Mzee Frederick Tluway Sumaye ajiondoa CHADEMA. Asema mambo yamembadilikia CHADEMA baada ya kuchukua fomu kugombea Uenyekiti Taifa

Mzee Frederick Tluway Sumaye ajiondoa CHADEMA. Asema mambo yamembadilikia CHADEMA baada ya kuchukua fomu kugombea Uenyekiti Taifa

Wote tumemsikia aliyepata kuwa waziri mkuu wa Tanzania kwa kipindi cha miaka 10 mfululizo, akiongea na waandishi wa habari mzee wetu Fredrick Sumaye ameongea mengi na kwa hisia zilizo changanyikana na machungu ndani yake.

Sumaye ametangaza kujiondoa kutoka chama kikuu hicho cha upinzani nchini kwa sababu ndani ya chama hicho hakuna demokrasia ya kweli ile ambayo wanaihubiri kwa watu, anaendlea kusema kuwa amefanyiwa figisufigisu kisa tu alichukua fomu ya kugombea nafasi ya uenyekiti wa chama hicho ngazi ya Taifa, kuna wajumbe walifichwa hotelini na wengine kupigiwa simu na kupewa rushwa ili tu kumpigia kura za hapana.

Sumaye anasema Mbowe aliwahi kumwambia kuwa sumu haionjwi kwa kuilamba na yeye kwa usalama wa uhai wake na familia yake ameamua kujondoa ndani ya chama hicho ili tu Mbowe angombee mwenyewe nafasi ya uenyekiti.
Yoyote anae jaribu ama kutaka kugombea nafasi ya uenyekiti basi atakumbana na fitina na hujuma za kutisha kutoka kwa Mbowe na watu wanaomzunguka, huku yeye akidhani hao wanaomzunguka wnamsaidia lakini wanakiangamiza chama.

Sumaye anaendelea kusema Prof. Safari alipotoa ushauri aliambulia matusi na kejeli kutoka kwa viongozi na wanachma wa CHADEMA, sasa hivi ukitoa maoni tofauti na wanavyofikiria wao ama ukikosoa basi utaitwa msaliti na matusi kibao CHADEMA wao kila kitu wapo sahihi hawakosei na wala hawajawah kukiri kosa.

Wengine tulijaribu kutahadharisha humu kugombea unyekiti CHADEMA ni sawa na ngamia kupita kwenye tundu la sindano kitu ambacho ni kigumu na hakiwezekani wote waliogombea uenyekiti. Walichokutana nacho mungu tu ndo anajua.

Who is next?
 
Tumeona kwa Zitto, sasa kwa Sumaye, unataka kusema Zitto nae hakuaminiwa Chadema? Tatizo ni Mbowe sio mtu yeyote
Sasa,hebu twende polepole sumaye kachukua fomu,hakuna mtu kamzuia,kajaza karudisha,
Lakini anajua wazi kwenye kura hataweza kumshinda Mbowe.

Kaamua kujitoa mwenyewe na kudai eti mbowe kamwambia sumu haionjwi,hatuambii hayo maneno kaambiwa lini na katika mazingira yapi.

Na pengine angwtuwekea hata audio Basi wakati mbowe akimwambia "sumaye,acha kugombea umwenyekiti,sumu haionjwi, usithubutu"
 
"Leo natangaza kuwa hiyo safari ya kugombea uenyekiti wa ngazi ya taifa naisitisha leo, kwa usalama wangu na familia kwa ujumla na Mbowe aliwahi kunitahadharisha kuwa sumu haionjwi kwa ulimi namimi sitaki kuionja" - Frederick Sumaye
Tukisema Mbowe ni dictator nyumbu hawaelewi, ila sasa wanaanza kuelewa, kilichomkuta Zitto ndio kimemkuta Sumaye, huko CDM ukitaka tu kugombea uenyekiti - taifa, lazima ufukuzwe au utaitwa msaliti au utazimwa ktk kura za awali ndani ya CDM
 
TETESI;
Secretariate ya Halmashauri kuu ya CCM kukutana kwa dharula Leo hii kujadili kujitoa kwa Sumaye kugombea uenyekiti na chama.
Hili limeonekana ni pigo kubwa la kufungia mwaka kwa CCM.
Swali;
Kwa nini ajitoe Chadema maumivu yawe kwa ccm?
 
