Elections 2015 Mzee Mkapa: Wanaosema Wanataka Kuikomboa Tanzania ni Wapumbavu na Malofa

Elections 2015 Mzee Mkapa: Wanaosema Wanataka Kuikomboa Tanzania ni Wapumbavu na Malofa

Wakuu, huwa najiuliza kwa nini Raisi Mstaafu Mh. Benjameni William Mkapa (a.k.a Mr. Clean) huwa hatunukiwi ile tuzo ya MO inayowahusu Maraisi wastaafu na kusimamiwa na Ahmed Salimu? Labda ni kwa sababu ana Jazba sana au....
Kwa matusi yale ya jana asitegemee kupata hata tuzo ya Kilimanjaro Music Awards(KTM)
 
Kwasasa mshapoteza hadhi yakumkashifu yeyote ndani ya CCM,tena ni vema mkaweka akiba ya maneno kwani hamuwezi jua 2020 kitatokea nini,mlimwita Lowasa fisadi leo mmemkabidhi bendera,sasa naona mnataka kurudia kosa lilelile,ni bora mkae kimya mshazoea vyakunyonga.
Mtaanza kumkashifu mzee Mkapa halafu kesho mtageuza maneno

Naona team campaign mpya mnaingia,karibuni!
Ondoeni hangover kwanza!

CCM mwisho wake umefika na ni nyie tu mliosinzia hamjui!
Toroka Uje,kibanda kinaungua.
 
Leo hii asubuhi jamaa huyu ndugu Bashiru Ally akihojiwa na shirika la utangazaji la BBC kasema mtazamo wake wa ujumla ni kwamba kampeni zilizoanza jana zimetawakiwa na vijembe, matusi na kushambuliana na akaonesha kuwa ana wasiwasi na kama wagombea na vyama vyao wenda watashindwa kujikita katika kuchambua sera na ilani zao.

Maajabu ya mchana, muda c mrefu akiobgea ba kituo cha matangazo cha DW cha ujerumani akihojiwa mara anabadirija ndani ya masaa 7 na kusema kampeni zilijikita katika kuchambua sera na ilani, binafsi nimeshabgazwa na undumila kuwili wa msomi huyu wa kiwango udhamiri kutojielewa na kukosa msimamo na sijui tuseme ndiyo wasomi wetu...?

Ebu ifike mahala wasomi tusimamie kile tunachokiona na kukijua kwa mjibu wa taaluma zetu, msidhani sasa hivi watu ni vipofu tunafuatilia kila point ya kauli ya watu mnaosema kwa niaba ya umma.

Binafsi jana nimekerwa na lugha za kebehi na matusi zilizotolewa na viongozi wastaafu wa kitaifa na makada wa ccm, wakiongozwa na mzee mkapa asiye kuwa na chembe ya uvumilivu kwa kuwaita watanzania kuwa ni wapumbavu na malofa...!

Licha yakuwa ni makada wa chama cha ccm, wanapaswa kuongozwa na hekima na busara hasa kuzuia kauli za kebehi na matusi kama alivyofanya mkapa.

Naomba nimalizie na rais kikwete kwa kumuonya kwa kumwambia yeye bado ni rais wa watanzania licha ya kuwa ni chairman wa ccm anatakiwa kutumia busara katika kunadi chama chake ili kuepusha kauli za kugawa nchi katika matabaka zaidi ingawa mpaka sasa matabaka ya kiuchumi ni dhahiri yapo.

Lakini tusipokuwa makini tutaangukia katika mtego wa MAHAKAMS ZA KIMATAIFA juzi Fatu bensuda kaonya juu ya matumizi mabaya ya vyombo vya ulinzi kwenye uchaguzi.
 
Mbona mnapotosha maana halisi nyie watu' Mheshimiwa mkapa amesema' Nanukuu' Kuna watu wanajifanya leo hii wanataka kuwakomboa watanzania wakati watanzania walishakombolewatangu enzi za Tanu na Asp kutoka kwa wakoloni watu hao Wanaojifanya Wanataka Kuwakomboa Watanzania Ni WAPUMBAVU" Eti mnasema Mkapa kawatukana watanzania Acheni Uongo Tusi Lenu Lile Ukawa, Kwani nani asiyejua sera za ukawa ni kuwakomboa watanzania kutoka kwenye Umasikini' wkt wenyewe hata hawafanani na wanachokisema Nyuso zao wote zimejaa uchu wa madaraka kila mmoja, Hivi Niwaulize! Nyie mliotoka ccm' Hivi Kweli Mlikuwa Na Nia Hii Ya Kutukomboa Watanzania Na Kuleta Mabadiliko Toka Kitambo..? Au Idea Hii Imekuja Pale Tu Alipokatwa Jina Baba Yenu Lowasa..? Kama Toka Kitambo Basi Mngetoka Nae Mapema Wala Msingesubiri Ccm Imkate Jina, Na Kama Baada Ya Kukatwa Jina Basi Dhahiri Kwamba Nyinyi Mna Uchu Wa Madaraka Kama Sio Ubinafsi, Kwani Nyinyi Mbona Hamfiki Hata Theruthi Ya Wana Ccm Wote Na Wala Hamstahili Kuongozi Umma Wa Watanzania Wote.

Mwenye uchu wa madaraka ni nani?
Ni aliyetawala miaka 50 na bado anataka kutawala?

Au ni anayeomba uongozi leo mara ya kwanza atumikie kwa heshima?
 
"Malofa na wapumbavu" wenzangu tunaohitaji ukombozi mpo?

