Elections 2015 Mzee Mkapa: Wanaosema Wanataka Kuikomboa Tanzania ni Wapumbavu na Malofa

Elections 2015 Mzee Mkapa: Wanaosema Wanataka Kuikomboa Tanzania ni Wapumbavu na Malofa

Jamani sisi “wapumbavu/fu malofa” tuwaulize Mkapa na CCM yao watupe majibu yafuatayo ili ikiwezekana tubainishe mpumbavu na lofa ni nani:-

Maana na uhalisia wa mpumbavu/fu ni asiyefundishika, asiye na busara

1. Mwalimu J. K. Nyerere aliondokea uwanja wa ndege akitembea kwa miguu yake bila msaada wa mkongojo kwa ajili ya kupima afya yake uingereza(kwa busara za Mkapa). Karudi kwenye sanduku tukamzika.
2. Wiki mbili baada ya mazishi ya Mwl NBC ikabinafsishwa
3. Ubinafishaji ukakumba mashirika ya umma vikiwepo viwandanzadi ya 400. Ubinafishaji ulihusisha mali zisizohamishika kama ndiyo hatua ya kwanza. Nyumba za shirika la posta tuwaulize familia ya Mkapa na akina Lukuwi kujiuzia hapo kuna busara.
4. Nyumba za serikali zikauzwa na serikali ya Mkapa chini ya usimamizi yaw a Magufuli. Naomba msomaji jiridhishe mwenyewe kuwa vile viwawanja vya nyumba zile hivi sasa wako kina nani pamoja na sheria kutaka visibadilishwe matumizi mpaka baada ya miaka 25. Watumishi wa serikali wakiwepo mawaziri wanapanga mahotelini kwa zaidi ya gharama za kukarabati hizo nyumba hata kujenga nyumba mpya kwenye viwanja hivyo. Hayo tunaambiwa ni maamuzi ya busara.

Maana ya neon lofa ni mtu zaidi ya masikini ambaye hata ukimpa mtaji mkubwa wa namna yo yote hataweza kuufanyia cho chote. Kifupi ni masikini wa mali na akili. Nawakumbusha huyu huyu Mkapa alipoanzisha msamiati wa wivu wa kike. Alikuwa na wazee wenzie na mawaziri wake wanakandia watu kupigia kelele wizi na ufisadi unaowatajirisha Mkapa na wale wateule wa CCM kuwa watu hawana akiuli na uwezo wa kutajirika wanabakia na wivu wa kike. Kumbe sababu ni kukosa mitaji na maarifa ndiyo inayo sababisha wao wateule wameatamia fursa zote za ujasiliamali. Huo nao ni ulofa wa kufikiri kama vile kuishi kwenye nyumba ya vioo katikati ya Uswazi.
Kifupi kuna yafuatayo

Awamu ya pili walihakikisha wanaua kabisa mfumo wa utendaji wa serikali na kuifanya serikali kuwa tawi la CCM. Hupewi uongozi wa namna yo yote kwa sifa za kitaalamu bali sifa ya CCM. Mtakumbuka siasa ilpoanza kuwa dili kupita uprofesa.

Awamu ya tatu ilikuja na mageuzi ya kiuchumi Mkapa na CCM watumia mageuzi ya uchumi kitaifa kuwa yao binafsi. Huo ndio ubinafsishaji.

Awamu ya nne ilikuja kwa kauli za kitaarabu elimu na huduma za kijamii ikaporomka uchumi wa mtu binafsi ndani ya wateule ukapaa uchumi wa mapumbavu/fu na malofa ukawa afadhali ya jana siku zilivyosaonga. Mikataba ya siri, kuuawa tembo na wanamageuzi hasa waandishi.

Bahati upinzani ukawa unajikongoja ukakurupusha hadidu za rejea za katiba na utendaji wa serikali. Wateule wakatunisha misuli hakuna cha katiba mpya wala utekelezaji wa maazimio ya bunge. Hizo nazo ni busara.

CCM wamekwenda kwenye kura za watia nia kumpata Magufuli mtendaji mzuri anatekeleza maamuzi ya wateule (Usisau uuzwaji wa nyumba ndio utendaji mzuri wa Magufuli lakini alitumia akili au akili yake alishikiliwa na wateule).
Wanaingia kwenye uchaguzi huu kwa ahadi siyo kwa sera kwa maana halisi ya sera, na sera ya kutukana wasiokubaliana nao.