Daudi Mchambuzi unamsikia mzee Sumaye, kazi ya upinzani ni kuifanya CCM isilale usingizi na siyo kushika Dola...... Uwepo wa Upinzani mnufaika namba 1 ni CCM!
Kumbe unaniwaza ehh???

CCM sio namba 1 ndiyo maana inabidi watendeji waitwe ikulu na kuagizwa waharibu form za wagombea wa upinzani.
 
Yaani Sumaye alikua na nia ya kuinyima usingizi CCM, ili iweje kwa mfano?
 
Hayo ni maneno ya mkosaji mbona wengine walishindwa hawaongei lengo lake halijatimia ndo hasira zake hizo binafsi naona kama hasira tuu na jazba zimemjaa
 
Roving Journalist,

HAKUNA ALIYE MAKINI ATAKAYEBAKI CDM.

Ilikuwa ni suala la muda tu; hakuna mtu aliye makini atasalia huko. CDM ni jahazi linalozama. Nahodha hataki kusaidiwa; ameg'ang'ania usukani.
 
Mbowe kwanini anahitaji zaidi uenyekiti kina zito waliletewa zengwe kwa hiyo nafasi chacha wangwe mnayajua sasa kwanini linapokuja swala la uenyekiti mbowe n

Anajimwambafai chama miaka 15 mwenyekiti mmoja eti kisingizio kwamba demokrasia inamajaribu kwani atafanya nini kuibadili hii hali ya sasa? Na wallahi naapa mbowe hatopata majibo hata 20 mwakani 2020 na atakuja na utetezi wake wa kura kuibiwa mbowe ni dunderhead na hana jipya zaidi sana kula fedha za wabunge chadema inamuhitaji kila mtu ila mbowe anajiona ye ndio anahitajika zaidi chadema kuliko yeyote
 
Halafu mtu anakuja na mapovu mengi tu akisema JPM ni dikteta, kiongozi ambaye mpaka dakika hii yupo katika nafasi yake kwa mujibu wa katiba aliyoapa kuilinda.

Huyo anayewaambia wenzake sumu hailambwi akipewa nafasi pale magogoni atafanya unyama mkubwa kiasi gani!, ni katika kutafakari tu.
 
HAKUNA ALIYE MAKINI ATAKAYEBAKI CDM.

Ilikuwa ni suala la muda tu; hakuna mtu aliye makini atasalia huko. CDM ni jahazi linalozama. Nahodha hataki kusaidiwa; ameg'ang'ania usukani.
Nope,si suala la kumpa mtu yeyote hata asiejulukana uenyekiti,after all hakuna mtu kazuiwa.
Chadema in watu wenye capacity ya kumrithi mbowe,watu Kama Henche,mnyika Tundu Lissu,halima etc.
Watu wenye damu ya chadema,SI mtu anakuja wiki hii,anataka awe mgombea pekee was uenyekiti
Sumaye is not serious
 
Halafu mtu anakuja na mapovu mengi tu akisema JPM ni dikteta, kiongozi ambaye mpaka dakika hii yupo katika nafasi yake kwa mujibu wa katiba aliyoapa kuilinda.

Huyo anayewaambia wenzake sumu hailambwi akipewa nafasi pale magogoni atafanya unyama mkubwa kiasi gani!, ni katika kutafakari tu.

Ninavyompenda Dr Magufuli mimi jamani...... yaani mtu akimsemea ubaya namwona kama adui mkubwa wa maendeleo ya nchi hii
 
Back
Top Bottom