Kwa matusi yale ya jana asitegemee kupata hata tuzo ya Kilimanjaro Music Awards(KTM)Wakuu, huwa najiuliza kwa nini Raisi Mstaafu Mh. Benjameni William Mkapa (a.k.a Mr. Clean) huwa hatunukiwi ile tuzo ya MO inayowahusu Maraisi wastaafu na kusimamiwa na Ahmed Salimu? Labda ni kwa sababu ana Jazba sana au....
Kwasasa mshapoteza hadhi yakumkashifu yeyote ndani ya CCM,tena ni vema mkaweka akiba ya maneno kwani hamuwezi jua 2020 kitatokea nini,mlimwita Lowasa fisadi leo mmemkabidhi bendera,sasa naona mnataka kurudia kosa lilelile,ni bora mkae kimya mshazoea vyakunyonga.
Mtaanza kumkashifu mzee Mkapa halafu kesho mtageuza maneno
Mbona mnapotosha maana halisi nyie watu' Mheshimiwa mkapa amesema' Nanukuu' Kuna watu wanajifanya leo hii wanataka kuwakomboa watanzania wakati watanzania walishakombolewatangu enzi za Tanu na Asp kutoka kwa wakoloni watu hao Wanaojifanya Wanataka Kuwakomboa Watanzania Ni WAPUMBAVU" Eti mnasema Mkapa kawatukana watanzania Acheni Uongo Tusi Lenu Lile Ukawa, Kwani nani asiyejua sera za ukawa ni kuwakomboa watanzania kutoka kwenye Umasikini' wkt wenyewe hata hawafanani na wanachokisema Nyuso zao wote zimejaa uchu wa madaraka kila mmoja, Hivi Niwaulize! Nyie mliotoka ccm' Hivi Kweli Mlikuwa Na Nia Hii Ya Kutukomboa Watanzania Na Kuleta Mabadiliko Toka Kitambo..? Au Idea Hii Imekuja Pale Tu Alipokatwa Jina Baba Yenu Lowasa..? Kama Toka Kitambo Basi Mngetoka Nae Mapema Wala Msingesubiri Ccm Imkate Jina, Na Kama Baada Ya Kukatwa Jina Basi Dhahiri Kwamba Nyinyi Mna Uchu Wa Madaraka Kama Sio Ubinafsi, Kwani Nyinyi Mbona Hamfiki Hata Theruthi Ya Wana Ccm Wote Na Wala Hamstahili Kuongozi Umma Wa Watanzania Wote.
Ina maana mtu hawezi kuchangia tofauti tofauti kwa nyakati tofauti? Hawa wanaojiita wachambuzi sometime hunichosha!!!
"Malofa na wapumbavu" wenzangu tunaohitaji ukombozi mpo?
Sikuwahi kujua kuwa kutaka kujikomboa kutokana na huduma mbaya za matibabu, akina mama wanaosubiri kujifungua kulala chini, haki ya kupata matibabu sahihi na kwa wakati kupatikana India na kwingineko ni ulofa na upumbavu.
Sikuwahi kujua kuwa ukitaka kujikomboa kutokana na kupata Elimu duni na bila kuwa na walimu wa kutosha, walimu wetu kutokupata mishahara na kama wakipata inakuwa imepunjwa nao ni ulofa na upumbavu!
Eti ni ulofa kutaka kujikomboa kutoka kumchagua muwakilishi wako halafu akifika kule anakokuwakilisha anaishia kuunga mkono kila kitu hata kama kinakuumiza wewe uliyemtuma!
Eti ni ulofa na upumbavu unapotaka kukiondoa chama kilichokaa madarakani kikajisahau kuwa kinatakiwa kusimamia rasilimali kwa manufaa ya wananchi wake kinaamua kuwalinda walioshindwa kuzilinda rasilimali hizo na wale wanaozipora kwa manufaa binafsi!
Au huu ulofa na upumbavu umekuja kwa sababu tumekaa muda mrefu bila kuchukua hatua???
Stupid gang of devils
This time we will know the truth about the the death of the father of our nation. Wait the game is begining!! ICC /hague