Mzee Kinana, trafiki wengi wako barabarani kwa vile kuna pesa zisizo na jasho. Nini kifanyike?

Mzee Kinana, trafiki wengi wako barabarani kwa vile kuna pesa zisizo na jasho. Nini kifanyike?

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Posts
44,629
Reaction score
83,056
Logic ya trafiki wengi barabarani iko hivi: (something like a syllogism)

1. Kuwa barabarani ni pesa
2. Kitengo cha Trafiki ni wengi sana (kila mmoja mwenye upenyo amampeleka mwanae/nduguye utrafiki
3. Automatically ili kila mmoja lazima apate pesa,
4. Lazima kuwe na vituo vingi vya kusimamisha magari ili kila mmoja apate pesa.
--------------------------------------------------------------------------------------
5. Aggravated more by: mabosi wanataka pesa, na si ndogo,. Unazipataje? lazima uwapange wengi barabarani and hence vituo vingi.

SULUHISHO:
1. Futa police kuwa barabarani! Inawezekana? Sidhani maana waafrika tumelogwa! Barabarani kutakuwa chaotic!
2. REFORM POLICE FORCE . How? This is debatable maana Mh!
 
Logic ya trafiki wengi barabarani iko hivi: (something like a syllogism)

1. Kuwa barabarani ni pesa
2. Kitengo cha Trafiki ni wengi sana (kila mmoja mwenye upenyo amampeleka mwanae/nduguye utrafiki
3. Automatically ili kila mmoja lazima apate pesa,
4. Lazima kuwe na vituo vingi vya kusimamisha magari ili kila mmoja apate pesa.
--------------------------------------------------------------------------------------
5. Aggravated more by: mabosi wanataka pesa, na si ndogo,. Unazipataje? lazima uwapange wengi barabarani and hence vituo vingi.

SULUHISHO:
1. Futa police kuwa barabarani! Inawezekana? Sidhani maana waafrika tumelogwa! Barabarani kutakuwa chaotic!
2. REFORM POLICE FORCE . How? This is debatable maana Mh!
Wamrudishe uwaziri mambo ya ndani Kangi Lugola awanyooshe Traffic Police
 
Yuko sahihi

Naona baada ya Kinana kuongea kuna mabadiliko kidogo vituo vingi ambavyo traffic hurundikana karibu karibu leo sijawaona .Usalama wa taifa wajitose kazini. wachukue daladala waendeshe au wawe makondakta washirikiane na wamiliki wa magari hilo zoezi wa mabasi, Malori na magari madogo ziwe taxi au binafsi kufanikisha zoezi.Traffic ni eneo sugu

Tunashukuru Raisi alipofanya mabadiliko.ya IGP alisema kutakuwa na mabadiliko makubwa hadi majeshi.Ushauri wa bure aanzie Traffic kwenye hayo mabadiliko

Traffic wengi kuliko mahitaji hasa.kwenye majiji na miji unajiuliza rundo lote la traffic kila hatua chache nini hicho kama sio overemployment?
Uchumi kwenda haraka ni pamoja na magari kwenda haraka ya mizigo na abiria

Waziri wa Uchukuzi na Raisi walisema Flyover kama Tazara zina lengo la kuongeza kasi ya magari kutembea wakaonya kuwa na Traffic wapunguze kupiga mkono kusimamisha magari hapa na hapa .Hawakusikia

Kinana pia kaongea kama wasiposikia Mama Samia kula vichwa tumbua na hamisha wakubwa wapeleke hata kuwa maofisa wa tarafa mawilayani huko porini watoa kabisa Jeshi la polisi

Hi kitu ni Kero. Traffic Kero tena kubwa hasa mijini na kwenye majiji na njia zenye magari mengi
 
Askari wa usalama barabarani wapo nchi zote duniani na kazi yao ni kupunguza misongamano barabarani,kusimamia sheria za usalama barabarani, kuzuia uhalifu unaotokana na vyombo vya usafirishaji, kuzuia ajali za barabarani kwa kutoa elimu na kudhibiti mwendo kasi pia kuweza kutoa msaada pindi ajali zinapotokea kwa kuhakikisha majeruhi wanafikishwa hospitali kwa wakati,kukusanya ushahidi kutokana na chanzo cha ajali na kuwafikisha mahakamani walio sababisha ajali.

Kuhusu uwepo wa askari wa usalama barabarani sheria imeshatoa uhalali wala si kwa matakwa ya mtu ikiwemo Road trafic Act,sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai,sheria ya polisi na wasaidizi wake na nyinginezo.

Jambo la msingi waendesha vyombo vya moto waone kufuata na kutii sheria za usalama barabarani ni moja ya majikumu yao sio kukimbilia kutoa vijipesa halafu wanaenda kuongelea pembeni hasa kwa wanasiasa hiyo sio njia sahihi fuata sheria na ukijiona umekiuka kubali kuwajibishwa.
 
