Mzee mmoja alikuwa haudhurii misiba leo kafariki, kinachoendelea hapa naona ni msiba wa familia tu

Mzee mmoja alikuwa haudhurii misiba leo kafariki, kinachoendelea hapa naona ni msiba wa familia tu

Jumanne Mwita

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2014
Posts
530
Reaction score
1,446
Mzee mmoja amefariki na M/Mungu alimjaalia kweli enzi za uhai wake mali kweli kweli za kutosha, katika kujumuika na nzengo Mzee hakuwa na historia ya kuhudhuria misiba ya wengine na hata kushiriki tu hakuwa anafanya hivyo enzi za uhai wake kabisa na hakuwa anajali.

Sasa ya Mungu mengi bwana leo yeye ndio amefariki toka Jumatatu. Nyumbani kwake pamewekwa maturubai na ratiba ya mazishi ila hakuna watu.

Bahati mbaya hata watoto wake mke pia walimuiga tabia. Wapo wenyewe na ndugu majirani hakuna hata mmoja na watu hawana habari napo ni kama vile hakuna kitu vinaendelea pale kila mtu anaendelea na mambo yake.

Hii stori inakuja kufanana kidogo sana na hii yangu ambayo niliishugudia.

Hii imenikumbusha mwaka 2019 nilihudhuria msiba wa babu huko Musoma kijijini cha Nyabange Wilaya ya Butiama. Nzengo walikuja kama kawaida wakashughulika kila kitu wakaandaa, lilipofika suala la kula kile chakula wakaitana baadae nikaona kila mtu anaenda kwake, kila kitu walicho andaa walikiacha kama kilivyo tukabakia ndugu tu.

Wakasema, mjomba ambae ndio msiba ulikuwa umepangwa hakuwa anakula kwenye misiba na yeye alikuwa anachangia tu. Na mke wake alikuwa anakuja kupika na kuondoka kula hawali wala hawakai kwenye msiba wa nzengo. Waligoma kabisa, sasa chakula walichokuwa wameandaa nikama sisi ndugu tusingekimaliza hata kama tungekula siku 2 bado kingebaki kingi tu. Ikabidi ndugu waitane na wakaongee na wazee mjomba akapigwa faini ya mbuzi ndio wakaja kushiriki.

Toka hapo mjomba hajawahi kuacha kuhudhuria misiba anakwambia nilichokiona sikuile ni fedheha hata kama unauwezo ile ni mbaya sana.
 
Mzee mmoja amefariki na M/Mungu alimjaalia kweli enzi za uhai wake mali kweli kweli zakutosha, katika kujumuika na nzengo Mzee hakuwa na historia ya kuhudhuria misiba ya wengine na hata kushiriki tu hakuwa anafanya hivyo enzi za uhai wake kabisa na hakuwa anajali.

Sasa ya Mungu mengi bwana leo yeye ndio amefariki toka jumatatu. Nyumbani kwake pamewekwa maturubai na ratiba ya mazishi ila hakuna watu..

Bahati mbaya hata watoto wake walimuiga tabia. Wapo wenyewe na ndugu majirani hakuna hata mmoja na watu hawana habari napo ni kama vile hakuna kitu vinaendelea pale kila mtu anaendelea na mambo yake.
So what?
 
Ila ni sawa tu maana wasioenda wamewapunguzia gharama wafiwa. Kama familia inajiweza kiasi hapo ni kununua tu jeneza, wakodi watu wachache wa kusaidia kuzika makaburini, siku imeisha.
Huwa tunacomplicate sana misiba
 
Mzee mmoja amefariki na M/Mungu alimjaalia kweli enzi za uhai wake mali kweli kweli zakutosha, katika kujumuika na nzengo Mzee hakuwa na historia ya kuhudhuria misiba ya wengine na hata kushiriki tu hakuwa anafanya hivyo enzi za uhai wake kabisa na hakuwa anajali.

Sasa ya Mungu mengi bwana leo yeye ndio amefariki toka jumatatu. Nyumbani kwake pamewekwa maturubai na ratiba ya mazishi ila hakuna watu..

Bahati mbaya hata watoto wake walimuiga tabia. Wapo wenyewe na ndugu majirani hakuna hata mmoja na watu hawana habari napo ni kama vile hakuna kitu vinaendelea pale kila mtu anaendelea na mambo yake.
Hana hasara walio na hasara ni wale wanaoishi.
Hapo ni wkamba hawana fedha, ingekuwa msiba kuna wapishi, vinywaji raia wangekuja tu.
 
Hapo shida ni pesa tu wala sio kuhudhuria misiba.

Hapo ingekua ng'ombe 1 ama 2 wako chini, michele ya kufa mtu msiba ungejaa watu na mazishi yangeenda poa tu.

Ukiwa masikini ukafa ndio unaletewa masharti ya kipumbavu kama hayo mara ulikua huhudhurii misiba, mara ulikua huchangii jumuia na ujinga mwingine ila ukiwa na pesa hata mbwa wako akifa askofu ama shehe anakuja kumuombea aende mbinguni.
 
Hivi hata mkizira kumzika faida au hasara ya nani iwapo ataanza kuwanukia ?

Wewe kama unaishi vizuri na ni mtu mwema fanya hivyo ila sio utende wema kwa kuogopa kutokuzikwa (hii imepelekea kuwa na wanafiki wengi sana) Na wa hivi hata wakikosekana kwenye msiba wako good riddance...
 
Misiba kama hiyo naipenda sana.

Familia mnaumaliza msiba fasta bila usumbufu na gharama za kulisha watu
Nani kawakwambia kuwa watu wanakuja nakwenda msibani kwa ajili ya kula? Unafikiri watu hawana vyakula majumbani mwao mpaka waanze kusubiri mtu afe ndio wakale. Kwenu wanakufa wangapi kwa wiki mpaka uhisi watu wanakuja kwa ajili ya kula.

Huna akili. Acheni kuvuta mibangi mkiwa na msongo wa mawazo.
 
Back
Top Bottom