Mahitaji ya baadhi yetu watanzania.

1. Ni uongozi unaoweza kutoa maamuzi na kuyasimamia. Si utendaji unaotekeleza maamuzi yenye ukakasi.
2. Maono ya miaka 50 ya Tanzania inayowakumbatia wananchi wake wakinufaika sawa na reasilimali na fursa za uchumi na kijamii.
3. Watanzania wenye kujitambua kwa kuwa na elimu ya kuchabua mambo na majasiri wa kuhoji uongozi mbovu. Hii ni pamoja na kuilewa katiba ya nchi ambayo inakidhi na kutokana na maoni yao.

Kwa kuitwa wapumbavu na malofa tumetngwa na kubaguliwa maana ni jumla jumla. Kwa hali hiyo wateule wamejitenga nasi hatuna namna yo yote ya kujinasibu nao. TUMIA KURA YAKO KWA BUSARA UACHANE NA UPUMBAFU NA ULOFA
Kuna wanao/waliofaidika na mfuma huuu huu unaoupigia chapuo uondoke na kunaowaliotupwa nje ya mfumo huu huu. Bila ya kujali wewe upo upande ganitujifunze kufaidika na mfumo wowote uliopo kwani hakuna serikali yeyote itakayokufuata ulipo na kukupa kazi au mshahara bila ya kufanya kazi,ke, maana tokea tukiwa shule ya msing wengi wa aliokuwa wanajibidiisha walifanikiwa wengine wote waliobakia walisubiri bahati ambayo mara nyingi huwaangukia wachache tena wateule. Cha msingi tuchape kazi na tuache kulaumu kula jamba kwa mihemko ya kisiasa.
 
Salaam.

Kampeni za uchaguzi zimefunguliwa na sasa Kumekucha Tanzania!

Nipende kuwapongeza wanaCCM kwa kufungua rasmi kampeni yao hapo jana (23.08.2015) lakini kwa namna mpya ya kejeli, vijembe, matusi(vilivyokataliwa na tume) kutawala ufunguzi huo. Nilishtushwa na kauli za viongozi wa CCM kama vile Mh. Benjamin W. Mkapa kutukana hadharani. Mengi yamesemwa ikiwa ni pamoja na kusema "upumbavu na ulofa" si tusi. Nabaki najiuliza hata kama si tusi hakuna maneno makali ya kutumia tofauti na hayo, hasa kwa Rais mstaafu? Nakumbuka Mh. Tundu Lissu aliwahi kutamka maneno hayo Bungeni(haikuwa hekima), kwa kuwa alikosea basi ndiyo inahalalisha matumizi yake? leo inaonekana kama mtindo!

Wazungu wanasema 'Great minds discuss ideas, average minds discuss events and small minds discuss people" Nilitegemea kwa kikosi kile pengine kutoa maneno ya busara na kutofanya kuwa kijiwe cha chuki kwa waliokatwa.(wakiwakejeli wakiokatwa, na baadhi ya waliokatwa walio ndani ya CCM kumalizia hasira zao pale kwa kuwa walikatwa)!

Wengi wa viongozi hawa hawajui maisha halisi ya mtanzania wa chini(Kama wanajua wanajua kwa namna kufikirika tu), leo hii hawa ni watu wa kufanyiwa hivi

Kauli kama "Wapigwe tu...",

"Wapinzani(Waliokwenda Upinzani) ni wapumbavu na malofa",

"Mil. 10 ni fedha ya mboga tu",

"Mkishindwa kulipa nauli mpige mbizi",

"Tutashinda tu hata kama kwa goli la mkono" na aina nyingine nyingi ya matusi, kejeli na dharau vinamdhalilisha mwanananchi!

Ninahitaji Kiongozi anayesimamia sheria, inaposemwa mwisho wa mkutano ni saa kumi na mbili jion(saa 12:00), basi na iwe hivyo lakini si saa 1231!

Ninahitaji kiongozi mwenye busara katika matamshi ya maneno na mwenye kuulinda ulimi wake!

Nahitaji kiongozi mwenye kunadi ilani yake, sera zake kwa umakini na namna nitakayoelewa na si kuponda upande mwingine(wa pili) kwasababu ya umasikini wa hoja anazoshindwa kutoa.

