Mzee katoa hoja "Mzungu kaitoa Afrika Porini" akamwagiwa kahawa yake

Rorscharch

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2013
Posts
878
Reaction score
2,014
Kuna ukweli kwenye hili?
Anasema kuwa:

1. Anasema mpaka sasa mbona tukisema tunaenda kuangalia majengo ya kale tunachokiona ni kazi ya mwarabu na mzungu, sisi ngome zetu zenye ubora kama ya hao watu ziko wapi? (Wazee wengi ne walifoka sana hapa)

2. Alisema wenzetu walikuja huku wakiwa wameachana na vita za kikabila kitambo sana na kilichokuwa kikinukishwa ni vita za nchi na falme, mzungu kakanyaga Afrika kakuta makabila na mifano ya makabila yanayojiita mataifa , ni sawa sawa katika harakati za kujenga ustaarabu tulionao sasa mtu atolewe shule ya msingi arushiwe chuo

Ni kweli kwenye haya?
 
Kulikua na Himaya na mataifa makubwa tu ya Ki Africa, mengine Yalikua yameendelea kushinda hata baadhi ya Mataifa ya Ulaya.

Egpty, Ethiopia ya kale (Aksum), Mali Timbuktu, Zimbabwe Stone town, Kilwa etc.

Kwa picha
1. Zimbabwe Ruins za miji ya Zamani
images (61).jpeg

2. Timbuktu
Barth_1858_Timbuktu_from_terrace.jpg

3. Aksum Empire
images (62).jpeg

4. Kilwa
images (63).jpeg

Wazungu wanakuja Africa wanakuta Chuma kipo advanced kuliko kwao wakawa wanaki export kwenda India na mataifa mbalimbali kutengeneza Bunduki.

Kabla ya wazungu kuja Kulikua na Empire 4 kubwa Duniani ambazo zina Balance Power, Aksum, Roma, Persia na China, Aksum (Africa) ilikua na Nguvu kama Roma na Persia.

So hawa wanaofanya Revisionism kwamba Ukoloni ulisaidia Mataifa wengi ni mazombie wa media za west ambao kila wanachofanya west wao wanakimeza kama kilivyo na kukiabudu.
 
Yaliyojaa mjini tu siyamalizi sa yanini nijisumbue na Historia..

Naisomaga tu kama hadithi ila hainishuulishi kubishana kabisa eti babu alikuwa sokwe..! Mara binadamu wa kwanza duniani aliishi Tanzania 😅😅
 
Kulikua na Himaya na mataifa makubwa tu ya Ki Africa, mengine Yalikua yameendelea kushinda hata baadhi ya Mataifa ya Ulaya.

Egpty, Ethiopia ya kale (Aksum), Mali Timbuktu, Zimbabwe Stone town, Kilwa etc...
Umeandika uongo mtupu,

Hakuna Himaya ya Africa iliyowahi kukaribia hata nusu ya Roman Empire, Himaya ya Roma walikuwa na barabara bora kuliko sehemu kubwa ya Africa leo hii, walikuwa na mavazi bora ya kijeshi, walikuwa na maktaba bora na nyingi Kuliko sehemu kubwa ya Africa.

Kupitia aqueducts raia wa himaya ya Roma walikuwa wanapata maji mengi na safi kuliko raia wengi wa Africa leo hii.
 
Muongo mkubwa huyu, sio kuwa hata nusu, hata zilizowahi kua hata robo ya roman empire ni almost mbili tu, zingine zilikua 5% ikizidi sana 10%.
 
Kulikua na Himaya na mataifa makubwa tu ya Ki Africa, mengine Yalikua yameendelea kushinda hata baadhi ya Mataifa ya Ulaya.

Egpty, Ethiopia ya kale (Aksum), Mali Timbuktu, Zimbabwe Stone town, Kilwa etc.

Kwa picha
1. Zimbabwe Ruins za miji ya Zamani
View attachment 3174031

2. Timbuktu
View attachment 3174033

3. Aksum Empire
View attachment 3174036

4. Kilwa
View attachment 3174037

Wazungu wanakuja Africa wanakuta Chuma kipo advanced kuliko kwao wakawa wanaki export kwenda India na mataifa mbalimbali kutengeneza Bunduki.

Kabla ya wazungu kuja Kulikua na Empire 4 kubwa Duniani ambazo zina Balance Power, Aksum, Roma, Persia na China, Aksum (Africa) ilikua na Nguvu kama Roma na Persia.

