Ya kwamba Kikwete miaka 10 ya uongozi wake hakuna chochote kizuri alicho ifanyia Tz?
Bila Kikwete kuanzisha mradi wa umeme vijijini wa REA bibi yako huko kijijini angekuwa anajua hata balbu ya umeme inafananaje?
Bila kikwete kuanzisha sera ya elimu kwa wote kwa kuanzisha shule za kata ww mtoto wa mlala hoi ungejua hata radha ya elimu inafananaje?
Hapa Tz kuna kiongozi aliye jenga km nyinyi za barabara kumzidi kikwete?
Huo umeme mlio kuwa mnamsifu kuwa haukatiki asilimia 65 ya vyanzo vyake si vilijengwa na huyo kikwete?
Kipindi cha kikwete ndo wakati ambao watz wengi masikini walijikwamua kwenye umasikini.
Hayo ni machache tu yapo mengi.
Mradi pekee wa maana ulio anzishwa na Magufuri ulikuwa ni hili bwawa la Nyerere tu mingine yote ilikuwa ni miradi ya hovyo na isiyo kuwa na manufaa yeyote kwa raia wa kawaida wa Tz zaidi ya manufaa ya kisiasa.
Yaani badala uchukue fedha uongeze mzunguko wa fedha mitaani ili urahisishe maisha ya masikini mitaani ,dabala yake una somba pesa kwa hao masikini na kwenda kununua ndege na kwenda Dodoma kujenga ikulu na majengo ya matrion ya fedha, alafu unajiita rais wa wanyonge.