Cha kufanya mtu mzima Kinana kaongea
Mambo ya Traffic kibao kuwa kila hatua chache yaondoke

Pili Daladala kufanywa miradi ya traffic kupata pesa kuondoke

Yaani Traffic wanafanya daladala mradi wao madereva wote waulizwe hii Kero watatapika nyongo

Yaani kumiliki daladala ni kutangaza gari yako kuwa mradi wa Traffic.Madreva wanayoya kuongea kwenye hili.Daladala hata trip moja ndio anaanza hajawafikisha hata abiria kituo wanachoshuka Traffic anataka hela wakati abiria hata nauli hawajampa

Traffic wabaki kuongoza magari tu kwenye maeneo ambayo hayana mataa sababu hayo mengine sio sawa mara analaghai tairi no wakati kila mwaka kuna zoezi la usalama barabarani la magari yote kukaguliwa na kupewa sticker
 
Yuko sahihi

Naona baada ya Kinana kuongea kuna mabadiliko kidogo vituo vingi ambavyo traffic hurundikana karibu karibu leo sijawaona .Usalama wa taifa wajitose kazini
... hii iendane na maboresho ya alama za barabara - la TANROADS hilo. Wakati mwingine kuna alama zinawekwa sehemu fulani hadi unashangaa! Sehemu imenyooka mnawekewa NO OVERTAKING; ikiisha tu 50 inafuata ilimradi tu magari yasiwe na mwendo na maeneo hayo ndio "PEPO" za TRAFIKI; wanayapenda balaa!

Ningetamani atokee mtafiti au reputable firm ifanye utafiti wa barabara za Tanzania hususan barabara kuu tupate picha ni km ngapi za barabara speed ni under 50 na ni muda kiasi gani unapotea kwa mwaka kwa makatazo hayo hence kiasi cha pesa kinachopotea na nini kifanyike ili kuokoa hasara. Si ajabu more than 70% ya umbali wa barabara za nchi hii ni makatazo (under 50; NO OVERTAKING).

Halafu sijui hata kama mamlaka husika zinajua hili; kadiri miaka inavyozidi kwenda, miji inazidi kuongezeka pembezoni mwa barabara kuu such that itafika mahali kwa akili za TANROADS 95% ya umbali wa barabara itakuwa makatazo. Fikiria unaendesha gari toka Dar hadi Mwanza kwa mfano speed limit 50kph! Serikali ianze kutafuta suluhisho la tatizo hili ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu ya barabara kuondoa kero hii.
 
Askari wa usalama barabarani wapo nchi zote duniani na kazi yao ni kupunguza misongamano barabarani,kusimamia sheria za usalama barabarani...
Sheria gani hizo zinazotamka kila hatua chache wawepo traffic? Na kila daladala la iazima kwenye hiyo route wawe wanatoa hela kwa Traffic?

Kinana katamka wazi kuwa Tanzania ndio nchi pekee ambayo ni kama Traffic police state kila hatua chache traffic kibao kuanzia stendi hadi barabarani

Mwendo mdogo tu unakumbana na Traffic
 
Utaratibu wa kuwaweka mapolisi barabarani umepitwa na wakati kabisa na umebaki kuwa ni mradi wa wakubwa ndani ya kikosi hicho.

Nchi iwekwe makamera tu kwisha habari na hawa maaskari wa barabarani warudi vituoni wapangiwe kazi zingine.

Ni ushamba sana kuweka mapolisi barabarani, kwanza hakuna kazi yoyote ya maana wanayofanya na ajali ndio sasa zinaongezeka huku wenyewe wakikusanya rushwa. Bure kabisa.
 
Nadhani utaratibu mzuri ni kukagua gari mara moja,na trafiki kukabidhi dereva uthibitisho wa maandishi gari imekaguliwa -validity period 24hrs?,48hrs? -whatever. Sioni logic ya gari hiyo hiyo kukaguliwa mara mia siku ile ile. Trafiki lazima kudhibitiwa.
 
Nadhani utaratibu mzuri ni kukagua gari mara moja,na trafiki kukabidhi dereva uthibitisho wa maandishi gari imekaguliwa -validity period 24hrs?,48hrs? -whatever. Sioni logic ya gari hiyo hiyo kukaguliwa mara mia siku ile ile. Trafiki lazima kudhibitiwa.
Kuna wiki ya nenda kwa usalama unakaguliwa na sticker unapewa lakini bado unasumbuliwa kukaguliwa.Sticker zile kazi yake huwa nini?
 
Logic ya trafiki wengi barabarani iko hivi: (something like a syllogism)

1. Kuwa barabarani ni pesa
2. Kitengo cha Trafiki ni wengi sana (kila mmoja mwenye upenyo amampeleka mwanae/nduguye utrafiki...
System yote imeoza, takukuru imeshindwa kuwanasa trafiki wakati rushwa wanapokea hadharani, kila mtu anakula kwa urefu wa kamba yake kama alivyoshauri mkuu wa nchi
 
... hii iendane na maboresho ya alama za barabara - la TANROADS hilo. Wakati mwingine kuna alama zinawekwa sehemu fulani hadi unashangaa! Sehemu imenyooka mnawekewa NO OVERTAKING...
Ndomana magari ya serikali Viongozi wanawapelekesha madereva wao kutembea mwendo wa pesa mfano barabara ya Mbeya ukifika Igawa, Igurusi nk unatembea zaidi ya km kumi 50kmph eti eneo la mskazi ya watu.
 