So hawa wanaofanya Revisionism kwamba Ukoloni ulisaidia Mataifa wengi ni mazombie wa media za west ambao kila wanachofanya west wao wanakimeza kama kilivyo na kukiabudu.
Kwanini hayakudumu? Mbona Watu wa Asia walikutana na hizo Kash Kash za ukoloni ila asili yao bado ipo?
 
Kudumu vipi yaani, si picha hizo nimekuwekea? Kama Zimepigwa picha ina maana zimedumu hadi sasa?

Kwani asili ya Africa imebadilika? Kuna wa Africa wanaishi karne Kadhaa North America na bado wanapenda Ngoma, asili ipo vile vile it's just kuna watu wanataka usifuate Natural Evolution yako bali uwafuate wao wanacho taka.
 
Wazungu walikuja Africa na cannons na bunduki
1. Kipindi wazungu wa Mwanzo kina Vasco da Gama wanakuja Bunduki ilishagunduliwa ila sio widely Available ilikuwa bado ni Expensive na huwezi ku Afford jeshi zima, miaka ya 1400

2. Wareno walivyokuja Africa Walikuta Chuma kinachofuliwa ni high Quality kuliko vyuma vyao, solution ni ku Export Chuma cha Africa kwenye Viwanda vyao.

3. Issue ya Chuma cha Africa ni stori ndefu mno ila ni Fact at that time Watu Africa walikua juu kwenye Ufuaji chuma. Jiulize swali moja kwanini Wakoloni waliwakata Mikono Blacksmith wa KI Africa? Why blacksmith na sio field nyengine?
 
Umeandika uongo mtupu,
Hakuna Himaya ya Africa iliyowahi kukaribia hata nusu ya Roman Empire, Himaya ya Roma walikuwa na barabara bora kuliko sehemu kubwa ya Africa leo hii, walikuwa na mavazi bora ya kijeshi, walikuwa na maktaba bora na nyingi Kuliko sehemu kubwa ya Africa.

Kupitia aqueducts raia wa himaya ya Roma walikuwa wanapata maji mengi na safi kuliko raia wengi wa Africa leo hii.
Sijui kama unajua unachosema. Nenda Misri uone zile pyramid ambazo hata leo wazungu hawajui zilijengwa vipi. Ni watu wachache wasiojua historia au wanaojikana wanaoona kama Afrika ilikuwa haina kitu. Utakuta huyo mzee ni yale mazalia ya kiarabu. Yupo mmoja kariakoo niliwahi kumsikia akijivuna kuwa waarabu wameendelea kwa sababu wana kitabu yaani quran nikashangaa kwanini asirudi kwao uarabuni anakokanwa na kuitwa mtumwa.
 
Kulikua na Himaya na mataifa makubwa tu ya Ki Africa, mengine Yalikua yameendelea kushinda hata baadhi ya Mataifa ya Ulaya.

Egpty, Ethiopia ya kale (Aksum), Mali Timbuktu, Zimbabwe Stone town, Kilwa etc.

Kwa picha
1. Zimbabwe Ruins za miji ya Zamani
View attachment 3174031

2. Timbuktu
View attachment 3174033

3. Aksum Empire
View attachment 3174036

4. Kilwa
View attachment 3174037

Wazungu wanakuja Africa wanakuta Chuma kipo advanced kuliko kwao wakawa wanaki export kwenda India na mataifa mbalimbali kutengeneza Bunduki.

Kabla ya wazungu kuja Kulikua na Empire 4 kubwa Duniani ambazo zina Balance Power, Aksum, Roma, Persia na China, Aksum (Africa) ilikua na Nguvu kama Roma na Persia.

So hawa wanaofanya Revisionism kwamba Ukoloni ulisaidia Mataifa wengi ni mazombie wa media za west ambao kila wanachofanya west wao wanakimeza kama kilivyo na kukiabudu.
Kama walikuwa advanced ikawaje wakatawaliwa?
 
Waafrika tutaendelea kutawaliwa kwa kutopambana kwa ajili ya leo yetu ili kupata kesho bora. Tumekalia mambo ya historia na kuwa inferior mbele ya wazungu kisa rangi. Ningekuwa Rais somo la historia lingekuwa kama Civics yaani halina combination yoyote. Tunaishi kwenye zama zilizopita badala ya leo. Bara la Asia walikuwa duni ila wakaamua kupambana hadi tunaona nao wanaenda sambamba na wakoloni. Sisi leo hii tunapewa misaada ya vyandarua. Hata ku-afford teknolojia na vifaa vya kuchimba madini wenyewe hatuna hadi tusubiri wawekezaji. Ni mambo ya aibu.
 
Back
Top Bottom