipate msaada. Yaani mama anawaambia watoto wake kuwa baba yenu mkimtumia hela anaimalizia kwa wanawake, pombe etc. ili mradi tu mme wake hasitumiwe hela. Muda mwingine maneno anayosema kwa watoto si ya kweli bali yakutunga au anatia chumvi.
Baada ya hayo maongezi kuna Mzee mmoja alianza kulia maana alikuwa anapitia hiyo hali. Akasema ana maumivu moyoni kwani aliipambania sana familia yake. Watoto wake wamefika hapo walipo kwa nguvu zake hadi wakawa na maisha yao ila inamuumiza kwa kumbagua katika uzee wake. Mke wake kawatia sumu watoto, na watoto wameingia kwenye mfumo. Hela wanamtumia mama yao kwahiyo Mzee akitaka hela inabidi amwombe mke wake. Anaipata kwa masimango.
Ushauri

- Watoto badilikeni acha kusikiliza maneno ya mama zenu. Baba zenu katika uzee wao wana mahitaji yao binafsi. Kama unatuma tuma kwa wote bila ubaguzi.
- Waazee watarajiwa weka vitega-uchumi vyako ili husiwe tegemezi kwa watoto. Hii itakusaidia kufurahia uzee wako.