Mzee Frederick Tluway Sumaye ajiondoa CHADEMA. Asema mambo yamembadilikia CHADEMA baada ya kuchukua fomu kugombea Uenyekiti Taifa

Mzee Frederick Tluway Sumaye ajiondoa CHADEMA. Asema mambo yamembadilikia CHADEMA baada ya kuchukua fomu kugombea Uenyekiti Taifa

Tamaa zake tu hizo! Amekaa "nyumbani" miaka 10 akipata marupurupu yote, kamaliza huo mda kaenda upinzani eti kuuimarisha! Hawaoni wakuu wenziwe akina Cigwiyemisi, Mtoto wa mlimaji, Mzee wa kule kwenye mlima mrefu ambaye sasa ni mwenyekiti wa KDF (kama sijakosea), wanetulia!! Tamaa lazima zidhibitiwe, angalia sasa amegusa kiti cha DJ, ameipata!!
 
Mzee anasaka fursa kivingine baada ya kunyea ile kambi ya intarahamwe, akajaribu kuzamia meli ya wagiriki maana alikuwa haelewani na wavietcong wa vietnam..

Wagiriki bwana nao hawana urafiki wakamtosa mzee deep sea na boya lake anajaribu kuelea elea kabla ya kuomba msaada kwa intarahamwe wenzie maana ana passport na uraia wa kule...

Watalebani sidhani kama watamuokoa maana wale wanakaurafiki fulani na Wagiriki ila kuna mahala kidogo hawaelewanagi..

Ila kwasasa Watalebani wakiungana na Wagiriki hali inaweza kuwa mbaya kwa intarahamwe maana inaonekana intarahamwe na wale wavietkong wa vietnam wanapasuana kimyakimya na kunahatari hawa wavietkong wakatoa msaada kwenye hii combination ya Watalebani na Wagiriki..

2020 is around the corner lets get ready...
 
Hakuna wanasiasa waliwekeza pesa nyingi chadema Kama Lowasa na Sumaye.Sumaye kajenga Hadi makao.makuu ya Kanda Ofisi nzuri kuliko ya makao makuu.Lakini chadema hawana shukrani naye.Lowasa kaingiza wabunge wengi na madiwani Leo hi Lowasa anaonekana si lolote si chochote Chadema

Haya chadema bakini na wakereketwa wasiochangia fedha na Mali akina Mdude,ole sosopi na akina Sugu.Matajiri timukeni chadema kabla hayajawakuta ya Lowasa na sumaye
 
GENTAMYCINE,
Na hapa mimi bado nachambua tusi nikutukane. Watu gani mnashabikia akili za wagonjwa wanatuharibia nchi?
 
Kama Sumaye anataka democrasia ya kweli akagombee nafasi ya uenyekiti wa ccm ya Dr. John Pombe Joseph Magufuli.
 
Nilitaka kuondoa hisia za hakuna Demokrasia ndani ya chama na nafasi ya uenyekiti wa CHADEMA hauguswi ndio maana nikachukua fomu, kumbe nilifikiri vibaya.

Kama mkipiga kura kama mlivyopanga, mtakuwa mmeudhihirishia umma kwamba nafasi ya Mbowe haiguswi. Walidhani wananikomoa mimi bali wameharibu Taswira ya chama. Mbowe, hao watu wa cabinet yako wanakudanganya

Nasitisha rasmi kugombea nafasi ya Uenyekiti. Kwa Usalama wangu. Tulipokuwa Arusha Mbowe alituambia Sumu haionjwi kwa kuilamba nami sitaki kuilamba.



Over!
 
Kama sumaye anataka democrasia ya kweli akagombee nafasi ya uenyekiti wa ccm ya Dr. John pombe Joseph magufuli.
Uchaguzi bado,inaruhusiwa kabisa,katoka Kikwete kaja magufuli,lakini katoka M kaja M,biashara hii inaruhusiwa ?
 
Bado wa kanda ya kati naye tuna mzoom tu, ahsante lema kwa kazi nzuri, waziri kivuli wa mambo ya ndani.
 
Sumaye kamwanga manyanga mwenyewe kugombea Uenyekiti.Kaogopa kumfuata Chacha Wangwe kaburini. Mbowe ni dictator.
Jamani kumbe nchi hii kila kona ni madikteta tu

CHADEMA kwishinehi.
 
Hivi kama alikosa uenyekiti wa kanda si angesubiri wa Taifa upite ndio aamue kwamba CDM haina demokrasia au la? Kama kwa miaka aliyokaa cdm hakuweza kupanga safu hata ya kanda, basi huyu ni yule yule mr Ziro wa MH Mkapa aka fundi mchundo. A loose point kwenye mikakati yake, amekurupukaaa. Unaumizwa kwa jambo la kujitakia.? Halafu ningekuwa mm afadhal. Mbona ulikuwa juu? Tena kwa miaka 10?
 
Back
Top Bottom