Kutokana na uchu na tamaa ya madaraka mzee wangu Abdalah Bulembo na wengine wanakuita alhaji ulitoa kauli ambayo iliishtua dunia na pengine dunia kuamini Tanzania ni nchi ambayo serikali inaua watu wanaohoji pesa za miradi
Kufuatia mkopo wa benki ya dunia(WB) kwenye mambo mbalimbali ambayo yangechochea maendeleo hususani suala la watoto wa like waliopata ujauzito kurudi shule ambalo ni suala ambalo uongozi uliopita haukuliona lipo sawa, zitto kabwe aliitoa maoni yake juu ya sharti hilo kutofanyika kwa kilichokusudiwa kwa mkopo huo na kuomba usitishwe.
Kufuatia maoni hayo ya zitto tarehe 03/02/2020 mzee bulembo ulitoa kauli hii, nanukuu: "Kuna mtu mmoja aliyechukua maswala yetu ya ndani na kuyapeleka nje ya taifa , hafai kuruhusiwa kurudi na anafaa kuuawa pale alipo .Uhaini! kile ambacho bwana Zitto Kabwe amekuwa akilifanyia taifa hili ni uhaini''.
Kauli yako hii ingeweza kuwa ni chanzo cha kuvunjika kwa mahusiano yote ya kimataifa lakini haikuwa hivyo hivo kwa uongozi unaosema ulivunja mahusiano hayo ulijitahidi kwa gharama yoyote kuyalinda. Hakuna mahali popote Rais Magufuli au waziri Kabudi aliwahi kutotoa kauli yenye kuhatarisha na kuchochea kuvunjika kwa mahusiano hayo ila ni wewe ulifanya hivyo kwa sababu ya uchu ulionao wa madaraka.
Napenda kukumbusha tu mzee bulembo katika uongozi wa hayati Magufuli mahusiano yetu na nchi nyingine yalikuwa ni imara sana hivyo tunajisikia aibu mzee kama wewe unapojaribu kupotosha umma kwa maslahi ya tumbo lako.
Tunaomba ukae kimya na uache kumuongelea vibaya hayati Magufuli kwa sababu utaishia kudhalilika na kuabika hata kwa wajukuu zako ambao wanaona mazuri yake kwa nchi hii.
Amelifanyia nini hili taifa huyu Bulembo.
Polepole anapigania haki za Watanzania kujieleza, kujitambua na kutambua haki zao.
Anatoa Elimu juu ya , haki, misingi, chanzo, maana ya demokrasia.
Watu wamebaki kumpinga kwa mipasho,KY jelly walioiweka wao, ili kuwatoa watu kwenye hoja.
Mmevamia nyumba yake, mmeiba TV, mmeweka KY mezani muipige picha, mmetupa vitu vyake vyote kama toilet papers, towel, kila kitu ili kumdhalilisha , kuondoa crecibility yake.
Hoja hata moja hamjawahi kuijibu. Kimsingi anasema hakuna awamu ya sita, ni kwamba anakwambia kiongozi aliondoka ni Mmoja JPM. Wote walikuwa wasaidizi wake, walipigania timu moja, sera moja. kitu kimoja. Awamu hii haikuchanguliwa upya na sera mpya, bali wanatekeleza sera za awamu ya tano.
Sasa hivi wanasema kila kibaya ni cha awamu ya Tano, Wakati walikuwa wasaidizi wakuu. Kila kizuri ni awamu ya sita.
Hata mkimuua Polepole, itakuwa ni sawa tu, yeye alishaamua kujitoa kutetea Watanzania mkisema ni gay ni sawa, wana propaganda za kitoto sana. Sababu kubwa hawana uwezo wa kujenga hoja.