Ndugu zangu watanzania,
Katika hali ya ubabe wa viongozi wa CCM na kwa kuwa wanaogopa kama wakitoka madarakani huenda wakafikishwa katika mahakama ya AICC au the Hague.
Kwa mara ya kwanza Kikwete alisikika akilalamika kwa nini mahakama ya AICC inawashughulikia viongozi wa nchi za Africa tu?! Mbona hajaona hata kesi moja inayomuhusu kiongozi wa nchi za Ulaya?!
Lakini katika kutilia mkazo kauli hiyo Rais wa Awamu ya tatu katika serikali ya Jamhuri ya Muungano Ndugu Benjamini W. Mkapa ambaye na yeye ana kashfa nyingi za kujilimbikizia mali. Ndiyo katika kuona hali ya kupelekwa AICC haiepukiki ameamua kufyatuka (sijui alikuwa kisha weka spirit kichwani?) na kuwaita wale wote wanaopigania raslimali za nchi kutumiwa na wanachi ni WAPUMBAVU NA MALOFA.
Nijuavyo mimi;
MALOFA ni watu wasiojua hali yao ya baadae kimaisha itakuwaje kwa upande wa KULA, KUNYWA, MAVAZI na HUDUMA ZA KIJAMII KWA UJUMLA.
WAPUMBAVU ni watu wanayeshindwa kuelewa jambo hata akielezwa, juha, zuzu, jura, nyange, baghami, bahau, hambe, maarasi, zebe, mbumbumbu.
ASUBUHI NJEMA
WAPUMBAVU NA MALOFA WENZANGU.
Ndio Mkapa kawatukanaKuna msemo unasema 'Do not underestimate the power of stupid people in large groups', Ninaimani Mkapa aliyakumbuka haya kabla ya kuita watu ni wapumbavu na malofa!
asante kwa ufafanuzi. nmkapa hoyeeeeeeeee
salaam.
Kampeni za uchaguzi zimefunguliwa na sasa kumekucha tanzania!
Nipende kuwapongeza wanaccm kwa kufungua rasmi kampeni yao hapo jana (23.08.2015) lakini kwa namna mpya ya kejeli, vijembe, matusi(vilivyokataliwa na tume) kutawala ufunguzi huo. Nilishtushwa na kauli za viongozi wa ccm kama vile mh. Benjamin w. Mkapa kutukana hadharani. Mengi yamesemwa ikiwa ni pamoja na kusema "upumbavu na ulofa" si tusi. Nabaki najiuliza hata kama si tusi hakuna maneno makali ya kutumia tofauti na hayo, hasa kwa rais mstaafu? Nakumbuka mh. Tundu lissu aliwahi kutamka maneno hayo bungeni(haikuwa hekima), kwa kuwa alikosea basi ndiyo inahalalisha matumizi yake? Leo inaonekana kama mtindo!
Wazungu wanasema 'great minds discuss ideas, average minds discuss events and small minds discuss people" nilitegemea kwa kikosi kile pengine kutoa maneno ya busara na kutofanya kuwa kijiwe cha chuki kwa waliokatwa.(wakiwakejeli wakiokatwa, na baadhi ya waliokatwa walio ndani ya ccm kumalizia hasira zao pale kwa kuwa walikatwa)!
Wengi wa viongozi hawa hawajui maisha halisi ya mtanzania wa chini(kama wanajua wanajua kwa namna kufikirika tu), leo hii hawa ni watu wa kufanyiwa hivi
kauli kama "wapigwe tu...",
"wapinzani(waliokwenda upinzani) ni wapumbavu na malofa",
"mil. 10 ni fedha ya mboga tu",
"mkishindwa kulipa nauli mpige mbizi",
"tutashinda tu hata kama kwa goli la mkono" na aina nyingine nyingi ya matusi, kejeli na dharau vinamdhalilisha mwanananchi!
Ninahitaji kiongozi anayesimamia sheria, inaposemwa mwisho wa mkutano ni saa kumi na mbili jion(saa 12:00), basi na iwe hivyo lakini si saa 1231!
Ninahitaji kiongozi mwenye busara katika matamshi ya maneno na mwenye kuulinda ulimi wake!
Nahitaji kiongozi mwenye kunadi ilani yake, sera zake kwa umakini na namna nitakayoelewa na si kuponda upande mwingine(wa pili) kwasababu ya umasikini wa hoja anazoshindwa kutoa.
Tatizo wengi wa viongozi wanadhani "immunity" waliyonayo inawakinga na uhai wao! Wananchi pia wana 'threshold' yao ya uvumilivu na hasira. Niwakumbushe tu kuwa kulikuwa na viongozi makini sana 'nchi za watu' waliouawa tena wakiwa na ulinzi wa kutosha kwa sababu ya kauli mbovu tu pamoja na umakini wao. Tena kwa sisi na vijana wetu(waliokwenda jeshi) na hawana ajira(ninyi mwawaita vibaka), watakaowa-assassinate, mmoja baada ya mwingine ndipo mtakapotambua 'maskini jeuri' wa nchi hii.
