Uchaguzi 2020 Mzee Kikwete: Ninakopanga sijafukuzwa

Hiyo lugha ya picha tu, maana yake nyumba yenu nimeipokea lakini sio kila kitu kwangu ndio maana nilikopangwa sijafukuzwa.
Kwa maana nyingine wapewe Wapangaji waliofukuzwa walikopanga!!
 
Chagua Lissu kwa katiba mpya inayomgusa kila mwananchi, tuachane na katiba ambayo inamuongezea aliye nacho tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Usithubutu kuchaguaLissu yeye atawajengea hadi akina robati Nyumba huko Ulaya kwa Kodi za Watanzania,Bora Magu anawajengea Watangulizi wake hapa hapa Tz!!
 
Jitambueni kwa faida ya Taifa letu. Tabia yenu ya kusifia kila kitu ndo inayowageuza viongozi kuwa miungu watu.

Yaani nyumba zote alizonazo Kikwete bado anajengewa nyumba? Huyo aliyepitisha hiyo sheria ya kinyonyaji ni mnyonyaji kama kupe. Hizo hela si bora zingejenga kituo cha afya?
 
Nimejiuliza sana sijui iyo sheria ilipitishwa vipi.umasikini hauwezi kuisha kwa nchi zetu za Kiafrica Sasa Mzee Kama Mwinyi unampa jumba lote lile la nini
 
Nimeangalia ID yako zaidi ya mara tano kuhakikisha kama ni ww kweli

Ila bado nina mashaka, I think simu yako itakuwa iko hacked [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Hahaha msidanganyike, Makonda alikuwa mkuu wa wilaya na Mkoa kwa miaka 4tu, kajenga maghorofa.

Kikwete kawa rais kwa miaka 10, waziri miaka 15, kanali wa jeshi, halafu akwambie kapanga nawe masikio yakusimame, hizo akili au matope?!
Kikwete hakua Mwizi,ni Mzalendo halisi!!
 
Wameua NHC ambayo ilikuwa na jukumu la kujenga makazi bora kwa ajili ya wananchi wa kawaida mijini kisa wao wanaweza kujijengea mahekalu, tena warejeshe nyumba za serikali maana maafisa wanapata shida za kuishi uswahilini.
 
Unashangaa JK amepanga wakati Jiwe amejijengea uwanja wa Ndege Chattle
 
Alikuwa anajoki,kikwete hajapanga popote,anakaa kwake msoga na akija dar anakaa mikocheni kwake
 
Nimejiuliza sana sijui iyo sheria ilipitishwa vipi.umasikini hauwezi kuisha kwa nchi zetu za Kiafrica Sasa Mzee Kama Mwinyi unampa jumba lote lile la nini
Sisi Wajuku zake Mwinyi tutajifunzia mpira humo,wala usiwe na wasiwasi!!
 
Nimejiuliza sana sijui iyo sheria ilipitishwa vipi.umasikini hauwezi kuisha kwa nchi zetu za Kiafrica Sasa Mzee Kama Mwinyi unampa jumba lote lile la nini
Magufuli bora hata angewajengea CDM kale ka office kao pale Ufipa, maana ka office kanatia huruma sana Kama kamekondeyana wakati Viongozi CDM wamenona!!
 
Waungwana muwe mnazielewa lugha za mafumbo zenye ujumbe wa kawaida tu.

Sio kila kitu ni cha kuamsha nongwa, mengine yatawaumiza mioyo pasipo umuhimu wowote.

Ujumbe wa Kikwete ni kusema kwamba hana haraka sana kwani anapo mahali pa kuishi.

Wakwere ni watu wa Pwani wenye ufundi mkubwa wa kiswahili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…