Usipotoshe umma, Salman Rushdie ni muislam halisi, Rushdie ni utamkaji wa kizungu, jina lake ni Salman Rashidi.
Kabla hujaandika kitu jaribu kufanya japo kautafiti kadogo. Rushdie alipoamua kuukosoa uislam alikuwa akiandika mambo anayoyafahamu kwani amekuzwa katika dini hiyo.
Yusuf Makamba sio mtoto mdogo, mtoto wake January amezaliwa mwaka 1974. Anayo haki ya kutolea mifano vitabu vyote vya dini kama anao uelewa wa kile kinachoandikwa. Mbona waislam wengi tu wanaanzisha mihadhara maalum ya kuichambua Biblia?. Mbona wakristo wengi wanaisoma Quran tena wakiwa seminary wakati wakiwa kwenye harakati ya kuwa mapadre?. Huna sababu ya kuchukizwa na tabia ya Mzee Makamba kuchambua vitabu vyote vya dini, hakuna binadamu mwenye haki maliki ya vitabu hivi vitakatifu.