Mzee Jakaya Kikwete, rudisha hilo hekalu Serikalini lipigwe mnada pesa zisaidie wananchi

Mtamuonea bure tu, Kikwete alijijengea nyumba yake kule msoga kijijini kwao na akahamia huko alipotoka State House.

Hii Sheria ilikuwepo Ila hakutaka kutumia pesa zenu Ila alipokuja Magufuli aliamua kutekeleza hiyo sheria kwa kuwajengea wastaafu wote nyumba kama stahikk ya kisheria kwa Marais wastaafu.

Hata mzee Mwinyi hakujijengea nyumba ambayo ni stahiki yake, alitumia fedha zake kujenga nyumba yake.

Magufuli ndio aliamua kuwajengea nyumba Marais wastaafu wote, sasa unaanzaje kumtaka Kikwete arudishe nyumba?

Lawama ziende kwa aliyeamua kuwajengea.
 
Aiseee! Kumbe Tanzania ni kubwa. How did you know, even, kwamba nina hivo vitu vyako!??

Aiseee! Kumbe Tanzania ni kubwa. How did you know, even, kwamba nina hivo vitu vyako!???
Kama huna unayo ile nyingine.Waache wafu wapumzike wameimaliza kazi Yao.Sio kila dk sijui angekuwa Fulani angepiga cm,Jana imepita na mambo yake uwezi irudisha mama anaendelea kwa ajili ya kesho ya Tanzania.
 
Ni nyumba ya kawaida sana. Wala si hekalu kama inavyosemwa.
 


Najua unamtetea mstaafu na mstaafu mwenzie. But, frankly, ^hawateteki^ Don't tell me hawana brain!??? Hawajui maisha ya Watanzania!??? For your information, wao ndio force behind ujenzi kukamilishwa. Like I hear someone's voice telling JPM: ^Mzee sasa kwa vile almost kila kitu umechukua, basi isiwe taabu. Tutimizie kile kipengele cha Katiba kwa wastaafu.^ JPM might have done it just to help save their lives some few more days, who knows!???
 
Kama huna unayo ile nyingine.Waache wafu wapumzike wameimaliza kazi Yao.Sio kila dk sijui angekuwa Fulani angepiga cm,Jana imepita na mambo yake uwezi irudisha mama anaendelea kwa ajili ya kesho ya Tanzania.

JPM is going nowhere --- there is a whole army of his own renewed incarnation. Stay tuned Mr Tiny Little Brain!!!
 
Hakulazimishwa kuipokea, angeweza kukataa kujengewa hiyo nyumba tena kwa maandishi na hoja za wazi kuwa haihitaji na serikali ingemsikiliza!

Lakini tunamlaumu kwa sababu sheria hiyo ilitungwa wakati wa Mkapa lakini yeye Kikwete wakati akiwa ni rais angeweza kuirekebisha au kuifuta lakini aliiacha tu.

Kitendo cha kuiacha maana yake kinatoa room kwa mstaafu yoyote in the future kuandika barua serikali kudai mjumba hata kama ana majumba 100
 
Basi kama yeye hakuifuta hata Magufuli angeweza kuifuta tu. Naona mmeamua tu kutafuta wa kumtupia maneno.
 
mzee hio yote ni sawa.mbona ni bahat kuwa na viongoz wanaopewa msaada wa makaz.nchi zingine za kiafrika unakuta wangekua na mahekalu.wazee wetu wapumzike kwa amani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Magufuli hayuko hai, hatuwezi kumuandikia barua ya wazi akaisoma
Lakini ndio alianzisha mchakato wa kujenga hizo nyumba na alishasema viongozi waliomtangulia waache kuwashwawashwa so ulitaka waanze kumuingilia kwenye masuala ya uongozi wake? Let's be honest kwenye hili hata wewe usingekataa maana unakataa kwa sababu zipi?

Mwishowe angeonekana amesusa napo mngesema mwacheni bana , aliyepata kapata tu.
 
