Elections 2015 Mzee Mkapa: Wanaosema Wanataka Kuikomboa Tanzania ni Wapumbavu na Malofa

Elections 2015 Mzee Mkapa: Wanaosema Wanataka Kuikomboa Tanzania ni Wapumbavu na Malofa

CHADEMA na UKAWA mpaka sasa wapo gizani. Mbaya zaidi hawajui kuwa wanatawaliwa.


1. Mgombea Urais ni mkoloni ambaye ametoka CCM


2. Mgombea Mwenza ni mkoloni kutoka CUF.


3. Hawana ofisi wamekuwa wapangaji kwa muda mrefu


4. Hawana vyanzo vya mapato wanategemea ufadhili wa wana CCM


5. Hawana uwezo wa kusimamisha wagombea kwa kila jimbo


6. Hawana uwezo wa kuwapata wanachama wapya isipokuwa makapi ya CCM

7. CHADEMA wanahubiri siasa za matukio.

8. Mgombea Urais wao hajui matatizo ya Watanzania. Analazimika kupanda daladala ili kuuliza matatizo ya madereva na makondakta.

Kweli hawa jamaa wapo gizani. Wanahitaji kujikomboa
 
sugu naye alishawahi kuyasema haya maneno kwa hiyo mkapa amepigia tu mstari
 
Kwa tafsiri ya mkapa ni kwamba yeyote asiyekubaliana na mawazo ya kiccm ni mpumbavu na Lofa, kwa kweli kama demokrasia ya Tz ndiyo hii inasikitisha sana.
 
Ndugu zangu watanzania,

Katika hali ya ubabe wa viongozi wa CCM na kwa kuwa wanaogopa kama wakitoka madarakani huenda wakafikishwa katika mahakama ya AICC au the Hague.

Kwa mara ya kwanza Kikwete alisikika akilalamika kwa nini mahakama ya AICC inawashughulikia viongozi wa nchi za Africa tu?! Mbona hajaona hata kesi moja inayomuhusu kiongozi wa nchi za Ulaya?!

Lakini katika kutilia mkazo kauli hiyo Rais wa Awamu ya tatu katika serikali ya Jamhuri ya Muungano Ndugu Benjamini W. Mkapa ambaye na yeye ana kashfa nyingi za kujilimbikizia mali. Ndiyo katika kuona hali ya kupelekwa AICC haiepukiki ameamua kufyatuka (sijui alikuwa kisha weka spirit kichwani?) na kuwaita wale wote wanaopigania raslimali za nchi kutumiwa na wanachi ni WAPUMBAVU NA MALOFA.

Nijuavyo mimi;

MALOFA ni watu wasiojua hali yao ya baadae kimaisha itakuwaje kwa upande wa KULA, KUNYWA, MAVAZI na HUDUMA ZA KIJAMII KWA UJUMLA.

WAPUMBAVU ni watu wanayeshindwa kuelewa jambo hata akielezwa, juha, zuzu, jura, nyange, baghami, bahau, hambe, maarasi, zebe, mbumbumbu.

ASUBUHI NJEMA

WAPUMBAVU NA MALOFA WENZANGU.

Hapo kwenye Red nakubaliana nawe mkuu..yeye na Makongoro walikuwa wapo maji
 
Kuna msemo unasema 'Do not underestimate the power of stupid people in large groups', Ninaimani Mkapa aliyakumbuka haya kabla ya kuita watu ni wapumbavu na malofa!
Ndio Mkapa kawatukana
tena ni Sumaye ambaye Mkapa katika Utawala wake kamuachia miaka 10 yote
  • Sumaye alilivunja Baraza la Madiwani la Jiji la Dsm na akaipa Tume ya Keenja wakati Jiji lote lilishika na kina Masumbuko Lamwai na kina MremaMkapa alikuwa ----- kunyamaza
  • Sumaye aliwapiga marufuku wafanyabiashara wote wa Tanzania kuishabikia NCCR ukionekana tu Leseni au TRA hao katika bisahara zako.Mkapa alikuwa ----- kunyamaza
  • Sumaye alijiamulia kila kiti licha ya kukopa NSSF mamilioni Mkapa alikuwa ----- kunyamaza
  • Sumaye alianziahs mashamba makubwa na kuwaweka Ndugu zake waMbulu na Mkapa alikuwa ----- kunyamaza

hippocratessocrates dogo kapige kura yako unakojua lakini Siasa huijui na hujui Sumaye alikuwa Waziri Mkuu wakati wa nani na kwa nini hana shukrani
naona weweni wa small Mind badala ya (Simple Mind)
 
asante kwa ufafanuzi. nmkapa hoyeeeeeeeee

Ukumbuke kwamba hata wewe alikutukana ila hujua tu.