Wengi wanadhani bado wanaweza kupumbaza watu kwa vyombo vya habari vya ndani(local media) lakini niseme afrika mashariki sasa inaona afrika na dunia nzima sasa inaona kinachoendelea tanzania(ikitazama viongozi wakubwa wakitukana hadhari, wakistaajabu aibu kubwa ya viongozi kujiandaa kusimama kuponda upande wa pili bila ya wao kuwa na hoja).
Kwa sasa ilani ya ccm imekuwa ni ukawa, hoja zao ni ukawa. Bila ukawa ccm haitaweza kuwepo!
Hivyo basi mimi na upumbavu, ulofa wangu nikiwa 'kibaka' na 'mnywa viroba' nitaisubiri oktoba 25, 2015 kwa mapenzi ya mungu kuonyesha ubora wangu na kichinjio changu.
Ndugu zangu watanzania,
Katika hali ya ubabe wa viongozi wa CCM na kwa kuwa wanaogopa kama wakitoka madarakani huenda wakafikishwa katika mahakama ya AICC au the Hague.
Kwa mara ya kwanza Kikwete alisikika akilalamika kwa nini mahakama ya AICC inawashughulikia viongozi wa nchi za Africa tu?! Mbona hajaona hata kesi moja inayomuhusu kiongozi wa nchi za Ulaya?!
Lakini katika kutilia mkazo kauli hiyo Rais wa Awamu ya tatu katika serikali ya Jamhuri ya Muungano Ndugu Benjamini W. Mkapa ambaye na yeye ana kashfa nyingi za kujilimbikizia mali. Ndiyo katika kuona hali ya kupelekwa AICC haiepukiki ameamua kufyatuka (sijui alikuwa kisha weka spirit kichwani?) na kuwaita wale wote wanaopigania raslimali za nchi kutumiwa na wanachi ni WAPUMBAVU NA MALOFA.
Nijuavyo mimi;
MALOFA ni watu wasiojua hali yao ya baadae kimaisha itakuwaje kwa upande wa KULA, KUNYWA, MAVAZI na HUDUMA ZA KIJAMII KWA UJUMLA.
WAPUMBAVU ni watu wanayeshindwa kuelewa jambo hata akielezwa, juha, zuzu, jura, nyange, baghami, bahau, hambe, maarasi, zebe, mbumbumbu.
ASUBUHI NJEMA
WAPUMBAVU NA MALOFA WENZANGU.
Jana mzee Mkapa alimwaga radhi, CCM nayo ikamwaga radhi.
Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, alipopata wasaa wa kuhutubia maelfu ya wanachama wa CCM waliokuwa uwanjani wa Jangwani, alirusha kijembe kwa wapinzani na kusema wanaosema wanatafuta ukombozi ni wapumbavu na malofa.
Kuna vyama vinajifanya vinataka kuleta ukombozi, ukombozi uliletwa na ASP na TANU, hao wanaojiita vyama vya ukombozi ni wapumbavu, ni malofa, nchi hii ilikwisha kombolewa na sasa inaendelea kuikomboa kwa kupambana ana umasikini, ujinga na maradhi na ndo kazi imekuwa ikifanywa na serikali zote zilizopita kuanzia ile ya awamu ya kwanza na hii inayokuja itafanywa na serikali ya Dk. Magufuli, alisema.
Mzee niliyemzoea kwa hoja zenye mashiko na takwimu akageuka mlevi asiyejiheshimu.
Kweli ufalme wa CCM umefitinika.Kati ya mambo ambayo kwa muda mrefu yamekuwa yakiitofautisha brand ya CCM na Upinzani ni kule kutumia lugha zenye staha,kuhubiri amani na kuiishi.Jana rasmi CCM imevunja ndoa yake na sifa hizi.
Sasa tunaanza kupata picha tukimtazama Makonda, baadae Nape,Wasira,Kamani,Job Ndugai na sasa Mkapa tunaona CCM mpya inayozaliwa; brand ya ngumi,matusi na lugha za mihemko.
Mimi niwaambie tu,busara na hekima ni tunu ila ujinga hafundishwi mtu.Ni suala la kuamua tu!
Magufuli karibu UKAWA,you are a good manager but not a leader.
BURIANI CCM!
Watanzania Hivi tumerogwa na nani? Yaani Ziara ya Lowassa Imeleta nini kwa wakazi wa Gongolamboto kama sio cheap politics? Sasa ndio amepeleka nini kwao kama sio usanii??
MODS NAOMBA HURUMA YENU HUU UZI UDUMU KIDOGO
1Wakorinto1:27-28 " bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu;"tena mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa;
Kumbe Mungu ametuchagua tuliodharauliwa ili tuwaiaibishe wenye nguvu! CCM mtaaibika mwaka huu kuanzia kwenye usemi wenu hadi matendo yenu!
Hongera mzee Mkapa, wapumbavu na malofa sio tu wale waliohama CCM kwa uroho wa madaraka, leo nimeamini hata humu JamiiForums wapumbavu na malofa wapo wengi!