Traffic wa Dar hadi kuna upatu wanacheza Kupeana hela laki moja kila siku chukulia wako 40 kila siku mtu anataka na milioni nne kila siku mwenye zanu yake hiyo ni nje ya Rushwa anayokusanya over and above hiyo laki moja ya upatu.Walipiaji huo ujinga madereva na wamiliki wa magari kwa Rushwa wanazoombwa na hao Traffic

Hili swala na Takukuru wahusishwe ni.mbinu gani ifanyike kukomesha for good Rushwa za traffic. Kunatakiwa kuangalia mifumo ya kazi na hiyo sio kazi ya polisi pekee.

Utumishi wahudishwe Takukuru wahusishwe, vitengo vya Tehama vihusishwe Usalama wa taifa wahusishwe, Tanroads, wizara ya Uchukuzi ihusishwe na wamiliki wa magari ya biashara na binafsi wahusishwe na uombwe msaada wa wawakilishi toka nchi ambazo zina uzoefu wa kudhibiti Tatizo la Rushwa kwa traffic police

Waongozwe na kamati ile aliyounda Raisi kuabgalia utendaji wa majeshi. Polisi Traffic kwenye hiyo kamati wasiwemo.
 
System yote imeoza, takukuru imeshindwa kuwanasa trafiki wakati rushwa wanapokea hadharani, kila mtu anakula kwa urefu wa kamba yake kama alivyoshauri mkuu wa nchi
Kuwanasa mmoja mmoja haisaidii sana tunatakiwa kuja na solution ya utendaji kazi ambayo traffic police hatafanikiwa kupata hata mia ya Rushwa hata wakitaka

Hili eneo wataalamu ikulu na utumishi na viongozi wa juu wa polisi wanatakiwa vichwa vichemke. Watafute solution haraka kabla Raisi kula vichwa vyao na kutumbua.

Kinana Mtu mkubwa kijeshi, kichama na kiraia akiongea ni command. Mtu akidharau shauri yake
 
Askari wa usalama barabarani wapo nchi zote duniani na kazi yao ni kupunguza misongamano barabarani,kusimamia sheria za usalama barabarani,kuzuia uhalifu unaotokana na vyombo vya usafirishaji,kuzuia ajali za barabarani kwa kutoa elimu na kudhibiti mwendo kasi pia kuweza kutoa msaada pindi ajali zinapotokea kwa kuhakikisha majeruhi wanafikishwa hospitali kwa wakati,kukusanya ushahidi kutokana na chanzo cha ajali na kuwafikisha mahakamani walio sababisha ajali.Kuhusu uwepo wa askari wa usalama barabarani sheria imeshatoa uhalali wala si kwa matakwa ya mtu ikiwemo Road trafic Act,sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai,sheria ya polisi na wasaidizi wake na nyinginezo.Jambo la msingi waendesha vyombo vya moto waone kufuata na kutii sheria za usalama barabarani ni moja ya majikumu yao sio kukimbilia kutoa vijipesa halafu wanaenda kuongelea pembeni hasa kwa wanasiasa hiyo sio njia sahihi fuata sheria na ukijiona umekiuka kubali kuwajibishwa.
Imekula kwako mkuu
 
Trafiki wa mjini ni kazi inayolipa sana na wao wanagombania sehemu zenye pesa zaidi hawataki kuhamishwa kabisa. Unakuta askari traffic kwa siku anatoka na laki nne hadi tano wengine hata kwenda likizo hawaendi maana wataachia 'gepu' kulingana na misemo yao.

Solution sio kuwakamata mana hata hao wakamataji wanakula rushwa. Watolewe barabarani zifungwe kamera kwanza hii utapunguza hata uongo wa askari kuchora michoro ya kimchongo ili mtu alipwe.

Makampuni ya bima na wadau wanaoibiwa kwa michongo ya askari wawekeze hapa kupunguza madai ya michongo hata serikali wanaweza kufunga camera barabara zote mijini kukawa hakuna haja ya trafiki camera zinarekodi kila kitu.

Mimi niko radhi hata kama wataanzisha tozo kidogo kwa ajili ya kufunga hizo camera ili kuondoa usumbufu wa hawa jamaa zetu.
 
Askari wa usalama barabarani wapo nchi zote duniani na kazi yao ni kupunguza misongamano barabarani,kusimamia sheria za usalama barabarani...
Kwani kinana anataka waondolewe ama? Sijakuelewa mkuu maana umeelezea umhimu wao tuuuuuu bila kujali utitiri wao 😁😁
 
Back
Top Bottom