Tuliyemweka madarakani kwa miaka kumi alipotoka alitoka na utajiri na ukwasi usiosemeka.Bado na kuuza NBC na mashirika ya umma kwa bei poa na mengi yakiwa yanafanya biashara nzuri tuliendelea kumpigia makofi mapka kesho.Kwanini asituite Maolfa na wapumbavu.

Huyu aligawa Madini yetu kwa wazungu/wakoloni kwa jina la wawekezaji eti akatudanganyia na asilimi 3 na wakoloni asilimia 97,na hapo kuna 20 za kwake leo madini yamezinufaisha nchi za wazungu na kutuacha Tanzania tukiwa kwenye lindi la Umasikini,ufukara na bado alivyowekwa JK kwa shangwe tukaingia kingi tukamchagua,leo uchumi wetu nafuu enzi za mkoloni,kaka yangu kwanini wewe na mimi tusitwe Wapumbavu na Malofa.

JK anaondoka IKULU akiwa na UTAJIRI na UKWASI usiosemeka,tumeona wizi wa mali za umma na uvunaji wa meno ya tembo,madawa ya kulevya,rushwa na ufisadi ukiwa kwenye kiwngo cha juu,bado anayekuja anatupa promise alizotupa miaka 20 iliyopita MKAPA,miaka 10 iliyopita JK na leo tunapewa ahadi zile zile!!!!!!!!!!

Ndugu yangu kwanini tusiitwe wapumbavu na malofa.Rafiki haijalishi uko chama gani sisi watanznaia ndiyo tuliotukanwa na si vyama vya upinzani tu,chukua acha.Leo aliyetukana akiumwa hata mafuao anaenda APPOLLO india wewe ukiumwa unaenda wapi??Je dawa zipo,hospitali zetu je.Watoto wao leo wako wapi??

Usijeukadhani kwenye TUSI lile wewe hauko.Upo vizuri sana.Maana kuikomboa Tanzania siyo kwenye uhuru tu hata kifikra ,kiuchumi,kielimu,na afya,na ndicho baadaye na yeye alisema...Je wewe na mimi sote si ndiyo wale wale wapumbavu na malofa????:hurt::hurt:
 
watu wa kanda maalumu wamemzingira Makufuri

30.jpg
 
salaam.

Kampeni za uchaguzi zimefunguliwa na sasa kumekucha tanzania!

Nipende kuwapongeza wanaccm kwa kufungua rasmi kampeni yao hapo jana (23.08.2015) lakini kwa namna mpya ya kejeli, vijembe, matusi(vilivyokataliwa na tume) kutawala ufunguzi huo. Nilishtushwa na kauli za viongozi wa ccm kama vile mh. Benjamin w. Mkapa kutukana hadharani. Mengi yamesemwa ikiwa ni pamoja na kusema "upumbavu na ulofa" si tusi. Nabaki najiuliza hata kama si tusi hakuna maneno makali ya kutumia tofauti na hayo, hasa kwa rais mstaafu? Nakumbuka mh. Tundu lissu aliwahi kutamka maneno hayo bungeni(haikuwa hekima), kwa kuwa alikosea basi ndiyo inahalalisha matumizi yake? Leo inaonekana kama mtindo!

Wazungu wanasema 'great minds discuss ideas, average minds discuss events and small minds discuss people" nilitegemea kwa kikosi kile pengine kutoa maneno ya busara na kutofanya kuwa kijiwe cha chuki kwa waliokatwa.(wakiwakejeli wakiokatwa, na baadhi ya waliokatwa walio ndani ya ccm kumalizia hasira zao pale kwa kuwa walikatwa)!

Wengi wa viongozi hawa hawajui maisha halisi ya mtanzania wa chini(kama wanajua wanajua kwa namna kufikirika tu), leo hii hawa ni watu wa kufanyiwa hivi

kauli kama "wapigwe tu...",

"wapinzani(waliokwenda upinzani) ni wapumbavu na malofa",

"mil. 10 ni fedha ya mboga tu",

"mkishindwa kulipa nauli mpige mbizi",

"tutashinda tu hata kama kwa goli la mkono" na aina nyingine nyingi ya matusi, kejeli na dharau vinamdhalilisha mwanananchi!

