Mzee wa Msoga haishiwi vimbenga, ni mtalaam wakung'ata na kupuliza . Leo inasambaa picha akiwa kavaa tshirt kama ya Yanga akiwa anatazama punda. Tshit ukiangalia kwa makini unabaini ina maneno yasomekayo "Kasi isambazayo tabasamu".
Maneno haya yana maana kubwa sana yanapokaa mgongoni mwake tofauti na yangekaa mgongoni mwa mwananchi wa kawaida.
Je, ni kweli tunayo kasi inayosambaza tabasamu au tumepingwa upofu kuyakumbuka na kuyaona machungu?
Haaa liko wazi hilo! Unashangaa makofi polisi? Mama ni mlezi, mama huleta tabasamu! viva Mama Samia, Viva Mama Mulamula, tunaanza kuiona Tanzania mpya, isiyo na vitisho, dhuluma na unyanyasaji, Tanzania ambayo ni sio kisiwa, bali sehemu ya dunia ya Mungu. Asante kina Mama, kazi iendelee!