Mzee mmoja alikuwa haudhurii misiba leo kafariki, kinachoendelea hapa naona ni msiba wa familia tu

Mzee mmoja alikuwa haudhurii misiba leo kafariki, kinachoendelea hapa naona ni msiba wa familia tu

Mzee mmoja amefariki na M/Mungu alimjaalia kweli enzi za uhai wake mali kweli kweli za kutosha, katika kujumuika na nzengo Mzee hakuwa na historia ya kuhudhuria misiba ya wengine na hata kushiriki tu hakuwa anafanya hivyo enzi za uhai wake kabisa na hakuwa anajali.

Sasa ya Mungu mengi bwana leo yeye ndio amefariki toka Jumatatu. Nyumbani kwake pamewekwa maturubai na ratiba ya mazishi ila hakuna watu.

Bahati mbaya hata watoto wake walimuiga tabia. Wapo wenyewe na ndugu majirani hakuna hata mmoja na watu hawana habari napo ni kama vile hakuna kitu vinaendelea pale kila mtu anaendelea na mambo yake.
Hiyo nzuri sana hata wafiwa hawapati gharama za mavyakula sijui vinywaji
 
Mzee mmoja amefariki na M/Mungu alimjaalia kweli enzi za uhai wake mali kweli kweli zakutosha, katika kujumuika na nzengo Mzee hakuwa na historia ya kuhudhuria misiba ya wengine na hata kushiriki tu hakuwa anafanya hivyo enzi za uhai wake kabisa na hakuwa anajali.

Sasa ya Mungu mengi bwana leo yeye ndio amefariki toka jumatatu. Nyumbani kwake pamewekwa maturubai na ratiba ya mazishi ila hakuna watu..

Bahati mbaya hata watoto wake walimuiga tabia. Wapo wenyewe na ndugu majirani hakuna hata mmoja na watu hawana habari napo ni kama vile hakuna kitu vinaendelea pale kila mtu anaendelea na mambo yake.
Wewe unadhani hiyo hali itabadilisha nini, everything in this universe is all about trading.
Niambie kwani atapata hasara Gani ama nyie mtafaidika nini, acha mtu aishi Maisha yake aliyoyachagua kwani unadhani yeye hakuwa na akili ama hakuyajua haya , binadamu tunafanya kitu huku tukijua outcome,mtu anaenda kuiba anajua ni nini kitakachomtokea , mtu anatoka na mke wa mtu ama mwanafunzi anajua kabisa, so usidhani Kama wewe una akili sana kuliko binadamu wengine, just live your life, kwani zengwe inasaidia nini? Kuna kampuni za kuzika zinakuja zipo ulaya na huku zipo, chukua mzoga mochwari kazikeni kwani kumuenzi marehemu kuwa ndio mnapata baraka Gani ama mnapoteza nini , ama yeye pia ananufaika nini ama amepoteza. Afrika bana inabidi utoe salamu usipotoa unaringa, masikini anataka kufarijiwa kwa kupewa human company, jiulize why diamond alihamia masaki
 
Nimemuuliza hivo hivo mkuu
 
Sio misiba tu ndugu, Watanzania tunacomplicate ubatizo, kutahiri kijana wa kiume, kuvunja ungo kwa binti, kipaimara,komunio, mahafali, birthdays, sikukuu, kuagwa kwa mabinti wanaoenda kuolewa na ndoa.

Kiujumla, ni Tanzania pekee kila jambo limtokealo mtu linatafutiwa sherehe.
Arobaini this Arobaini that, waswahili wanapenda shughuli kwenye kila jambo
 
Juzi kati mtaani kulikuwa na msiba, mwili ukatolewa ndani tayari kwa safari ya kwenda kuzika kitongoji cha mbali. Kuna watu walitaka tule kwanza ila wengi wakasema haina haja ya kula, tukaenda kuzika bila kula. Tuliporudi kutoka mazikoni ndio tukapewa chakula. Chakula kikawa ni ugali kwa mboga za majani tu, wengine tukajitenga kula ugali kwani ugali tumekula nyumbani ya nini kula tena? Tuliambiwa kula msibani ni lazima usipokula na kwako hawaji kula utaachiwa vyakula ule mwenyewe kwa kuwa huwa huli kwenye misiba ya wenzako hivyo ni lazima ushiriki kula hata kama ni uji
 
Mzee mmoja amefariki na M/Mungu alimjaalia kweli enzi za uhai wake mali kweli kweli za kutosha, katika kujumuika na nzengo Mzee hakuwa na historia ya kuhudhuria misiba ya wengine na hata kushiriki tu hakuwa anafanya hivyo enzi za uhai wake kabisa na hakuwa anajali.

Sasa ya Mungu mengi bwana leo yeye ndio amefariki toka Jumatatu. Nyumbani kwake pamewekwa maturubai na ratiba ya mazishi ila hakuna watu.