Ninahitaji kiongozi anayesimamia sheria, inaposemwa mwisho wa mkutano ni saa kumi na mbili jion(saa 12:00), basi na iwe hivyo lakini si saa 1231!

Ninahitaji kiongozi mwenye busara katika matamshi ya maneno na mwenye kuulinda ulimi wake!

Nahitaji kiongozi mwenye kunadi ilani yake, sera zake kwa umakini na namna nitakayoelewa na si kuponda upande mwingine(wa pili) kwasababu ya umasikini wa hoja anazoshindwa kutoa.


Tatizo wengi wa viongozi wanadhani "immunity" waliyonayo inawakinga na uhai wao! Wananchi pia wana 'threshold' yao ya uvumilivu na hasira. Niwakumbushe tu kuwa kulikuwa na viongozi makini sana 'nchi za watu' waliouawa tena wakiwa na ulinzi wa kutosha kwa sababu ya kauli mbovu tu pamoja na umakini wao. Tena kwa sisi na vijana wetu(waliokwenda jeshi) na hawana ajira(ninyi mwawaita vibaka), watakaowa-assassinate, mmoja baada ya mwingine ndipo mtakapotambua 'maskini jeuri' wa nchi hii.

Wengi wanadhani bado wanaweza kupumbaza watu kwa vyombo vya habari vya ndani(local media) lakini niseme afrika mashariki sasa inaona afrika na dunia nzima sasa inaona kinachoendelea tanzania(ikitazama viongozi wakubwa wakitukana hadhari, wakistaajabu aibu kubwa ya viongozi kujiandaa kusimama kuponda upande wa pili bila ya wao kuwa na hoja).

Kwa sasa ilani ya ccm imekuwa ni ukawa, hoja zao ni ukawa. Bila ukawa ccm haitaweza kuwepo!

Hivyo basi mimi na upumbavu, ulofa wangu nikiwa 'kibaka' na 'mnywa viroba' nitaisubiri oktoba 25, 2015 kwa mapenzi ya mungu kuonyesha ubora wangu na kichinjio changu.

hakika we lofa na pumbavu kweli sasa tunakuambia hicho kichinjio chako kitunze, ila jua raisi ni magufuli
 
Ndugu zangu watanzania,

Katika hali ya ubabe wa viongozi wa CCM na kwa kuwa wanaogopa kama wakitoka madarakani huenda wakafikishwa katika mahakama ya AICC au the Hague.

Kwa mara ya kwanza Kikwete alisikika akilalamika kwa nini mahakama ya AICC inawashughulikia viongozi wa nchi za Africa tu?! Mbona hajaona hata kesi moja inayomuhusu kiongozi wa nchi za Ulaya?!

Lakini katika kutilia mkazo kauli hiyo Rais wa Awamu ya tatu katika serikali ya Jamhuri ya Muungano Ndugu Benjamini W. Mkapa ambaye na yeye ana kashfa nyingi za kujilimbikizia mali. Ndiyo katika kuona hali ya kupelekwa AICC haiepukiki ameamua kufyatuka (sijui alikuwa kisha weka spirit kichwani?) na kuwaita wale wote wanaopigania raslimali za nchi kutumiwa na wanachi ni WAPUMBAVU NA MALOFA.

Nijuavyo mimi;

MALOFA ni watu wasiojua hali yao ya baadae kimaisha itakuwaje kwa upande wa KULA, KUNYWA, MAVAZI na HUDUMA ZA KIJAMII KWA UJUMLA.

WAPUMBAVU ni watu wanayeshindwa kuelewa jambo hata akielezwa, juha, zuzu, jura, nyange, baghami, bahau, hambe, maarasi, zebe, mbumbumbu.

ASUBUHI NJEMA

WAPUMBAVU NA MALOFA WENZANGU.

Mimi na familia yangu yote tunaitwa wapumbavu na malofa,hiki kiburi sijui kinatoka wapi
 
Jana mzee Mkapa alimwaga radhi, CCM nayo ikamwaga radhi.

Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, alipopata wasaa wa kuhutubia maelfu ya wanachama wa CCM waliokuwa uwanjani wa Jangwani, alirusha kijembe kwa wapinzani na kusema wanaosema wanatafuta ukombozi ni wapumbavu na malofa.

