Mzee Kinana Umetukataza Kukagua Taa za Magari Mchana, Sawa Tumekuelewa

Tena ilitakiwa upelekwe police mess, ukatandike vitanda na kuwahudumia maafande chakula na vinywaji,
 
Mimi trafiki naowajua hawakagui chochote ni kukusanya hela barabarani, Kama huna ndio wanaanza kukagua, huu mfumo unafanya kila dreva LAZIMA awe mtoa rushwa, Hadi watu wanafikiri ni mradi wa serikali, huu mfumo uangaliwe upya.

Yaani kutoka wilaya moja Hadi nyingine uwe na angalau elfu ishirini ya kusafisha barabara hata Kama gari ni jipya. Tusitetee upumbavu
 
Pole sana, unaandika kwa hisia hadi sauti inasikika.

Wako askari waadilifu na wasio waadilofu.

Wasio waadilifu kwenye sekta ya usalama barabarani ndo wamebeba hulka kuwa askari wote wa barabarani ni wasumbufu, wala rushwa etc.
Shukrani sana mkuu
 
Umekaririshwa tu ndugu yangu
 
Nasema Uongo Ndugu Zangu kipindi cha Dkt Magufuli mlifanya kazi vizuri, yaani mlisimamia sheria na mkimkamata mtu kafanya kosa ndiyo mlichukua rushwa ila kwa kosa halisi. Ila kwa sasa mlikuwa mnashindana kuchukua hela hata kama gari halina kosa mnatafuta makosa hasa kwa daladala au basi
 
Kwa teknolojia tuliyo nayo sasa hapa nchini ni lazima tufanye hivyo ila siku tukiwa na uwezo wa kufunga camera za kufuatilia mienendo ya vyombo wala huta sumbuka.
 
Trafiki wa tanzania mchango wao mdogo sana kwenye kuzuia ajali..mana hata walipokuwepo ajali zilikuwa zikitokea..wengi ni wazuri na wataalamu wa kupokea rushwa.

Kitengo hichi kifumuliwe na kiendane na modern world...na sio kujaza trafic barabarani.

#MaendeleoHayanaChama
 
Mudawote mrembo nimemiss sana ile kitu ulinipea... nilikuja Lumumba nikaambiwa haupo tena na simu sikupati. Naomba nitafutie namna tena, Thanks.
 
Mimi sijawahi kubadilika, nimejifunza kuwa mwadilifu na natambua thamani ya uadilifu, siwezi kusemea wengine ila raia mnatufanyia vibaya mpaka hatufurahii kazi yetu.
 
Walikuwa wanatunyanganya hela hawa trafic.
 
Mi naonaga trekta zikitembea usiku na zingine mijini utadhani ni magari. Trekta ni mitambo ya kazi mashambani. Serikali itoe elimu na ikataze hii midude kutembea mwisho saa 12 jioni.
 
Pole sana mkuu , mimi binafsi nawapenda sana Trafick wanafanya kazi ngumu wanaochukia ni wale magari yao mabovu , wabongo wengi wanashabikia vitu .
 
Hamjakatazwa kukagua magari Ila mlikuwa Wengi mpaka mnachelewesha safari .Unatoka Bunju kwenda Mbagala hapo hapo Bunju unakaguliwa ,boko Tena Tegeta Tena Mbezi Tena ,Mwenge Tena, Mawasiliano Tena,Buguruni Tena,Uhasibu Tena kwa Aziz Ally Tena ,Mission tena na Zakhem Tena. Yaani 40km unakaguliwa Mara 10
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…