Eti "isitoshe ni mwana CCM ambaye imani yake haina chembe ya shaka" Hiyo haitutoshi, tuhakikishie kama Mwinyi ni mzanzibari au si mzanzibari! Zanzibar inatakiwa iongozwe na mzanzibari. Mwinyi si mzanzibari, hakuna hata mzanzibari mmoja wa chama chochote au wasio na chama anaeweza kusema anamjua Mwinyi toka utotoni, hakuna anaekumbuka kuwa jirani wa mwinyi na hakuna kabisa hata mmoja aliekuwa rafiki yake utotoni mitaani zanzibar. Hakuna mzanzibari yeyote yule anaekumbuka kumuona Mwinyi, kabla ya kuwa mgombea urais, katika msikiti wowote ule zanzbar kwa ibada zozote zile iwe sala tano, maziko au khitma. Mwinyi mwenyewe akiachwa pale bandarini Malindi na akiambiwa atembee kwa miguu hadi ikulu basi atashindwa kwa vile haijui zanzibar. Mzanzibari yeyote yule ukimuacha Bandarini Malindi atafika Ikulu tu kwa sababu kila mzanzibari anajua kuwa ni mwendo ulio staright forward, lakini kwa mgeni ni vigumu! Mwinyi si mzanzibari.