Raisi Mstaafu JK kusema hayo, Sisi kama Wananchi wa kawaida, hatuwezi kukosa haya ya kujiuliza
Umiliki wa Uchumi Kwa wananchi, zaidi ya tawala nne zote, wamehangaikia kupata na wakafanikiwa $900, hapo ni zaidi ya miaka 50+
Mpango wa viongozi wetu hao ambapo pia ni Jambo jema, ni kuona kwamba, kufikia 2025 angalau kipato cha mwananchi kifikie $3000
Unajiuliza, Kwa nini miaka zaidi ya 50+, hawakuweza kufikia hata nusu ya mpango wao? Iweje wapange Hilo lifanyike Kwa miaka kumi pekee?
Ukiangalia nchi walivyoiacha, unaona kabisa kwamba mpango wao japo ni mzuri, Ila Bado ulikuwa na mapungufu
Nchi ilivyoachwa, Rushwa ilikuwa ni njenje, Ukusanyaji wa Kodi ulikuwa hovyo, mikataba mibovu, kwenye madini ndio usiseme, bandari nako hakuelezeki, ilikuwa kama wewe ni mtoto wa Fulani unapita bila kuulizwa, wizi wa nyara za serikali, vitalu watu kujimilikisha, gesi kupewa wageni na vitu vingi tu vilivyokuwa ni hovyo
Nchi Kwa mfano ilikuwa na nini cha Maana
Kwa jinsi hiyo, utawekaje sasa mpango wa miaka kumi kwamba uone kipato cha mwananchi kikifikia $3000 ili Hali hawa viongozi wetu hawakuifikia hata Ile robo yake tena zaidi ya miaka 50+?
Je, waliuona Uwezo wa anayekuja kwamba ni mzuri zaidi Kwa maswala ya Uchumi au ndani mwao kulikuwemo unabii?
Kivyovyote vile, Magufuli ni mzuri tena sio kidogo, mbali na Changamoto hizo zote, lakini tunayo macho tunaona
Naamini pia kwamba, kipato hicho ikiwa majanga ya kidunia yataondoka mapema, itakuwa
Mungu Ibariki Tanzania na Watanzania wote