Heshima yenu wanabodi!
Nimesikitishwa sana na kitendo cha Rais wa tatu wa Tanzania Mh.Benjamin Mkapa kuporomosha matusi jukwaani badala ya kujenga hoja!
Mkapa amekuwa mtu wa kupanic sana tangu alipokuwa Rais,aliwatukana waandishi wa habari wa Tanzania hadharani na kuwaita wasiofaa huku akiwakumbatia waandishi wa nje.
Wakati wa kampeni za ubunge jimbo la arumeru mashariki Mkapa pia aliporomosha matusi kwa wapinzani badala ya kujenga hoja matokeo yake Chadema ilishinda asubuhi na yeye kukimbilia uwanja wa ndege na kuondoka mapema sana asubuhi!
Mkapa amerudia kuporomosha matusi jana kwenye uzinduzi wa kampeni za CCM na kuwaita watu malofa na wapumbavu! Hivi mh.Mkapa pamoja na kukaa ikulu miaka kumi anashindwa kujenga hoja kweli na anaamua kutumia matusi kama sehemu ya kampeni kweli?
Wapinzani fanyeni kampeni ya kistaarabu acheni kujibu matusi ya Mkapa,waelezeni watanzania mtawafanyia nini mkipewa ridhaa,wananchi wanataka maendeleo sio matusi!
Kila la heri UKAWA kila la heri Lowassa na maalimu Seif.
MAIGIZO KWENYE MAISHA YA WATU NI DHAMBI MBAYA NA AIMPENDEZI MUNGU.
Mkapa was one of the intellegent president ambae anauwezo mkubwa sana kiufahamu kuwaita SASA LOWASA NA SUMAYE WAPUMBAVU NA MALOFA.
HAKIKA mtu mwerevu akifikia kutumia TERMS za aina hiyo basi ujue kamdharau mhusika kupewa terms hizo yani hana tofauti na yule jamaa wa ile picha iliotoka jamaa anafanya maneno na ile kitambaa ya Ukawa.
Manake mtu kuitwa Mpambavu ni extreme ya wajinga kwa kuwa imemchukua Mzee Mkapa 10 years kumtrain Sumaye aka ZERO ...Lakini with all training on how to be a true Leader bado uziro umetamalaki.
Sasa ona mwingine nae watu wanasubilia utoe llani yenu watu wajue nini mtafanya anaingia kwenye madaladala kwenda kutafuta scrip ya uwezo wa akili yake ya kikomed.
Hata kina joti wanawakilisha ujumbe ..sasa kupanda daladala katika zama za kutoweza hata kupunga mkono leo toka miaka ya Pesa ya kukwapua kwa Baba na kununua Voku...ujapanda daladala leo hii kuja kusanifu maisha ya watu wa chini kama si kumchokoza Mungu si upunguani huo.
Haya kama wanazani maisha ya watu ufanyiwa majaribio msemo wa Mrisho...haya ngoja tuone wao na dhihaka kwa Muumba kupanda na kuenjoy usanii wa kinafiiki na kuwafanya Watanzania wajinga ni watu wa kudanganywa kama watoto wadogo.
Kila mtanzania angependa kuwa na Private Car yake ama usafiri wa umma ulio bora na kisasa usio na msongamano na hivyo mtanzania huyo kwa usafiri wa yeye na familia yake.kuwa wa kistaarabu na afya .
Lakini kwa kuwa MAFISADI wamekwapua na kusafisha cha umma kuwa chao ..sasa wanakufuru kwenda kuwananga kwa roho walio wakwapulia NASEMA MALIPO NI HAPA HAPA DUNIA.
WAO WAENDELEE KUMDHIHAKI MUNGU.