Mzee mmoja alikuwa haudhurii misiba leo kafariki, kinachoendelea hapa naona ni msiba wa familia tu

Ila ni sawa tu maana wasioenda wamewapunguzia gharama wafiwa. Kama familia inajiweza kiasi hapo ni kununua tu jeneza, wakodi watu wachache wa kusaidia kuzika makaburini, siku imeisha.
Huwa tunacomplicate sana misiba
Sio misiba tu ndugu, Watanzania tunacomplicate ubatizo, kutahiri kijana wa kiume, kuvunja ungo kwa binti, kipaimara,komunio, mahafali, birthdays, sikukuu, kuagwa kwa mabinti wanaoenda kuolewa na ndoa.

Kiujumla, ni Tanzania pekee kila jambo limtokealo mtu linatafutiwa sherehe.
 
Wafundisheni upendo.
Acheni chuki na visasi
Ushindeni ubaya kwa wema
Kwanini mna kuwa na chuki kama wapagani ilihali hata wapagani wako na afadhali.
 
Waswahili watu wa nongwa Sana.....wanataka kila mtu aache mambo yake ya msingi ahudhurie misiba utasema wewe ndio utamfufua....
Kwanza kwenye misiba wingi wao kama NZI hauna faida yoyote zaidi ya kula, kunywa na kujaza Choo tu.......kama wamesusa ndio vizuri.....unaita funeral service.... wana maliza kazi.....mnaendelea na mambo mengine....
 
Hakuwa anahudhuria Nzengo!
Hakuwa anatoa michango ya Nzengo!
Marehemu alikuwa anajidai sana!
Akina mama hatupiki wala kulia!

Bongo hii watu tuna nongwa sana. 😁
Mnaivimbia familia yenye uwezo si wanaleta buffer tu wanakula,mazikoni mwili unabebwa na gari.
Haya mambo yanafaa kwa watu masikini au vijijini huko ndo mambo ya umoja ni nguvu.
 
Ila ni sawa tu maana wasioenda wamewapunguzia gharama wafiwa. Kama familia inajiweza kiasi hapo ni kununua tu jeneza, wakodi watu wachache wa kusaidia kuzika makaburini, siku imeisha.
Huwa tunacomplicate sana misiba
MTU akifa uende au usiende kwa aliekifa hana cha kupoteza...
Hujambo jirani
 
Hapana,nadhani amemaanisha mtu akifa hata mkimwacha aozee ndani bado haipunguzi kitu maana tayari ameshakufa.
Msicomplicate mambo wakuu,msiba si lazima mzike wote
 
Tena na wengine wanafika mbali zaidi wana haribu na mazingira kwa kujisaidia hovyo hovyo tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…