Mzee Kinana Umetukataza Kukagua Taa za Magari Mchana, Sawa Tumekuelewa

Mzee Kinana Umetukataza Kukagua Taa za Magari Mchana, Sawa Tumekuelewa

Nchi hii siyo traffic tu
Kila mtu anakula sehemu yake
Kuna wazee wa OSHA,kuna TBS,TRA,kuna jamaa wa misitu TFS
Kuna TFDA,
Mfano ukikutana na osha wakivamia
Hko viwandani rushwa zao kuanzia laki tano hadi mamilion...sema ttz hao hamuwaoni....
Traffic anaonekana kwa sababu kila siku yuko Road

Ova
Kweli
 
Japo ni kweli mnlikuwa na changamoto zenu na pia kupenda sana ela ila kwenye sula la usalama barabarani bado kuna shida kubwa saana yaani tanzania bora tu ujue kuendesha gari hayo mengine kila mtu anatumia utashi na akili zake, jifunzeni kutoka hata rwanda mbona hana ajali za kipuuzi kama tanzania
Tanzania Kila Mtu ni dereva. Halafu anatokea Mtu kiujumlajumla anawatetea wote hata hao wanaoendesha matrekta usiku bila taa. Na ukiangalia eneo ilipotokea ajali Hakuna traffic, yaani ni Uhuru wa Manyani.
 
mleta uzi anaonekana kabisaa ni mwela amechukia balaa kuambiwa wanabugudhi wananchi kwa kusimamisha simamisha ovyo magari, pole sana kwake mkalime kama mmekereka nyambaf, kwani pamoja na utitiri wooote wa hao trafiki barabarani mbona maajali ndio kwaaanza yanazidi. Badilikeni kima nyie mtu Bongo kuwa na Gari inakuwa kama Adhabu nchi gani hiyo, tena mnatakiwa woote mkalinde benki mtulindie hela zetu shubaaaaaaaaaaaaaaaamittt zenu.
 
Hamjakatazwa kukagua magari Ila mlikuwa Wengi mpaka mnachelewesha safari .Unatoka Bunju kwenda Mbagala hapo hapo Bunju unakaguliwa ,boko Tena Tegeta Tena Mbezi Tena ,Mwenge Tena, Mawasiliano Tena,Buguruni Tena,Uhasibu Tena kwa Aziz Ally Tena ,Mission tena na Zakhem Tena. Yaani 40km unakaguliwa Mara 10
Kwa maana nyingine ni kwamba, kila baada ya km 4, unasimamishwa na trafiki kwa ajili ya ukaguzi wa gari!
Hatari sana.
 
Hiyo barabara Kahama-Isaka hajaondolewa traffic hata mmoja,wapo vilevile tu hukaa sehemu tatu ila saa 10 jioni wote hawapo barabarani.
 
Kuna mwenzenu mmoja wa pale kinyerezi kwenye zebra na matuta ,hlf Kuna mmoja wa TAA za pale Kipawa ,na mwingine 2018 pale tazara na mwingine kwenye daraja la treni pale Ruvu 2017- nyie mkiingia anga zangu nawagonga na gari mkufilie mbali
 
Pole sana, unaandika kwa hisia hadi sauti inasikika.

Wako askari waadilifu na wasio waadilofu.

Wasio waadilifu kwenye sekta ya usalama barabarani ndo wamebeba hulka kuwa askari wote wa barabarani ni wasumbufu, wala rushwa etc.
Kuna stori yako moja.....Kuna police alikuweka ndani baada ya gari lako kupata majanga
 
Kuna stori yako moja.....Kuna police alikuweka ndani baada ya gari lako kupata majanga

Una kumbukumbu, usifukue kaburi tafadhali sitaki kukumbuka kile kisa.

Alikuwa mtu wa sekta nyeti, nilimchezea rafu barabarani akatoa oda kwa askari wa barabarani niwekwe ndani....!
Nilikuwa nimetoka sokoni vitu vyangu viliharibika akaleta misosi nikagoma kula, siku natoka akanilipa iharibifu wa vitu....!

Nilikasirikaaa...!
 
Baada ya agizo lako, tumeitwa na tupo kwenye utekelezaji. Nadhani ajali ya Usiku wa kuamkia leo imesababishwa na Taa.

Tunashukuru, wengine tumebadilishiwa mpaka idara ila sawa tu. Kila la kheri ndugu Kinana endelea kufurahia ku-drive maana hatuta kusumbua.
Sasa hiyo ajali ndio unataka kuitumia kama ngao ?
 
Na askali wakamuuliza (Yohana mbatizaji) sisi nasi tufanye Nini tupate uzima? Akawajibu, " mtoshewe na mishara yenu"

My take: kumbe Askari wana njaa Kali toka enzi za Yesu
 
Back
Top Bottom