Mzee Jakaya Kikwete, rudisha hilo hekalu Serikalini lipigwe mnada pesa zisaidie wananchi

Mbona unamlenga Mhe Kikwete pekee an kuwaacha Mwinyi na Mkapa? Hata hivyo naungana na hisia zako. Rais anayestaafu lazimahuwa amendaa nyumba atakapoishi baada ya kustaafu. Watu wanaoweza kuadhirikia wakastaafu bila na kuwa na nyumba ni watumishi wa umma lakini si Rais. Kama dhumuni la kwajengea marais wastaafu nyumba ili waishi humu historia inatuambia kwamba hilo halifanyiki, kwani Mzee Mwinyi haishi katika nyumba aliyojengewa. Hata Mh Mkapa alikuwa anaishi katika nyumba aliyojenga mwenyewe na si aliyojengewa na serikali. Maana yake ni nini? Maana yake ni kwamba hawazihitaji nyumba hizo. Sheria hii iangaliwe upya.
Wanajimegea tu keki ya Taifa bila kujali umasikini wa wananchi wetu
 
Kwani unadhani anaenda kuishi yeye mle...anakizazi chake ndiyo urithi huo
 
Ukweli hawa watu hawana hata mshipa wa aibu, wameiibia sana nchi hii yeye na familia yake still wanazidi kujineemesha kama vile walitumika kwakujitolea
 
Usishangae kusikia waliopeleka hiyo sheria ni haohao waliojengewa
 
Nani alikudanganya kuna kuchelewa katika kupinga dhuluma, wizi na ufisadi unaofanywa katika nchi yoyote ile dhidi ya raia!?
 
Ukweli hawa watu hawana hata mshipa wa aibu, wameiibia sana nchi hii yeye na familia yake still wanazidi kujineemesha kama vile walitumika kwakujitolea
Acha chuki jadili hoja! Kikwete ni Rais mstaafu wa nne kujengewa nyumba kwa mujibu wa sheria. Mwalimu, Mzee Mwinyi, Mzee Mkapa nao walijengewa. Hayo mengine yako msingi wake ni nini?
 
We jamaa MNAFIKI wa kiwango cha SGR!!

Yaani unaona suala la kupiga simu uwanjani ndo muhimu kuliko mamilioni ya wavuja jasho aliyoyatumia kuwajengea nyumba akina Kikwete?! Hivi zinakutosha kweli wewe?!

Halafu Misukule ya JPM mmeshikilia sana kwamba Jiwe angepiga simu! Kuna sheria ngapi, let alone kanuni zilizovunjwa pale bungeni wakati yeye akiwa hai?!

Au kwa akili yenu suala mechi ya Simba na Yanga ndo muhimu zaidi kuliko ushenzi unaondelea pale bungeni?! Au kwavile mnafahamu ni mtu wa kiki kwahiyo mnajua simu ya pale Mkapa Stadium ingempa mileage kubwa?
 


Ukimaliza kubwabwaja, njoeni na Bi Mkubwa wako, raia wanataka hela zao mlizowahadaa na kuwaghilimu, sawa!??? Nasikia ndizo mmetumia kumnunulia mstaafu wenu benzi ya mabilioni. Jiuzuluni, Watanzania wameshawasomeni wizi wenu!!!
 
Ukimaliza kubwabwaja, njoeni na Bi Mkubwa wako, raia wanataka hela zao mlizowahadaa na kuwaghilimu, sawa!??? Nasikia ndizo mmetumia kumnunulia mstaafu wenu benzi ya mabilioni. Jiuzuluni, Watanzania wameshawasomeni wizi wenu!!!
Tumechoka kabisa na wizi wa waziwazi mchana kweupe, tuna mahitaji mengi ya msingi, tulitegemea kodi zetu zielekezwe huko na siyo watu wachache au kikundi cha watu fulani kufanyia anasa kodi zetu
 
Mkuu, hatugombani nao. Ila tunataka watumie busara.
Jamani tusiwalaumu kwanza bali turekebishe sheria inayoruhusu wajengewe hizo nyumba ifutwe. Ukigombana na JK sasa utagombana na wangapi?
Mkuu kulaumu ni lazima. Hata kama sheria inaruhusu, busara ni lazima itumike. Hizo sheria walipendekeza kwa maslahi binafsi... Hicho ni kitu cha kukemewa na hizo sheria lazima zifutwe. Serikali inaweza kuwahudumia kama kawaida na siyo lazima wajimilikishe mali kwa mgongo wa kwa mujibu wa sheria. Kuna vitu vingi hata wafanyakazi wa serikali wanatakiwa kipara kwa mujibu wa shetia lakini hawapati kwa sababu ya hali yetu ya uchumi.

Viongozi Waliopata walitumia busara hawakufanya hayo mpaka yule bwana alipoingia maana yeye hakujali.
 
Nyerere kazi yake ya kwanza kwenye serikali ya Uhuru ni urais, uadilifu wake ulimfanya hata nyumba ya maana asiwe nayo.

Lakini hawa wengine wamekuwa wabunge kwanza, kisha mawaziri na baadae ndo urais, ina maana miaka yote hiyo hawana nyumba mpaka wangojee wajengewe nyumba kutokana na kushika kwao wadhifa wa urais?—Waisubiri nini kujenga kama hawana nyumba?