Kama ni muungwana alirudishe kwa umma, lipigwe mnada pesa zikasaidie kutatua kero za wananchi. Yeye ana mijumba mingi hana uhitaji huo wa kukamua wananchi kujengewa nyumba nyingine
 
Jamani tusiwalaumu kwanza bali turekebishe sheria inayoruhusu wajengewe hizo nyumba ifutwe. Ukigombana na JK sasa utagombana na wangapi?
 
Kama ni muungwana alirudishe kwa umma, lipigwe mnada pesa zikasaidie kutatua kero za wananchi. Yeye ana mijumba mingi hana uhitaji huo wa kukamua wananchi kujengewa nyumba nyingine
Hapana Mambo mengine yanakuwa kama wivu binafsi, mwacheni, he served the nation na hiyo ni stahiki aliyoikuta hata hakupitisha yeye hiyo sheria. Aliyepaswa kujua haya no aliyemjengea.

Amejitoa sana tu, kajenga shule za kata, dispensary, vijana walipata mikopo ya chuo pamoja na kuhakikisha nchi inakuwa salama kwa kuwajali wapiganaji wetu na kulinda mipaka ya nchi pamoja na kuheshimu Katiba ya nchi.

Mwacheni hiyo ni pesa ndogo sana hata yeye anaweza kuitoa Ila kuna heshima yake kwa kiongozi wa nchi .

Tuwe na heshima wakati mwingine.
 
Is too late kulalama sasa. Hizi sheria zingewza kubadilishwa Bungeni. Lakini wakati Wapinani hasa CGADEMA wwakilalamika kubanwa ns Spiika au wanamna alivyoiuba uchaguzi na sisi tuka kaa kimya haya ndiyo matokeo yake. Wako wapi akina Lissu, Lema, Mbowe watete hoja hii Bungeni? Wapi Zitto Kanwe na Mnyika
 
Rais sio sehemu ya bunge ndio maana haingii bungeni ule muhimili mwingine hata akienda bungeni ni mpaka aalikwe na kifungu kitenguliwe kumruhusu kuingia, tuacheni na hayo sasa ulikuwa wapi kumwambia JPM wakati alipokuwa madarakani? Mambo ya mwinyi na Nyerere sote tunajuwa tulikuwa tunatoka katika Ujamaa kuja kwenye soko huria yalikuwa ni mambo yalazima na yaliishinishwa na CCM sio Mwinyi. Hizo ni chuki binafsi kwa JK hakutunga sheria hizo mlaumu aliyetunga. Wewe ungerudisha hiyo nyumbani? sisi unafiki na chuki ndio tumetawaliwa. Ogopa watu waliojificha nyuma ya udini na ujamaa hawa ni hatari sana.
 
Kama ni muungwana alirudishe kwa umma, lipigwe mnada pesa zikasaidie kutatua kero za wananchi. Yeye ana mijumba mingi hana uhitaji huo wa kukamua wananchi kujengewa nyumba nyingine
Halafu watu huwa tunaaminishwa Mambo ya mtaani tu, imagine hakuna aliyeamini Nyerere mpaka anastaafu hakuwa na nyumba ya maana zaidi Ile ya matofali ya kuchoma kule kwao kijijini.

Nachomaanisha ni kwamba, waweza kuhisi ana nyumba nyingi sana, unakuta anazo mbili tu ambapo kwa kiongozi wa nchi hazimtoshi sababu ana wageni wengi sana ukiacha ndugu wategemezi ambao hawezi kuishi nao nyumba moja.

Huyu alikuwa Rais wa nchi sio Rais wa wasafi media, let's give him the respect he deserves hata kama hamumpendi.

Same as Magufuli, pamoja amekufa Ila familia yake watajengewa nyumba pamoja nae ana majumba kibao aliyojimilikisha wakati wa kuuza nyumba za serikali, imagine lile kasri pale ADA estate, kule Chato na kwingine Ila bado nae atajengewa Tena pamoja amefariki Ila ni haki yake. So nayo mjiandae kukataa asijengewe sababu hayupo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…