Mzee mmoja alikuwa haudhurii misiba leo kafariki, kinachoendelea hapa naona ni msiba wa familia tu

Kwahiyo Wana nzengo mnamkomoa marehemu!
Nendeni mkamsitiri mwenzenu acheni mambo yenu hayo.
 
😂😂😂

Kwan Kuna Sheria inasemaje kuhusu aina ya mapishi mazikoni?
 
Hata msipoenda atazikwa tu
 
Ila ni sawa tu maana wasioenda wamewapunguzia gharama wafiwa. Kama familia inajiweza kiasi hapo ni kununua tu jeneza, wakodi watu wachache wa kusaidia kuzika makaburini, siku imeisha.
Huwa tunacomplicate sana misiba
Ndio maana kuna umuhimu wa kuwepo na yale makampuni ya mazishi hata huku Tanzania.

Jamaa wanahandle kila kitu hadi mourners (watakaolia msibani)
 
Nimefurahi kusikia aliwekeza kwa ajili ya familia yake,naona hao watatosha kumzika baba yao.
Haina maana unajiunga na vyama mia moja vya kufa na kuzikana lakini uwekezaji sifuri,siku mbili baada ya msiba mkeo anaanza kuhangaika ya nini?
 
Haya mambo naonaga ni ya kipumbavu tu na huchangiwa na ufukara. ..kwamba majiran wakija ndio atafufuka? Hii tabia ya kuona kua kila msiba uhudhurie hata kama haikuhusu ..
Mambo ya ya kizamani haya. Kipindi hicho watu walikuwa hawana shughuli za kufanya. Msiba watu walikuwa wanakesha wiki nzima kwa mfiwa. Mwanzisha thread andani hiyo familia ya huyo mzee imekomolewa? Sana sana hao majirani ndiyo wanahangaika kuchungulia mambo yasiyowahusu.
 
Ni ujinga tu na umaskini wetu. Watu vyakula wanakula kwa msharti hawali hovyo wanaishi kwa dozi. Nani anataka kufupisha maisha kisa watu wanalazimisha desturi? Halafu unakuta mzee alikuwa anajitoa kweli kwenye michango na kusaidia jamii ila anahukumiwa k2a kutokula. Kwanini hawakuwa wanakataa hata michango yake ili ajifunze akiwa hai?
 
Nimefurahi kusikia aliwekeza kwa ajili ya familia yake,naona hao watatosha kumzika baba yao.
Haina maana unajiunga na vyama mia moja vya kufa na kuzikana lakini uwekezaji sifuri,siku mbili baada ya msiba mkeo anaanza kuhangaika ya nini?
Hao watoto wanashindwa kujiongeza tu.
 

Yeye keshakufa hata msipomzika hakuna shida, issue ni ndugu zake nao wana Dhambi hiyo? Maana ndo mnawaadhibu!
 
Bunda kijana kafariki wazazi wanaishi huko, eti wakamzika tu ila hawawezi kusaidia familia kuandaa chakula eti marehemu hakuwa anafika msibani , eti mtu anaishi Dar msiba ukitokea awe anaenda kuzika, yaani mie nilichoka wale watu!
 
Siungi mkono watu kutojumuika na jamii,lakini jamii tujifunze kuna watu wapo busy ili wewe uishi vizuri.
upate umeme,maji ulinzi n.k
wasipokuona kwenye hiyo sijui nzengo yao wanaweka bifu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…