Zanzibar 2020 Mzee Kikwete: Mnataka Rais wa namna ya Dkt. Mwinyi sio Rais mwenye makeke mengi, mbwembwe nyingi...

Zanzibar 2020 Mzee Kikwete: Mnataka Rais wa namna ya Dkt. Mwinyi sio Rais mwenye makeke mengi, mbwembwe nyingi...

Kikwete naye walewale tu wapiga hela hakuna jipya hapo. Watanzania wanadanganyika sana na hawa jamaa, no wonder hawaimprove elimu maana siku ujinga ukiwatoka wadanganyika itakua mwisho wao
 
"sina maana hiyo" (in JK voice) huku anachekaa ila akijua fika ujumbe umefika.

"Tumenunua ndege, mbona hao waliopita hawakuweza?

Statement kama hizi wanapozisikia sijui huwa wanajisikiaje maana hamna kitu kinachokera mtu kukuona boya wakati kuna mchango umetoa.
 
Eti "isitoshe ni mwana CCM ambaye imani yake haina chembe ya shaka" Hawa viongozi bwana! Ameshindwa kututhibitishia kama Mwinyi ni mzanzibari au si mzanzibari. Hilo ndilo la muhimu zaidi, wazanzibari wanataka kuongozwa na mzanzibari.
 
Kikwete huwa simuelewi. Aliwahi kusema " Ndege wakati wa baridi hunyonyoa manyoya yake ili kuwakinga kinda dhidi ya baridi. Lkn ndege huyo lazima awe makini kwani anaweza kujinyonyoa sana mwisho akashindwa kuruka kwenda kutafuta chakula. Akafa yeye na kinda wake".

Aliwahi pia kusema " Ukiwa unahitaji kufanya usafi na marekebisho kwenye nyumba, lazima uvitoe vitu vyote nje kwanza. Kisha utafanya usafi marekebisho na hata kupiga rangi mpya. Na nyumba itapendeza kweli kweli. Lkn utakuwa Juha kama hutakumbuka kuvirudisha vile vifaa ndani kwa wakati vitaharibika na mwisho utalazimika kuvinunua vingine kwa gharama kubwa. Sasa sijui huko ndiyo kubana matumizi au kuongeza gharama zaidi".

Nafikiri alimlenga mtu fulani ndiyo maana nasema huwa simuelewi.
Duuh! Kikwete vijembe vyenye hadhi ya majembe kabisa. Kwa vyovyote vile anamlenga mtu fulani.
 
Eti "isitoshe ni mwana CCM ambaye imani yake haina chembe ya shaka" Hiyo haitutoshi, tuhakikishie kama Mwinyi ni mzanzibari au si mzanzibari! Zanzibar inatakiwa iongozwe na mzanzibari. Mwinyi si mzanzibari, hakuna hata mzanzibari mmoja wa chama chochote au wasio na chama anaeweza kusema anamjua Mwinyi toka utotoni, hakuna anaekumbuka kuwa jirani wa mwinyi na hakuna kabisa hata mmoja aliekuwa rafiki yake utotoni mitaani zanzibar. Hakuna mzanzibari yeyote yule anaekumbuka kumuona Mwinyi, kabla ya kuwa mgombea urais, katika msikiti wowote ule zanzbar kwa ibada zozote zile iwe sala tano, maziko au khitma. Mwinyi mwenyewe akiachwa pale bandarini Malindi na akiambiwa atembee kwa miguu hadi ikulu basi atashindwa kwa vile haijui zanzibar. Mzanzibari yeyote yule ukimuacha Bandarini Malindi atafika Ikulu tu kwa sababu kila mzanzibari anajua kuwa ni mwendo ulio staright forward, lakini kwa mgeni ni vigumu! Mwinyi si mzanzibari.
 
Back
Top Bottom