Sikuwahi kujua kuwa kutaka kujikomboa kutokana na huduma mbaya za matibabu, akina mama wanaosubiri kujifungua kulala chini, haki ya kupata matibabu sahihi na kwa wakati kupatikana India na kwingineko ni ulofa na upumbavu.

Sikuwahi kujua kuwa ukitaka kujikomboa kutokana na kupata Elimu duni na bila kuwa na walimu wa kutosha, walimu wetu kutokupata mishahara na kama wakipata inakuwa imepunjwa nao ni ulofa na upumbavu!

Eti ni ulofa kutaka kujikomboa kutoka kumchagua muwakilishi wako halafu akifika kule anakokuwakilisha anaishia kuunga mkono kila kitu hata kama kinakuumiza wewe uliyemtuma!

Eti ni ulofa na upumbavu unapotaka kukiondoa chama kilichokaa madarakani kikajisahau kuwa kinatakiwa kusimamia rasilimali kwa manufaa ya wananchi wake kinaamua kuwalinda walioshindwa kuzilinda rasilimali hizo na wale wanaozipora kwa manufaa binafsi!

Au huu ulofa na upumbavu umekuja kwa sababu tumekaa muda mrefu bila kuchukua hatua???
 
Ni jambo la ajabu sana kwa kuwa chanzo cha ulofa na upumbavu ni matokeo ya Sera ya serekali ya ccm kwa kuua viwanda na elimu halafu wanatukebehi kwa mambo walioyaanzisha wao. Wakati ccm hii haijapoteza dira ajira na elimu vilikuwa vitu muhimu kwa vijana lakini sio sasa kwa kuuza kila kiwanda na kuharibu mfumo wa elimu.
 
Ina maana mtu hawezi kuchangia tofauti tofauti kwa nyakati tofauti? Hawa wanaojiita wachambuzi sometime hunichosha!!!
 
Ina maana mtu hawezi kuchangia tofauti tofauti kwa nyakati tofauti? Hawa wanaojiita wachambuzi sometime hunichosha!!!

Kusimamia unachokiona na kuamini kunaleta heshima mtu asubuhi hivi mchana kitu kilekile kabadirika...! Si tabia ya kisomi huu ni ukanjanja ns ukasuku kama wasanii..
 
Upumbavu na ulofa wetu wameusababisha wenyewe halafu sasa wanatutukana,kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu tumejitambua,sasa tunajijua kuwa si wapumbavu na malofa,na kizuri zaidi tu tumeshajua chanzo chake ni CCM,suluhisho letu kutumia kikatio chetu kukata mnyororo huu tuliofungwa nao kwenye upumbavu na ulofa.
 
Hata mm nimemsikia nimeshapata sana hivi hawa wasome wa Tanzania wako je hawa wezi simamia wanayoyaona na kuamini Bush iri huyuuuu anayeichambua siasa za ccm leo amegeuka kbs an sema jana kulikuwa siasa za kistaarabu!!!!!!
 
Ni nani mwenye uwezo wa kuleta Ukombozi huko UKAWA wakati SUMAYE ndio kwanza amekuja kuwasaidia kuendesha SERIKALI?

"Malofa na wapumbavu" wenzangu tunaohitaji ukombozi mpo?

Sikuwahi kujua kuwa kutaka kujikomboa kutokana na huduma mbaya za matibabu, akina mama wanaosubiri kujifungua kulala chini, haki ya kupata matibabu sahihi na kwa wakati kupatikana India na kwingineko ni ulofa na upumbavu.

Sikuwahi kujua kuwa ukitaka kujikomboa kutokana na kupata Elimu duni na bila kuwa na walimu wa kutosha, walimu wetu kutokupata mishahara na kama wakipata inakuwa imepunjwa nao ni ulofa na upumbavu!

Eti ni ulofa kutaka kujikomboa kutoka kumchagua muwakilishi wako halafu akifika kule anakokuwakilisha anaishia kuunga mkono kila kitu hata kama kinakuumiza wewe uliyemtuma!

Eti ni ulofa na upumbavu unapotaka kukiondoa chama kilichokaa madarakani kikajisahau kuwa kinatakiwa kusimamia rasilimali kwa manufaa ya wananchi wake kinaamua kuwalinda walioshindwa kuzilinda rasilimali hizo na wale wanaozipora kwa manufaa binafsi!

Au huu ulofa na upumbavu umekuja kwa sababu tumekaa muda mrefu bila kuchukua hatua???
 
Sikutegemea kama mkapa anaweza ku bwatuka namna ile kweli ccm wameshikwa pabaya mwaka huu
 
Wale wale wakishatishiwa kidogo tu au kujikomba kwa wanasiasa nilidhani ni Bana peke yake kumbe wako wengi pale udsm kumbe maccm wako wengi
 
Ni aibu kwa chama cha upinzani kukaa miaka jirani bila kuandaa mgombea wa urais wa chama hicho. Sasa kama kuandaa mtu mmoja wameshindwa kwa miaka 5 watawezaje kuwaletea watanzania mil 50 maendeleo kwa miaka hiyo mitano. This is a joke.
 
Huyu mwizi alianza matusi siku nyingi,mtakumbuka kwenye uchaguzi wa Arumeru alimtusi waziwazi Vicent Nyerere.Nadhani alipovunjwa nyonga na akilia zikaisha,demented old crook
 
Mzee anapokosa hekima inasikitisha sana!sijui ni kupanick au nini!atauona ulofa wetu na upumbavu kwy box
 
Back
Top Bottom