Tatizo wengi wa viongozi wanadhani "immunity" waliyonayo inawakinga na UHAI wao! Wananchi pia wana 'threshold' yao ya uvumilivu na hasira. Niwakumbushe tu kuwa kulikuwa na viongozi makini sana 'Nchi za watu' waliouawa tena wakiwa na Ulinzi wa kutosha kwa sababu ya kauli mbovu tu pamoja na umakini wao. Tena kwa sisi na vijana wetu(waliokwenda jeshi) na hawana ajira(ninyi mwawaita vibaka), watakaowa-assassinate, mmoja baada ya mwingine ndipo mtakapotambua 'maskini jeuri' wa nchi hii.

Wengi wanadhani bado wanaweza kupumbaza watu kwa vyombo vya habari vya ndani(Local Media) lakini niseme Afrika Mashariki sasa inaona Afrika na Dunia nzima sasa inaona kinachoendelea Tanzania(ikitazama Viongozi wakubwa wakitukana hadhari, wakistaajabu aibu kubwa ya viongozi kujiandaa kusimama kuponda upande wa pili bila ya wao kuwa na hoja).

Kwa sasa ilani ya CCM imekuwa ni UKAWA, Hoja zao ni UKAWA. Bila UKAWA CCM haitaweza kuwepo!

Hivyo basi mimi na upumbavu, ulofa wangu nikiwa 'kibaka' na 'mnywa viroba' nitaisubiri Oktoba 25, 2015 kwa Mapenzi ya MUNGU kuonyesha ubora wangu na kichinjio changu.

Jitendee haki basi kwa kuwachukia mafisadi wa CCM popote walipo kwa kuunga mkono
ACT wazalendo twende na mama ikulu
 
Jitendee haki basi kwa kuwachukia mafisadi wa CCM popote walipo kwa kuunga mkono
ACT wazalendo twende na mama ikulu

Huku unanadi ACT kule unanadi CCM!!! mna akili kweli??
 
[h=3]KAMPENI ZA MAGUFULI ZAITIKISA MPANDA[/h]

Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wa Mpanda wakati akiwasili kwenye viwanja vya Azimio tayari kwa mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM ambapo alihutubia wananchi hao waliojazana kwa wingi.
Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa Mpanda mkoani Katavi na kuwaambia wananchi hao kuwa hatokuwa na msamaha kwa watu wasiotimiza majukumu yao.
Waziri Mkuu Mhe. Mizengo pinda akimtambulisha Mgombea wa Urais wa CCM Dk. John Pombe magufuli kwa wakazi wa Katumba mkoani Katavi.
Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi Mishamo mkoani Katavi .

Wakazi wa Mishamo Katavi wakionyesha mabango ya kumchagua Magufuli kwenye mkutano wa kampeni.

Wananchi wa Mishamo wakimsikiliza Dk.John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa kampeni za CCM mkoani Katavi.

Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akihutubia wakazi wa Katumba kwenye mkutano wa kampeni wa kumnadi mgombea wa CCM kwa nafasi ya Urais Dk. John Pombe Magufuli.

Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Katumba mkoani Katavi.
Umati wa wakazi wa Katumba kwenye jimbo la Nsimbo wakimsikiliza Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Pombe Magufuli.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
 
MALOFA wote na WAPUMBAVU wote, Tuhakikishe ULOFA na UPUMBAVU wetu unakuwa Historia Jumapili ya Oktoba 25, 2015
SAM_2200.JPG
 
It is very true.

Ni bora sote tunaoitwa wapumbavu na malofa tukatumia 'kichinjio' chetu (kitambulisho) cha kupigia kura, tarehe 25 Oktoba mwaka huu kuwathibitishia wale waliotuita sisi wapumbavu na malofa kuwa sisi siyo malofa bali matajiri wa maamuzi magumu na tutatumia utajiri wetu huo wa fikra kwa kuwang'oa madarakani wale wote waliotuita sisi kuwa ni wapumbavu na malofa.
 