Bahati mbaya hata watoto wake mke pia walimuiga tabia. Wapo wenyewe na ndugu majirani hakuna hata mmoja na watu hawana habari napo ni kama vile hakuna kitu vinaendelea pale kila mtu anaendelea na mambo yake.

Hii stori inakuja kufanana kidogo sana na hii yangu ambayo niliishugudia.

Hii imenikumbusha mwaka 2019 nilihudhuria msiba wa babu huko Musoma kijijini cha Nyabange Wilaya ya Butiama. Nzengo walikuja kama kawaida wakashughulika kila kitu wakaandaa, lilipofika suala la kula kile chakula wakaitana baadae nikaona kila mtu anaenda kwake, kila kitu walicho andaa walikiacha kama kilivyo tukabakia ndugu tu.

Wakasema, mjomba ambae ndio msiba ulikuwa umepangwa hakuwa anakula kwenye misiba na yeye alikuwa anachangia tu. Na mke wake alikuwa anakuja kupika na kuondoka kula hawali wala hawakai kwenye msiba wa nzengo. Waligoma kabisa, sasa chakula walichokuwa wameandaa nikama sisi ndugu tusingekimaliza hata kama tungekula siku 2 bado kingebaki kingi tu. Ikabidi ndugu waitane na wakaongee na wazee mjomba akapigwa faini ya mbuzi ndio wakaja kushiriki.

Toka hapo mjomba hajawahi kuacha kuhudhuria misiba anakwambia nilichokiona sikuile ni fedheha hata kama unauwezo ile ni mbaya sana.
Mm ndio napenda hivyo misiba isiwe na mambo mengi watu wachache mambo yanaisha faster ata msiba wangu natamani usiwe na lundo la wanafki yaani ndugu wachache tu inatosha kabisa.
 
Hao wanaojaa kwenye misiba hasa huku uswahili hata ukiwachangisha wote upati pesa ya kulipia tent siku mbili.
Wameipunguzia gharama familia hio,unadhani wangetumia gharama kiasi gani kulisha watu msibani
Huku kwetu vijana wamejaa msibani kusubiri msosi, kazi yao ni kucheza karata na hakuna la maana wanalofanya
 
Mleta mada namfananisha na wapumbavu fulani wanasemaga usiposhiriki jumuiya, kanisani na kutoa zaka hatuji kukuzika 🤣🤣🤣

Yani wanajiona wajanja sana kumbe kumbe wangejua ninavyowadharau wasingeamini
Ni mbea pia
 
Afadhali hii mada imenzishwa ilikuwa inanikera sana mambo ya kanda hii
Ni ujinga na umasikini kuchunguliana.Kwani ni lazima mtu ale kwenye msiba? kwa tabia hata mimi mmoja wapo huwa sipendi kula nje ya nyumbani kwangu.
Mambo haya haya ya kula msibani yuko mzee mmoja aliwekewa sumu.
Kama mzee alikuwa haendi msibani nyie mkaacha kwenda hapo mtakuwa mnamuadhibu yeye au familia yake?.Endapo familia nao walikuwa hawaendi naweza kuona sawa wakiziliwa.
Ila niwaambie kitu mtu mwenye ukwasi huwezi shindana naye na hizo shillingi 1000 zetu mnazochanga hazifikia hata laki mbili.
Niliona msiba mmoja kanda ya hii mzee kafiwa na baba yake jamaa alikuwa na ukwasi wa kutosha kukatokea jambo kama hilo alichofanya alikwenda kuchukua buffe ya chakula na waliohudhuria ni ndugu zake wachache hawazidi 30 waliaji alikwenda kukodishi jamaa akapiga gari moto akapeleka marehemu wake kwao napahifadhi yale masufuria ya zengo akawarudishia.
Wakati mwingine mtu hahudhuriagi misiba ya zengo kutokana na nature ya shughuli zake nitoe mfano mtu anafanya kazi anasafiri na mabasi atakaa nyumbani muda gari au hawa waheshimiwa wetu mawaziri,makatibu,viongozi wa chama muda wote kusafiri.
Ifike mahali tubadilike watanzania tunawaza kula tu.Kingine ninachochukia kanda hii mtu anakuletea chakula kwenye sahani amekujazia anajua unakula kiasi gani chakula kwa sasa ni self service.

Kingine ni sisi watanzania kwa ujumla wake tumezidisha mno michango ya harusi unakuta mtu ana kadi sita anatakiwa atoe michango inazidi mshahara wake.
Tubadilike watanzania kuchangia harusi halafu ukiomba mchango harambee shule ya mtoto wako mtu anakuambia ni mzigo wako.
Mgonjwa akiumwa ni mzigo wako siku akifa anachinjwa hadi ngombe mkubwa dume na watu wanakula wanasema marehemu alikuwa mtu mzuri sana hii ni shida ya Tanzania
Nenda hapo Kenya hakuna ujinga huu
Nenda nchi ya Ghana mtu hachangiwi harusi ila siku ya harusi zawadi zinazidi michango ya harusi
 
Back
Top Bottom