Mstaafu Jakaya Kikwete ameingilia kati mjadala wa kupanda kwa gharama za maisha kunakolalamikiwa na wananchi wengi na hii ni moja ya nukuu yake kupitia clip moja hivi inayosambaa sana kwenye mitandao.
'Bei imepanda sasa mtu ndio wanatunga na nyimbo, mafuta yamepanda bei ni unafiki mkubwa kwa kweli
'..eeeh unajua wakati mwingine offcourse ndio unasema adui yako muombee njaa wale wasiombea heri Serikali wanadhani lakini wakati mwingine ni lazima wawe wakweli tu haya mazingira wangekuwa wao ndio wako kwenye uongozi wana majawabu gani ndio bei ya mafuta ingeshuka?
Bei ya mafuta imepanda Uingereza penyewe'