Nimefuatilia sana kuna watu kadhaa ambao mimi nimewatafasri kuwa ni wachovu kisiasa, wanadai eti Mkapa alitukana na baadhi yao wameenda Mbagala rangi 3 kualika mkutano wa Jumamosi. Je watu hawa wamesahau kuwa Sugu aliwahi kumwita Waziri Mkuu Pinda Mpumbavu hadi kesi ikaenda mahakamani na Jaji akatoa uamzi kuwa pumbavu siyo tusi, na wao wakashangilia usiku na mchana. Lakini leo Mh. Mkapa kusema neno lile lile imekua nongwa. " chongo kwa mnywezi kwa Mbowe kengeza".
 
Hiyo lugha yake ya matusi ndiyo aliyoitumia Kule Arumeru mashariki na ndio maana CCM wakaambulia 0.
 
Nimefuatilia sana kuna watu kadhaa ambao mimi nimewatafasri kuwa ni wachovu kisiasa, wanadai eti Mkapa alitukana na baadhi yao wameenda Mbagala rangi 3 kualika mkutano wa Jumamosi. Je watu hawa wamesahau kuwa Sugu aliwahi kumwita Waziri Mkuu Pinda Mpumbavu hadi kesi ikaenda mahakamani na Jaji akatoa uamzi kuwa pumbavu siyo tusi, na wao wakashangilia usiku na mchana. Lakini leo Mh. Mkapa kusema neno lile lile imekua nongwa. " chongo kwa mnywezi kwa Mbowe kengeza".
Tofauti ya sugu na Pinda ni kwamba..SUGU alisema sifa ya kweli ya Pinda na hivyo si tusi...Mkapa kawaita watu anaowaomba Kura ili awaondoe ktk Ulofa kawacheka kwa kuwa malofa....Halafu MKAPA KAELEZA SABABU YA KUWAITA WAPUMBAVU KISHA MWENYEWE AKARUDI NA KUTHIBITISHA SI WAPUMBAVU...kasema nchi imeshakombelewa na CCM ,hapo hapo akamalizia kwamba CCM bado inakimbizana kukomboa watz kutoka k tk Umasiki, ujiinga, maradhi....kwa vipimo na kauli ya Mkapa ni kwamba kawaita wasio wapumbavu kuwa wapumbavu na hivyo katukana.
 
Wewe ukimuita baba yako pumbavu ni kosa?if you know that you have answer.

Swissme
 
Nimefuatilia sana kuna watu kadhaa ambao mimi nimewatafasri kuwa ni wachovu kisiasa, wanadai eti Mkapa alitukana na baadhi yao wameenda Mbagala rangi 3 kualika mkutano wa Jumamosi. Je watu hawa wamesahau kuwa Sugu aliwahi kumwita Waziri Mkuu Pinda Mpumbavu hadi kesi ikaenda mahakamani na Jaji akatoa uamzi kuwa pumbavu siyo tusi, na wao wakashangilia usiku na mchana. Lakini leo Mh. Mkapa kusema neno lile lile imekua nongwa. " chongo kwa mnywezi kwa Mbowe kengeza".
Those fools have short memory.
 
Hajakosea isipokuwa, WATU, kisiasa zaidi, wanamnukuu nusunusu ili wanapofanya usanii wao mitaani wawe na ka'wimbo' ka kusindikizia salamu zao!
 
Hajakosea isipokuwa, WATU, kisiasa zaidi, wanamnukuu nusunusu ili wanapofanya usanii wao mitaani wawe na ka'wimbo' ka kusindikizia salamu zao!
sidhani km hata mama mkapa atakubaliana na wewe km kamwona na kumsikia tena mumewe kabla na baada ya reaaction ya watu....Mkapa hata tukimhurumia tutamwita very IRRESPONSIBLE nadhani bado itakuwa mbaya sana kwake.
 
nyerere aliwahi kusema siwezi kuwapa mbwa nchi na tukasema ni tusi
 
Ukawa ni Malofa na Wapumbavu. An idiot will not see that.
Nani kakuambia ------ hawaoni?Sasa umekuwa mbea kuliko umbea wenyewe.Vipofu na walio na macho ila vit husika vimeficha nao ni ------.
 
Hivi mkiitwa wapumbafu na malofa mtakataa? Mnatumia mda mwingi kujadili maneno mawili ya Nkapa badala ya kujadili hoja za Magufuli, au mmeona kuongea point tupu mmekosa cha kumkosoa?Punguzeni ULOFA basi
 
Back
Top Bottom