Hata kama ingekuwaje, hawa watu wana marupurupu mengi ambayo wamepewa kwa mujibu wa sheria, marupuruou ambayo Nyerere hakuyapata baada ya kustaafu maana Sheria hii ya marupurupu yaliyonona zaidi ilikuja baadae kipindi cha Utawala wa Mkapa, Kwa hiyo Nyerere hakuwa na fedha za Kujijengea Nyumba za maana kama hawa wa sasa ambao wana mipensheni minonominono kwelikweli!

Kwa hiyo hawa wastaafu wasitupe mzigo, waache mteremko, watumie mafao yao kujijengea mijumba kama wakitaka lakini wasitutwishe mizigo isiyobebeka
 
No one knows sidhani kama Bwana yule alikuwa eti mtu wakuambiwa tufanyie hivi.....kama aliamua Wastaafu wajengewe Nyumba nadhani aliamua Yeye kama yeye kumbuka aliwapa na zawadi ya Tausi wakiwa na chakula complete Bado hatujaongelea Tausi waliokuwa complete na Bajeti yake ilikuwa kubwa tu aliwapa na chakula sijui hela ya matunzo ya TAUSI Kama kuna mtu mnataka kumchafua narudia tena siyo Kikwete naomba tulete kumbukizi za wastaafu na TAUSI ILI TWENDE SAWA
 
I share a different opinion on this context without forgetting that I respect your constitutional right and freedom of expression, in my personal view and belief hii sio courtesy ni Sheria ilipitishwa walikuwa wanajua haya yote, kwa walio na nyumba na walioweza kujiwekeza ninsawa Ila Sheria inasaidia sababu ikija kutokea mwingine atakayejitoa kwenye utawala na akastaafu bila mali ni vema Sheria ikamback up.

Kama ilitokea kwa Nyerere basi inaweza kutokea kwa mwingine pia. Hatuwezi kuwaacha viongozi wetu waibe ili wajijengee nyumba zao.

Hatusemi hawa waliopewa hawajaona Ila hatuwezi kuacha gap kwamba kiongozi akiingia ikulu ndio ajue kwamba akitoka Hana haki ya mafao yani ajitafutie mafao yake mwenyewe, huo sio utaratibu wa nchi.

Kama ataiba aibe kwa utashi wake ili wananchi tubaki kumshangaa kwa sababu hana sababu ya kuiba since nyumba, magari, ulinzi tutampatia akistaafu.

Kuna hatari kubwa sana kama tutaruhusu kiongozi wa nchi asipewe mafao yanayostahili hadhi yake. Ataamua kujitafutia mwenyewe na hii itakuwa balaa maana itakuwa ndio utaratibu so hatutaweza kuhoji uadilifu wake sababu itakuwa kama mapato ya kanisani huwezi kumuhoji mchungaji maana atakujibu kwamba anafanya kazi kwa kujitolea.

Nchi lazima iwajali wastaafu kulingana na hadhi zao kwenye jamii, simply kiongozi ana nyumba binafsi haisababishi tusimpe stahiki zake.

Mbona watumishi wa kawaida tunalipwa hela ya Kodi kwenye mshahara pamoja nyumba tunazo? Mbona unalipwa usafiri na gari unayo? Mbona unalipwa lunch wakati mkeo anakufungia msosi toka home au unaishia kunywa chai ya ofisini wakati chai ipo nyumbani kwako?

I think tuwe progressive kidogo.
 
Gombeeni nanyinyi Urais mpate hizo privileges , hii kitu iko ndani ya Sheria kwamba Rais Mstaafu lazima apewe Nyumba awe nayo ama hana lazima apewe na Serikali ,yaani kwa maneneo mengine ni kwamba hata Trump na mahekalu yake yote angekua Bongo angepewa nyumba tena , kwahiyo inakua mitano tena, kinachotakiwa hapa ni Katiba mpya ndiomaana Jobo nduugway nayeye kashinikiza sheria za hovyo za kutokushtakiwa zipitishwe yooote ndio mambo hayahaya tu
 
Hii bqrua inaonesha ujinga wa Watanzania wengi.

Sheria zinatungwa bungeni, kwa nini usiwaandikie wabunge wabadilishe hiyo sheria?

Halafu mtu kashapewa hilo kasri kisheria, kwa nini unamshikia bango?

Kwa nini usibadili sheria hiyo iwe nzuri zaidi kwa marais wajao?

Walivyopitisha sheria ulikuwa wapi?

Marais wastaafu wote wanepewa hayo ma kasri, warudishe wote au unampenda Kikwete tu?

Halafu, ukiwa na marais ambao hawana uhakika na mafao yao kuwa mazuri, wakikuibia ili wajiandae na maishanya kustaafu, napo utalalamika?
 
Yaani kutopewa nyumba ndo kuiba?

Wakati Nyerere anastaafu hskujitungia sheria ya mafao ya kujengewa nyumba pindi akistaafu, tuambie Aliiba sh ngapi akiwa madarakani?

Mwinyi alikaa miaka 25 kabla ya kujengewa nyumba na kukabidhiwa hapa majuzi, ina maana alipokuwa rais aliiba ili ajijengee nyumba zake?, Mana wakati wake sheria ya mstaafu kujengewa nyumba haikuwepo
 
Rudia comment yangu, haukuwa na haja ya kuendelea kubishana nami, Soma mstarinwa kwanza wote. I share a different opinion na pia naheshimu sana Uhuru wako wa mawazo na kujieleza.

As gentlemen say, let's agree to disagree, haitakupunguzia kitu. Nilichoona una mawazo tofauti sana na yangu so amini unachoamini tu.
 
Kwani kule Msoga hakumtoshi kuishi? Kwa kweli kuhenyeka kote huku tunahenyeka ili wanasiasa waneemeke
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…