Mh Rais Mstaafu Jakaya Kikwete naomba kukung'ata sikio ila pia naomba pia sio lazima chukua wazo langu mimi ni mdogo sana ila natamani kuona ccm na Taifa lina kuwa tulivu na ccm ina tawala hata kama miaka mia ila zingatia haya.
Wewe ni Rais mstaafu kama wastaafu wengine wa serikali epuka kuwa mbele kama mzee namba moja utaepuka mengi.
Amani ya Taifa hili ina hitaji busara na hekima na wewe kama Rais mstaafu unajuwa hili ktk milango ya Siri.
Mh Rais kwa hali ilivyo sasa na kile nakuona unakibebea bango mbele shimo litakuwa refu sana na uwenda likaleta maafa kwa Taifa na muktadha wa Taifa hili kwa miaka kadhaa mbele nakuomba baba yangu epuka kuwa reference heshimu mawazo ya wengi na hasa ya wakongwe wa Taifa hili ukikumbuka hakuna mtoto wala mjukuu wa Nyerere au Benjamin Mkapa kwenye siasa ila walikuwa na watoto. Kiapo cha sitopendelea mtu kwa dini,kabila au kwa dam kitakutesa once mambo yatakuwa mambo.
Kifo cha JPM bado kina watesa wa Tanzania? wengi busara itumike kuliko nguvu lolote mnaweza fanya ila yaweza geuka kuwa kiza kati kati ya vilindi vya bahari ya kina kirefu.
Mwisho wema wamelala ila wapo kudai haki zao ktk hali yakushitua embu tuwakumbuke kwa sala na maombi. Amen