“Kuna vyama vinajifanya vinataka kuleta ukombozi, ukombozi uliletwa na ASP na TANU, hao wanaojiita vyama vya ukombozi ni wapumbavu, … ni malofa, nchi hii ilikwisha kombolewa na sasa inaendelea kuikomboa kwa kupambana ana umasikini, ujinga na maradhi na ndo kazi imekuwa ikifanywa na serikali zote zilizopita kuanzia ile ya awamu ya kwanza na hii inayokuja itafanywa na serikali ya Dk. Magufuli,” alisema.

Mzee niliyemzoea kwa hoja zenye mashiko na takwimu akageuka mlevi asiyejiheshimu.

Kweli ufalme wa CCM umefitinika.Kati ya mambo ambayo kwa muda mrefu yamekuwa yakiitofautisha brand ya CCM na Upinzani ni kule kutumia lugha zenye staha,kuhubiri amani na kuiishi.Jana rasmi CCM imevunja ndoa yake na sifa hizi.

Sasa tunaanza kupata picha tukimtazama Makonda, baadae Nape,Wasira,Kamani,Job Ndugai na sasa Mkapa tunaona CCM mpya inayozaliwa; brand ya ngumi,matusi na lugha za mihemko.

Mimi niwaambie tu,busara na hekima ni tunu ila ujinga hafundishwi mtu.Ni suala la kuamua tu!

Magufuli karibu UKAWA,you are a good manager but not a leader.

BURIANI CCM!



CCM imewatukana watanzania
 
Last edited by a moderator:
QUOTE=Domy;13749200]Mpumbavu na Lofa ni yule aliyeuza Benki kwa bei ya kutupa![/QUOTE]
attachment.php

Paul Alex huyo ndiye mbabe Mkapa aliyeweza kukaa na Sumaye kama Waziri Mkuu kwa miaka 10
na enzi hizo Wapinzani (Mrema na NCCR) bila ya kufurukuta licha ya MEDIA nayo kutukanwa kubanwa
leo mnashangaa matusi
HIVI ANGERUDI sijui UKAWA wangeenda wapi?
 

Attachments

  • JK.jpeg
    JK.jpeg
    8.5 KB · Views: 401
Hongera mzee Mkapa, wapumbavu na malofa sio tu wale waliohama CCM kwa uroho wa madaraka, leo nimeamini hata humu JamiiForums wapumbavu na malofa wapo wengi!
 
MODS NAOMBA HURUMA YENU HUU UZI UDUMU KIDOGO


1Wakorinto1:27-28 " bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu;"tena mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa;

Kumbe Mungu ametuchagua tuliodharauliwa ili tuwaiaibishe wenye nguvu! CCM mtaaibika mwaka huu kuanzia kwenye usemi wenu hadi matendo yenu!
 
Watanzania Hivi tumerogwa na nani? Yaani Ziara ya Lowassa Imeleta nini kwa wakazi wa Gongolamboto kama sio cheap politics? Sasa ndio amepeleka nini kwao kama sio usanii??

Alitaka awe karibu zaidi na Malofa wa pande hizo.
 
Vichekesho Kweli,eti Chama Cha Watu Wa Kanda Ya Kaskazin Ndo Kishke Dora?Bora Umpe Nchi Msukuma Kuliko Mtu Wa Kanda Ya Kaskazn Maana Ukimpa Utakuta Kina Mlay,mushi Ndo Watatusumbua Sana,kama Sasa Wanavyokuwa Wasumbufu Kwenye Maofs,kwa Tunaoujua Hatuhangaiki.Mbinu Za Watu Wa Kaskazn Kushka Dora Tumeshaziona,
 
MODS NAOMBA HURUMA YENU HUU UZI UDUMU KIDOGO


1Wakorinto1:27-28 " bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu;"tena mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa;

Kumbe Mungu ametuchagua tuliodharauliwa ili tuwaiaibishe wenye nguvu! CCM mtaaibika mwaka huu kuanzia kwenye usemi wenu hadi matendo yenu!

Mungu Si Dhalim Kama Wewe,usitake Kubdirisha Neno La Mungu,na Wala Usitake Kumsafisha Mtu Kwa Ku2mia Neno La Mungu.Be Careful Unapokuwa Ukitamka Neno La Muumba Wako.
 
1Wakorinto1:27-28 " bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu;"tena mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa;: Kwahiyo Mungu amechaguwa UKAWA sisi Wapumbavu na malofa ili tuwaaaibishe CCM wenye hekima na nguvu.
 
Back
Top Bottom